Kwa graduate wa ifm-please read

Kingmairo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
4,936
3,533
Katika pekuapekua zangu za magazeti ya leo, nimepita katika gazeti la Mwananchi na nikakuta tangazo linalowata graduates wote wa IFM waliomaliza mwaka jana (2011) ambao wamechukua awards (vyeti) vyao wavirudishe mara moja kwasababu ya tatizo/makosa ya kiufundi yaliopo katika awards hizo. Sambamba na kuvirudisha, pia wamesitisha utoaji wa vyeti kwa wale ambao hawajachukua bado.

My take:
Graduation ilikuwa mwaka jana kama sikosei na hadi leo ni takribani miezi sita toka graduate astahili kupewa cheti. Je muda wote huu umepita bila kulibaini hilo kosa la kiufundi?
Pili, kama mtu ameshakitumia na pengine kapata hadi kazi kwa kigezo cha cheti kilicho na makosa na ikabidi kazi nayo isitishwe, si kumhujumu mwanafunzi?
Kwa kuwa wamesitisha utoaji wa vyeti kuanzia certificate, diploma hadi degree, vipi kwa wanafunzi wanaotegemea kuomba chuo kwa vyeti hivyo hususan diploma na certificate. Deadline za vyuo vingi ni may/june.
Huu ni udhaifu ambao kutokana na muda mrefu kupita inaonesha hawapo serious kabisa.
 
Back
Top Bottom