Uchaguzi 2020 Kwa Gharama yoyote Tutaulinda Umoja Wetu wa Kitaifa: Sera ya Majimbo ni Haramu ya kila Mtanzania

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Na:
McWenceslaus

Leo nimekuja nikiwa na ujumbe maridhawa wenye lengo la kutukumbusha kuhusu malengo ya Muungano wetu na utawala wa umoja wa kitaifa ambao tumekuwa nao kwa zaidi ya miaka 56 sasa!

Kabla sijaendelea naomba tujikumbushe Mambo machache yenye kuhusiana na ajenda hii ya leo. Kwa hiyo nitarudi katika miaka ya 1780's katika nchi ya Muungano wa Majimbo ya Marekani (USA).... Napenda nianze kama ifuatavyo, kuyaunganisha majimbo ya kaskazini mwa Marekani, iliwachukua zaidi ya miaka 6 ili kusubiri maamuzi ya majimbo ya kaskazini mwa Marekani yaingie katika Muungano kwa hiari, bahati mbaya haikuwa hivyo.

Marekani iliamua kutumia nguvu ya ziada hata kuiingiza nchi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ili kuyalazimisha majimbo ya kaskazini kuingia kwenye muungano huo. Kwa miaka 4 mfululizo Baba wa Demokrasi Marekani Rais Abraham Lincoln alitumia nguvu ya dola ili kuwaunganisha watu na kukomesha utumwa ndani ya Marekani. Hatimaye mwanzoni mwa mwaka 1865 majimbo ya kaskazini ya Marekani yaliingia kwenye Muungano wa kitaifa.

Stori hiyo ya kuiunganisha Marekani na kuwa taifa moja lenye nguvu, haitofautiana sana na historia ya kuiunganisha Tanzania na kuwa nchi yenye nguvu kusini mwa nchi za Jangwa la Sahara. Ndio kusema kwa Tanzania ilichukua takribani miaka 9 (1955-1964) ili kujenga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa miaka 8 ilitazamiwa kuwa Muungano huo ungefanyika kwa hiari kwamba hautaingiliwa na mwarabu wala muingereza (1955-1963), bahati mbaya haikuwa hivyo. Badala yake mwaka 1 ilimtosha Baba wa Demokrasia Zanzibar Sheikh Abeid A. Karume kutumia nguvu kiasi ili kuwezesha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Na hiyo ni baada ya kukubali nguvu kutumika kwa kufanya mapinduzi matukufu ya 12/01/1964, na miezi 3 na wiki 2 baadaye Muungano wa Tanzania ukazaliwa.

Kwa hiyo, tunajifunza kwamba ili Muungano uundwe na ulindwe ni lazima kuwepo na gundi yenye nguvu ambao utashikilia Muungano huo, gundi hiyo ikiligea hakuna Muungano utakaodumu. Gundi ambayo inashikilia Muungano wetu imetokana na utayari wa Viongozi wetu na Uzalendo wa Viongozi wetu kwa kuupenda Muungano na kuona faida zake kwa vizazi vya sasa na vya baadaye.

Marekani kwa miaka zaidi ya 200 sasa, hakuna Rais ye yote aliyewahi kucheza na kuchekeana na wanasiasa wamarekani wanaozungumza kuvunja Muungano wao, ama awe ni m-demokratik au m-Repablik. Wote wako na nia na dhamiri njema juu ya Muungano wao. Wakitambua kuwa umoja wao kama waamerika unawafanya waweze kuwa na nguvu ya kumaliza matatizo yao wenyewe na hasa yale ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Kama vijana watanzania wazalendo kwa nchi yetu na Muungano wetu, ni lazima tuwaambie watanzania waachane na habari za kugawanywa na kuondolewa umoja wao kwa kutumia jina MAJIMBO. Ni sera ambayo inataka kurudisha nchi ilipotoka kabla ya uhuru, ambapo wakoloni waliwagawa watu kwa utawala wa kimajimbo, kwamba baadhi ya majimbo ambayo yalikuwa hayana rasimali za kutosha yaliachwa nyuma na watu wake waliishi katika hali ya umasikini wa kutupwa, mfano mikoa ya kanda ya kati yaani Dodoma na Singida; na kwa majimbo ambayo yalikuwa na rasimali za kutosha, ndizo hizo zilipewa kipaumbele na kwamba watu wake waliishi katika hali ya maisha mazuri na waliweza kupata huduma zote muhimu za jamii.

Watanzania ni lazima tufahamu kuwa haijalishi changamoto tunazozipitia kama nchi, kwamba zitaweza kuharamisha njia ya umoja wetu wa kitaifa kuwa ndio njia itakayoweza kutuondolea matatizo yetu ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ni katika utawala nje ya utawala wa majimbo, watanzania wa mahala popote ndani ya Tanzania wataweza kufaidika na rasilimali za Tanzania na sio za jimbo fulani. Tunataka mapato ya mlima Kilimanjaro ukamsomeshe kijana wa Mtwara, tunataka Gesi ya Mtwara ikawashe umeme Mara, tunataka kahawa ya Kagera, ikanywewe Dodoma n.k.

Vijana wazalendo watanzania wenzangu, tunayo nafasi moja na ya adhimu yenye ustaarabu tele ndani yake, nayo ni siku ya kupiga kura tarehe 28/10/2020 siku ya jumatano. Ni siku hiyo ndio ambayo tutaitumia kuwaadhibu wanasiasa wote wenye lengo la kutugawa kwa jina la SERIKALI ZA MAJIMBO kwa kumchagua Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Chama cha Mapinduzi kuiongoza na kuitawala hii nchi kwa jina la umoja wa kitaifa Kama Tanzania, na ambao wataulinda utanzania wetu; Muungano wetu ndio utanzania wetu. Tukishindwa katika njia hiyo, basi ni budi tukubaliane kuwa tutakuwa na nguvu ya ziada ambayo ni lazima tuilipe katika kurudisha umoja wetu wa kitaifa, wanasiasa wenye sera za kutugawa ni maadui wangu na ni maadui wako, vilevile ni maadui wa taifa hili la Tanzania.

#magufuli5Tena
#magufuliNimafanikio

Sauti ya Mdodomia.
10/10/2020
 

Attachments

  • Screenshot_20201010-065800~2.png
    Screenshot_20201010-065800~2.png
    29.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_20201008-192827.png
    Screenshot_20201008-192827.png
    162.7 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom