Kwa fikra za kibinadamu, je Mungu hakuwaonea Adamu na Eva?

MACHALE

Senior Member
May 22, 2016
163
53
Heshima kwenu viongozi napenda kuwasalimu wote. Na zaidi wale waaminio hawa waaminio napenda kuwataka radhi kwani swali langu laweza kuwakera. Naam swali hili hata Mimi sikupenda kuliuliza lakini imenibidi kuliuliza.
Kwani nikupitia kuuliza ndipo nitakapo pata elimu zaidi.

Swali langu lina uliza "Je mungu hakuwaonea au kuwapa adhabu Kali kuliko kosa walilotenda Adamu & Eva ??"

Najiuliza hivi kwani katika vitabu vitakatifu, tunaambiwa sisi tutahukumiwa, kwani sisi tuna utashi na akili. Kwamba sisi tuna tambua mema na mabaya,

Lakini kwa Adamu & Eva mambo hayakuwa hivo, kwani Adamu & Eva wenyewe hawakuwa na ufahamu wa mema na mabaya na ndiyo maana walijitambua baada ya kula tunda.

Hii ni ishara kwamba walitenda kosa bila ya kujua kwani walikuwa hawawezi kutofautisha mema na mabaya.

Waweza kusoma kitabu cha mwanzo katika biblia au kwenye quran, utaona wazi kwamba walijitambua baada ya kula tunda ina maana hapo kabla walikuwa hawajitambui sasa kwanini adhabu Kali iliwakuta??.
 
Mungu aliwaumba Adam na Eva wakiwa wakamilifu wenye UHURU wa KUCHAGUA.
 
Hakika Mungu aliwahurumia ndio maana akatengeneza mpango wa kuupatanisha uzao wake(jamii ya binadamu) na Mungu hata kumtuma mwanaye pekee aje atukomboe. Baada ya YESU kufa pale Kalvari swali la dhambi likawa limemalizwa nasi tunaweza kuwa na ushirika tena na Mungu kupitia kwa Ile Damu iliyomwagika msalabani.

Lakini naomba nitoe angalizo mambo ya Kimungu kwa fikra za kibinadamu ni kama hayapo vile. Kwakuwa Imeandikwa Hekima ya Mungu ni upumbavu kwa wanamu halikadhalika Hekima ya mwanandamu ni upumbavu kwa Mungu. Hivyo Jaribu kulichukulia kiroho kuwa mtu asiye na dhambi wala hatia alikufa ili Mimi na wewe tuwe na ushirika na Mungu tena
 
Kama dhambi zilimalizika au ziliishia pale msalabani.Je? Kwa kipindi hiki zinaendelea au kwa sasa hakuna dhambi.
 
Kama dhambi zilimalizika au ziliishia pale msalabani.Je? Kwa kipindi hiki zinaendelea au kwa sasa hakuna dhambi.
Dhambi ni Jambo ambalo adhabu yake hakuna mwanandamu awezaye kuilipa. Adhabu yake ni Mauti na kwakuwa Mauti ni moja na uzima ni mmoja tu ambao ni uzima wa milele. Sasa YESU alipokufa ambaye pekee ndiye aliyestahili kufa kwa ajili yetu akaweka njia ambayo kwayo twapata Uzima wa milele na kupita kutoka mautini. Usipokuwa katika njia hiyo huwezi kamwe kuwa na uzima wa milele. kwa hiyo Dhambi ipo na itakomeshwa mwishoni baada ya Shetani kuhukumiwa na kuteketezwa kwa moto.
 
Kama dhambi zilimalizika au ziliishia pale msalabani.Je? Kwa kipindi hiki zinaendelea au kwa sasa hakuna dhambi.
Kwasasa tumepewa mwanga wa kuzitambua dhambi kwa wepesi kupitia amri za Mungu hivyo Amri za Mungu ni kioo cha kutumlikia kuwa tusitende dhambi
 
Kwasasa tumepewa mwanga wa kuzitambua dhambi kwa wepesi kupitia amri za Mungu hivyo Amri za Mungu ni kioo cha kutumlikia kuwa tusitende dhambi
Zimebaki story hakuna action yoyote siku hizi tujadiliane tu hapa jamvini kana sehemu ya kupeana na kuongeza maarifa lakini sisi wote ni watenda dhambi na tumepungukiwa na utukufu wa Mungu
 
Kwa mujibu wa maandiko Adam na Hawa walikua ni wakamilifu kwa sifa zote za ukamilifu wa kibinadam. Kwa yale walioyafanya wakiwa bustanini waliyafanya kwa utashi wa nafsi zao, ikumbukwe kabla ya hapo Mola wao aliwatahadharisha juu ya hayo yote. lakini kwa khofu ilio ingia ktk nafsi zao kwa kumsikiliza mwenye kutia khofu ktk nafsi za watu ili wamuasi Mola wao, mwisho walijikuta wakitenda lile ambalo Mola wao kawakataza, na baada ya kutenda ndipo wakajutia kwa kutenda lileambalo Mola wao aliwakataza. Walijutia makosa yao na wakaomba msamaha kwa Mola wao na Mola wao aliwasamehe, baada ya hapo Mola wao aliwabadilishia mazingira ya maisha kwa kuwateremsha duniani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom