Kwa Fikra, Siasa na Sera hizi; Tanzania itabaki maskini!

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
Fikra,siasa na sera hizi zinazo tumiwa na viongozi na kuwaaminisha watanzania zitaifanya Tanzania ibaki maskini na tegemezi milele.

Leo nimekumbuka tangia nianze kusoma huko primary nilifundishwa kuwa KILIMO NI UTI WA MGOGO WA TAIFA. Mpaka leo nimemaliza kidato cha nne bado ninaambiwa kauli, fikra na sera hiyo hiyo.

Najiuliza kama kilimo ndo uti wa mgongo mbona mpaka leo maskini wengi ni wakulima?

Kama tunategemea kilimo sasa tutashindanaje na mataifa mengine na je hii si inaendelea kutufanya tegemezi wa watu wenye viwanda ambao wao ndo wanapanga bei?

NADHANI NI WAKATI MUAFAKA WA KUSEMA UTI WA MGONGO WA NCHI YETU NI VIWANDA KULIKO KILIMO.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,644
116,816

Mkulima analima kwa jembe la mkono, kutoa mazao shambani mpaka kufikisha sokoni mkulima anakutana na barriers zaidi ya mbili na zote hizo lazima atoe kitu kidogo. Mkulima huyu akifika sokoni na mazao ya kuuza anapangiwa bei inayomkandamiza ukizingatia mbolea ya ruzuku imeuzwa yote na vingozi macheki bob.Namna pekee ya kunufaika kwa mkulima wa Tanzania ni kuuza mazao nje ya nchi ila ndo hivyo mipaka imefungwa ili tupangiwe bei kandamizi ya kuuza mazao yote hapa Tanzania.
Hakika naamini ipo siku wakulima tutaingia barabarani na majembe yetu alafu tutachekana sokoni.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Hakika Watanzania tutaendelea kuwa maskini si kwa sababu ni wavivu au hatuwezi kilimo bali kwa kuwa viongozi wetu wameamua kuwa Watanzania walio wengi ambao ni wakazi wa vijijini kwa asilimia themanini [80%] wataendelea kuwa masikini daima.

Tunaitaji Kiongozi Jasiri mwenye uthubutu wa kusimamia yale yote yanayomfanya mpaka Mkulima Maskini wa Tanzania kuonekana kuwa hana nguvu na uwezo wa kufanya mapinduzi kilimo ya kijani [Green Revolution] ndani ya Nchi yake kwa gharama zozote zile.Tunaitaji Kiongozi atakae weza kuondoa siasa kwenye kilimo bali aweze kuweka sayansi kwenye kilimo.

Safari hii itakayo endeswa na JASIRI ASIYEA ACHA ASILI ya kujikwamua kutoka kwenye makucha ya kifo cha KILIMO CHA KUSABABISHIWA NA KUJISABABISHIA kutokana na miongozo ya Watawala wetu basi na vivyo hivyo kujikwamua kwenda kwenye maono [vision & Mission] ya KUIBUKA KAMA MAGWIJI WA KILIMO KWENYE NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA kwa kuweka muda [Time limit] na mikakati [Strategies] sahihi ya kufikia malengo ya KILIMO WA TAIFA.

Hayo Mapinduzi ambayo wengine tunayoyaota yatawezekana kwa kuwa VITA HII NIA TUNAYO,SABABU TUNAYO NA UWEZO TUNAO tunachoitaji ni KAMANDA/JEMADALI/MTEMI/KOMANDO/KINGANGANIZI/ ambae hatasita kunyofoa macho ya mtu yoyote yule atakae yumbisha nguvu za Serikali katika kusimamia MAPINDUZI YA KILIMO [GREEN REVOLUTION] na atakae tuongoza akionyesha njia kwa kuwa MAPINDUZI NI VITA na SIO SIASA AU LELEMAMA.Tunaitaji kiongozi ambae siku zote apokee taarifa za Mapinduzi ya kilimo na maendeleo yake yeye mwenyewe wakati mwingine akiwa shambani [Site] analima na sio kwenye ofisi, kwa kuwa kamanda wa vita daima yuko mstari wa mbele kwenye eneo [Field] la vita ili aonyeshe mbinu na mikakati ya kumshinda adui na kuwapa mori makamanda wasaidizi na wapiganaji wake ambao ndio Wananchi wakulima kupigana kwa moyo wote.

TUNAITAJI KUONA PAMBAZUKO LA VITENDO KWA KUWA KAMA NI MAKALABRASHA YA KILIMO NA SEMINA ZIMEAANDIKWA SANA SANA NA WATU WA MAOFISINI WAMESAFILI SANA KUFANYA TAFITI KILICHOBAKI NI UTEKELEZAJI KWA VITENDO NA KWA NGUVU ZOTE.

MURA UNAKUJA MUCHINI NA CHEMBE,UNAKUCHA KULIMA LAMI MURA, MUCHINI NI FYETI MURA.KWELI MASWALA YA KILIMO YANALETWA KUPIGIWA KAURI MBIU MUCHINI BADALA YA SHAMBANI WALIKO WAHUSIKA, HIYO HAKIKA NI KUWATUKANA WAKULIMA WETU KUWA HAWAUSIKI KATIKA MAPINDUZI HAYO.

Tumechoka tunaitaji mabadiliko ya kifikra kuona kuwa mambo yote yanayohusu KILIMO CHA WATANZANIA yatoke kuwa yanajadiliwa MIJINI NA MAJIJINI mwetu,wakati tunaelewa wazi kuwa mijini sio mahali pake,mijini watu wanaangaika na vyeti vya maofisi na uchuuzi wa vitu.Mambo yote ya KILIMO NA SHUGHUKI ZOTE ZINAZOHUSU KILIMO yapelekwe kwa Wananchi Wakulima huko waliko VIJIJINI MWETU.Hata kama ni Semina za Upandaji bora kwa wataalamu zitengewe sehemu na kuwekwa kambi huko huko vijijini na waandishi watok Dar es Salaam au Arusha mjini waeende vijijini [Rural Areas] ndani kuchukua taarifa hizo kisha wazilete makao makuu kwa ajili ya kusambazwa kama habari kwenda kwa Umma.

Tulipofika Wananchi wamesha anza kumjua adui yao,kwa kuwa Umaskini wa Mwananchi Mkulima wetu umefika sehemu umeibua matamanio ya kujiangalia yeye binafsi AMEMKOSEA NINI MUNGU,lakini Wanafalsafa walipata kusema UTAWADANGANYA WATU FULANI WAKATI FULANI BALI UWEZI KUDANGANYA WATU WOTE WAKATI WOTE.
 
only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,524
Ni kauli mbiu tu mkuu,uwa zinabakia kwenye midomo na kwenye makaratasi............usitegemee hata tukisema "VIWANDA UTI WA MGONGO" ndio mabadiliko yatakuja,kama hakuna vitendo ni porojo tu.....chamsingi ni kuweka kwenye vitendo mambo yetu...
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,330
Mkuu kila kitu kinaenda na mtaji ulionao..., wenye mafuta waache wafanye biashara, sisi wenye ardhi ya kumwaga yenye rutuba unataka tufanye nini na hio ardhi..?

Kinachotakiwa ni kutumia hiyo ardhi vizuri na kuzalisha kisasa na kupata miundo mbinu ya kufikisha mazao sokoni.., (na sio kwamba yafike kama nafaka, bali tunaweza kuwa na viwanda vidogo huko vijijini ili kuongeza value ya mazao na yafike kwa mlaji yakiwa processed tayari..

Viwanda tulikuwa navyo vya nguo, beef, n.k. ila sasa tunataka kununua kila kitu kutoka nje..!! mfano viatu hivi hatuna ngozi..?, nguo hivi hatuna pamba..?

Mkuu in short kitu kitakachotutoa kwenye hili janga inabidi twende tukachunguzwe vichwa vyetu sababu tunafikiri in reverse...

Tuache wengine watangeze magari na ma-tv sisi tuna malighafi ready made ambazo zina demand ulimwengu mzima Tanzania ina kila kitu vyanzo vya maji, rutuba, na ardhi ya kutosha..., lakini yanayotokea utafikilia tupo katikatika ya jangwa..!! kweli sijui ni nani alituloga!!!
 
mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
185
Inawezekana hizo kaulimbiu ni nzuri sana tatizo ni wasimamizi (Magamba na viongozi wake) ndiyo bomu
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
Tatizo linatoka wapi hasa?Ebu angalia leo unawambia wananchi kuwa kilimo kwanza lakini mashuleni somo la kilimo sio lazima na kama kuna shule zinafundisha kilimo ni chache,sasa utapata wapi watekelezeji wa hiyo sera kama aundai watekelezeji na ujuzi kuanzia ngazi ya chini?Somo la kilimo linabidi angalau liwe la lazima kama kweli kilimo ndo uti wa mgongo kwa niaba ya siasa na sera za Tanzania. Jamani ufike wakati tujiulize where are we,what we are,where should we be and go.VIWANDA KWANZA.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mtaji wa CCM ni hao masikini so wanaongea tu maneno lakini kuwakomboa hawataki maana wanajua watasomesha watoto ambao baada ya kupata Elimu watakuwa threat sana kwa ustawi wa CCM .
 
Maarko

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,178
572
Kuna azimio moja silikumbuki la mwaka gani,linasema Siasa ni Kilimo,hilo ni tatizo ni mpaka ijulikane kua Kilimo siyo Siasa bali Kilimo ni Sayansi hapo tutaweza kusonga mbele,
Tuyakatae Mgamba hiyo ndiyo njia pekee ya kufika tunakotaka,Ccm wanatumia ujinga/umaskini wa watanzania kama mtaji wao hawawezi kuwasaidia katika kilimo cha Kisayansi kwakua wanajua wakulima masikini wakifanikiwa ndiyo mwisho wa utawala wao!
 
maulaga

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
472
120
Mkuu, unategemea maendeleo yoyote katika nchi ambayo viongozi wake wameamua kuacha kufikiri na kusubiri fikra zitoke Ulaya na Marekani? Hao unaowaita wakulima wameaminishwa na viongozi wa taifa hili kuwa maendeleo bila wafadhili na wawekezaji hayawezekani. Wanaambiwa wawape wawekezaji ardhi yao ili wapate ajira ktk mashamba yatakayoanzishwa na wawekezaji hao.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
13,122
14,043
Fikra,siasa na sera hizi zinazo tumiwa na viongozi na kuwaaminisha watanzania zitaifanya Tanzania ibaki maskini na tegemezi milele.

Leo nimekumbuka tangia nianze kusoma huko primary nilifundishwa kuwa KILIMO NI UTI WA MGOGO WA TAIFA. Mpaka leo nimemaliza kidato cha nne bado ninaambiwa kauli, fikra na sera hiyo hiyo.

Najiuliza kama kilimo ndo uti wa mgongo mbona mpaka leo maskini wengi ni wakulima?

Kama tunategemea kilimo sasa tutashindanaje na mataifa mengine na je hii si inaendelea kutufanya tegemezi wa watu wenye viwanda ambao wao ndo wanapanga bei?

NADHANI NI WAKATI MUAFAKA WA KUSEMA UTI WA MGONGO WA NCHI YETU NI VIWANDA KULIKO KILIMO.

Dogo,

Kwa vile umemaliza form four leo, ninaomba unipe nafasi ya kukumbusha tulikotoka; mimi nilimaliza form four iliyokuwa inaitwa darasa la kumi na mbili zamani sana.

Tamko la Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa hili ni la zamani sana; lilianza wakati wa mpango wa kwanza wa mwaendeleo ya miaka mitano ambao ulikuwa unadumu kuanzia mwaka 1964 hadi 1969, ingawa ulikuwa extended hadi mwaka 1972; hata hivyo mwaka wa 1974 tamko hilo liliongezewa nguvu zaidi kwa nembo ya Azimio la Iringa la Siasa ni Kilimo kutokana na njaa kubwa iliyolikumba taifa hili baada ya shughuli za kilimo kuwa zimevurungwa na operesheni vijiji.

Baada ya mpango wa kwanza wa miaka mitano, mweleko wa Tiafa hili ulikuwa ni wa kuwa na taifa la viwanda kwa ajili ya kusindika mazao tunayolima. Ndiyo maana Serikali ilijenga viwanda vingi sana kati ya mwaka 1974 hadi mwaka 1985 ambavyo vyote vilikuwa ni vya kusindika mazao ya wakulima. Unfortunately, baada ya vita ya Uganda ambayo ilivuruga sana uchumi wa nchi hii, lile lengo la ujenzi wa viwanda likadorora na kufikia kufutika kabisa tangu Nyerere atoke Madarakani mwaka 1985. Sera ya kwanza kabisa iliyoletwa na rais Mwinyi mwaka 1985 ilikuwa ni ya kubinafsisha viwanda vyote vilivyojengwa na serikali ya Nyerere. Naweza kujua ni kwa nini Mwinyi alifanya hivyo wakati huo ila sioni sababu ya kwa nini bado tunafanya hivyo leo hii, miaka ishirini na sita baadaye ( karibu sawa na ile aliyotumia Nyerere kujenga viwanda hivyo.)

Baada ya vita ya mwaka 1979, nchi hii imebaki haina mwelekeo kabisa kwa vile viongozi waona mbali hawapo tena. Kwa hiyo nakubaliana nawe kuwa Kilimo siyo njia yenye nguvu kuiendelza Tanzania katika mazingiora ya leo, ila ni njia imara ambayo iwapo tungeindeleza kwa kulima na kusindika mazao yetu kabla ya kuyauza tungekuwa tunatengeza ajira nyingi sana kwa watu wetu.

Muyumbo wa uchumi duniani miaka ya hivi karibuni nadhani umesaidia watu kuona kwa kina kuwa mwelekeo wa Nyerere katika mazingira yetu ya vurnerability wakati ule ulikuwa sahihi. Kwa leo hii unaona jinsi ambavyo tumekuwa hatuna sauti tena juu ya raslimali zetu.
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
Hatua gani zifanyike sasa baada yakushindwa jitahada za 5year Development Plan.Tunakumbushana sana yaliyopita,mfano leo hii mkuu wa inji alipitisha pamoja na bunge the 5Dev. Plan 2011-2016 ikiwa imelenga kwenye viwanda,kilimo na elimu.Sasa ninajiuliza watanzania wangapi wamepata mwongozo huu?Je vijana ambao wako mashuleni na ambao tumemaliza wangapi wanauelewa huu mwongozo.Tukisema tumekosa viongozi wa kusimamia haya siyo sahii kwani na sisi tunaweza kutoa mahamzi ya kuingoza nchi yetu TANZANIA VIWANDA KWANZA.
 
Simcaesor

Senior Member
Jul 15, 2011
112
8
kwanza unayosema ni ya kweli lakini hii kauli ya ukweli zaidi isipokuwa shida ipo katika aina ya kilimo ambacho watanzania wengi wanakifanya tasmimini inaonesha kwamba katika ardhi inayofaa kwa kilimo tanzania ni asilimia 0.7 tu ndiyo inalimwa, kilimo ni kweli kabisa ni uti wa mgongo kama large scale agriculture itafanyika. pili hakuna maendeleo ya viwanda kama hatutalima malighafi tutapata wapi, kumbuka asilimia 80% ya malighafi ya viwanda zinatoka katika kilimo.
 
Kitu kinacho nisukuma na kukubari VIWANDA KWANZA nikama ifatavyo. 1.Viwanda vitaleta soko za raw materials kitu ambacho kitafanya uzalishaji kuongozeka kwenye kilimo
2.Viwanda vingine vitajikita katika kuzalisha farming implements ambazo wakulima watatumia na kuongeza thamani ya mazao
3.Viwanda vitatoa ajira na siyo kutegemea kilimo tu
4.Tanzania itakuwa tayari kushindana na nchi nyingine kwenye soko la dunia kwa bidhaa zitakua ziko kwenye good quality
5.Mkulima atanufaika kwani ataweza kuuza mali zake kwenye soko lenye tija.
Tukiangalia nchi ambazo zimefanya vizuri na kuupunguza umaskini wamefanya hivyo kwa pamoja huku viwanda huku kilimo anzia Britain Agralian Revolution,Brazil,SINO-Green Revolution etc
VIWANDA KWANZA .
 
Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,571
234
Fikra,siasa na sera hizi zinazo tumiwa na viongozi na kuwaaminisha watanzania zitaifanya Tanzania ibaki maskini na tegemezi milele.

Leo nimekumbuka tangia nianze kusoma huko primary nilifundishwa kuwa KILIMO NI UTI WA MGOGO WA TAIFA. Mpaka leo nimemaliza kidato cha nne bado ninaambiwa kauli, fikra na sera hiyo hiyo.

Najiuliza kama kilimo ndo uti wa mgongo mbona mpaka leo maskini wengi ni wakulima?

Kama tunategemea kilimo sasa tutashindanaje na mataifa mengine na je hii si inaendelea kutufanya tegemezi wa watu wenye viwanda ambao wao ndo wanapanga bei?

NADHANI NI WAKATI MUAFAKA WA KUSEMA UTI WA MGONGO WA NCHI YETU NI VIWANDA KULIKO KILIMO.

Kuna mkulima na mlima wima.
Sisi hatuna wakulima tuna walima wima.
Sasa hawa walima wima watalipeleka wapi taifa?
Ndo walima wima wanaitwa wainua mgongo?

Tunakosa mipango inayopangika na kutekelezeka.

Raisi wenu amekuwa mzururaji,hana maono ya mbali,
Kwenda kupga picha na wakina husein bolt,50cent inamaslai gani na kilimo kwanza?au kwa walima wima?
Napata mashaka.
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Umenkumbusha mbaliiii... Enzi zile somo la siasa primary unapewa katiba ya magamba kuikeremua, lol, nadhani ujinga wa watz ulianzia pale. Mambo ahadi za mwanachama...
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
hivo viwanda unasema ni viko wapi? hoja yako ni nzuri, lakini kubadili slogan na kujiita nchi ya viwanda hapo sikuungi mkono kwa sababu viwanda vingi si vya wazawa na mbaya zaidi vinazalisha biskuti na peremende tena kwa kiwango duni.
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,039
hivo viwanda unasema ni viko wapi? hoja yako ni nzuri, lakini kubadili slogan na kujiita nchi ya viwanda hapo sikuungi mkono kwa sababu viwanda vingi si vya wazawa na mbaya zaidi vinazalisha biskuti na peremende tena kwa kiwango duni.

Viwanda havitoke mbinguni ni sisi wenyewe kuwa wa kwanza kushinikiza na kusimamia viwanda vinajengwa kuanzia vidogo hadi vikubwa mkuu.VIWANDA KWANZA.
 
Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,706
1,788
Halafu kilimo chenyewe hutegemea mvua zisizo na uhakika. Mbejeo za kilimo ni juu si mchezo. Hizi ni kauli mbiu za kutia watu hamasa tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom