Elections 2010 Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
0
Najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

Msimamo wa Chadema haujabadilika

by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pmKuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.
Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook


NYONGEZA: Kuna thread imewekwa hapa chini na Mwanajamii mmoja (Chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (Lawful na Legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi


Moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: legitimate - Google Search


Zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.


Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: meaning and definitions — Infoplease.com.


Kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principlesTukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

Sheria inasema Raisi ni Raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.


Hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.


Kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule Georgia

http://georgiandaily.com/index.php?option=com_content&task=view&id=2829&Itemid=68
 

Mpevu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,809
0
Ahsante kwa mchakato huu, ngoja niupitie tena kwa makini ili kutanabahi.
 

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
195
Tunaamini msimamo wa CHADEMA ndiyo maana hatuterereki kwa habari zinazochakachuliwa na baadhi ya vyombo vya habari. HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE...............................
 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
0
Hapo umenena mkuu. Na ambacho nadhani CHADEMA wanapaswa kufanya ni kusimama kidete na kuongoza maamuzi ya msingi yatakayotuvusha hatua nyingine.

Otherwise nahisi inaweza kutokea kama unavyohisi, kuchakachua tena na kutaendelea mpaka siku moja mahali ambapo "BUSARA" haitafanya kazi tena.

Kama mambo hayafanyiki kwa wakati yanaweza kuwa na madhara makubwa hapo baadae

Well noted mkuu
 

Proud Patriot

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
224
195
mwanakijiji kweli LIMBUKENI, kaingizwa chaka na magazeti ya kifisadi akadhani CDM wametetereka! naye eti akatoa tamko kuwa WAOMBE MSAMAHA, embu jiheshimu! yani sa hvi ccm wana kazi ya kupindisha kauli za viongoz wa CDM
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,237
1,500
mwanakijiji kweli LIMBUKENI, kaingizwa chaka na magazeti ya kifisadi akadhani CDM wametetereka! naye eti akatoa tamko kuwa WAOMBE MSAMAHA, embu jiheshimu! yani sa hvi ccm wana kazi ya kupindisha kauli za viongoz wa CDM

Hata mimi nimehisi Mwanakijiji ana matatizo siku hizi.
 

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,875
1,195
hebu tuangalie maana ya haya maneno waliyotumia:

law·ful   
[law-fuhl] Show IPA
–adjective
1.
allowed or permitted by law; not contrary to law: a lawful enterprise.
2.
recognized or sanctioned by law; legitimate: a lawful marriage; a lawful heir.
3.
appointed or recognized by law; legally qualified: a lawful king.
4.
acting or living according to the law; law-abiding: a lawful man; a lawful community.

il·le·git·i·mate   
[adj., n. il-i-jit-uh-mit; v. il-i-jit-uh-meyt] Show IPA
adjective, noun, verb, -mat·ed, -mat·ing.
–adjective
1.
born of parents who are not married to each other; born out of wedlock: an illegitimate child.
2.
not legitimate; not sanctioned by law or custom.
3.
unlawful; illegal: an illegitimate action.
4.
irregular; not in good usage.
5.
Logic . not in accordance with the principles of valid inference.
6.
Obsolete . (formerly, in London)
a.
of or pertaining to stage plays in which musical numbers were inserted because of laws that gave only a few theaters the exclusive right to produce straight dramas.
b.
acting in or producing such productions.
–noun
7.
a person recognized or looked upon as illegitimate.
–verb (used with object)
8.
to declare illegitimate.

embu wakuu nisaidieni kufafanua zaidi hapa...maana mimi sioni tofauti za haya maneno mawili. Can something be lawful yet illegitimate?
Mifano hai ingefaa...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom