Kwa dunia ya sasa, Gari ni moja ya hitaji muhimu sana kwa binadamu

Dah! hiyo ilikuwa hela ndogo sana mkuu ... ingia kwenye ubadilishaji pesa uone..
Ilikua ni hela ndogo?wkt mwaka 1998 manesi kibao huko serikalini mishahara yao ilikua Tsh 37,000(elfu thelathini na saba) kwa mwezi.
 
Hapa ndio tunapokosea waswahili.wahindi wana msemo mmoja usianze kutumia hela kabla hujaingiza hela.Ndio maana huishi maeneo ya biashara.Anajenga ghorofa analala juu duka liko chini.Hana hata nauli hata ya daladala kwenda dukani kwake.Anashuka kwa miguu dukani .Chai anakunywa saa nne baada ya mauzo.Mswahili unaanza kutumia hela tena nyingi kwenye mafuta ya gari kwenda eneo la biashara . Ukienda Na kurudi mhindi keshakupita mbali sababu yeye gharama ya mafuta ya gari haimo kwenye hesabu ya Matumizi ya siku hiyo.Kuendekeza magari ya kutembelea ni moja ya chanzo cha umaskini Africa.
Public transport system ya kuweza kumsaidia mtu anayeondoka kwake sa 10 alfajiri na kurudi nyumbani saa 6 usiku iko wapi?
 
Sio 98 ni 1998;
Unaona ni zamani sana! majuzi tu hapa ... nambie walonunua magari yapo? tena mwingine rafiki yangu alishakufa kwa sababu hako kagari alikafuata Uganda kakampa kiburi akawa anabadilisha mademu. RIP my friend.
Narudia tena - gari ni jeneza linalotembea.
Nyumba vipi sio jeneza unalolalia humo ndani?Hjawahi kusikia watu wameungua moto ndani ya nyumba?
 
Public transport system ya kuweza kumsaidia mtu anayeondoka kwake sa 10 alfajiri na kurudi nyumbani saa 6 usiku iko wapi?
Uliza wapika supu Huwa wanatumia usafiri Gani kwenda machinjioni Na uliza wauza samaki usafiri Huwa wanatumia upi kwenda ferry mnada wa samaki uliza wafanyakazi wa mahoteli Na baa zinazofungwa usiku wa saa sita Huwa wanarudi makwao kwa usafiri gani
 
Watu mnaongelea nyumba kama ni kitu cha maana sana kuna mtu alijenga hotel ya vyumba 13 kwa almost mil 300 na ushee hapo Mwz,biashara imezingua, ameigeuza hostel ya wanafunzi wa chuo.

Wanamlipa Tsh.600,000 kwa mwaka per room ukizidisha kwa room 13 anapata mil 7.8 kwa mwaka bado maintainance cost(kupaka rangi,mabomba kurepair etc)

Mpk hela irudi ni miaka zaidi ya 40 na ushee amejaribu kukopa bank wanasema watampa mil. 100 only,what a https://jamii.app/JFUserGuide.
 
Naamini gari na nyumba vyote ni muhimu, inategemea na yafuatayo;
1. Priority zako katika maisha.
2. Nature ya kazi yako.
3. Aina ya watu unaokutana nao.

Gari inahitaji kipato cha uhakika(though inategemea ni aina gani ya gari). Hizi vitz na jamii zake unaweza kuzimudu kwa kipato cha kawaida tu.

Ardhi haishuki thamani hata siku moja, ukinunua plot leo kwa 5M, baada ya miaka mitatu utaiuza kwa faida. Angalia tu usinunue kwenye hifadhi za barabara, unaweza kufwa kwa shambulio la moyo.
Uko sahihi mkuu
 
Halafu sasa wafanya biashara wenye akili hizi utawakuta huku tanzania tu.. huwezi kukuta kwenye developed country yoyote huu upuzi, kuna wale madogo waliotengeneza snap chat mpaka leo wanatumia usafiri wa umma na hawana hata expensive cars na ni mabilionea wa kariba ya dunia.
Usafiri wa umma hapa bongo wakujivunia ni upi?Mwendokasi(ukashike bomba) au unaongelea train ya Mwakyembe sio?
 
Uliza wapika supu Huwa wanatumia usafiri Gani kwenda machinjioni Na uliza wauza samaki usafiri Huwa wanatumia upi kwenda ferry mnada wa samaki uliza wafanyakazi wa mahoteli Na baa zinazofungwa usiku wa saa sita Huwa wanarudi makwao kwa usafiri gani
Kwa hio na mimi nikapande usafiri wa wauza supu sio?hahah akili zao unazijua mwenyewe boss.
 
Watu mnaongelea nyumba kama ni kitu cha maana sana kuna mtu alijenga hotel ya vyumba 13 kwa almost mil 300 na ushee hapo Mwz,biashara imezingua, ameigeuza hostel ya wanafunzi wa chuo.

Wanamlipa Tsh.600,000 kwa mwaka per room ukizidisha kwa room 13 anapata mil 7.2 kwa mwaka bado maintainance cost(kupaka rangi,mabomba kurepair etc)

Mpk hela irudi ni miaka zaidi ya 40 na ushee amejaribu kukopa bank wanasema watampa mil. 100 only,what a ****.
Nashangaa watu wanasema ardhi haishuki thamani. Hivi bei za viwanja na nyumba zilivyoshuka wachangiaji humu hawajui? Hadi nyumba za kupanga zimeshuka bei.
 
Nashangaa watu wanasema ardhi haishuki thamani. Hivi bei za viwanja na nyumba zilivyoshuka wachangiaji humu hawajui? Hadi nyumba za kupanga zimeshuka bei.
Ardhi ilipanda bei sana kipindi pesa chafu ikitembea mitaani, ila kwa sasa bei za viwanja zipo stable tu, inategemea ni eneo gani hasa mtu anataka kiwanja/shamba.

Japo kila mtu ana vipaumbele vyake katika maisha, ninachoona muhimu mwenzangu haoni umuhimu wake.
 
gharama za kulihudumia gari zinaendan na kipato chako? per day uwe unatoa 20k au zaid ya mafuta!it means ww per day uwe unaingiza 50k ili uish vzr na gar..kuna jamaa nafany nae kaz aliniiga kununua gar hakumaliz 6 months anatafuta mtej auze..so be careful

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom