Kwa dunia ya sasa, Gari ni moja ya hitaji muhimu sana kwa binadamu

Kwahio unawashauri nini waTz? Wasijenge majumba makubwa ya kuishi au wasinunue magari ya ndoto zao? Tuelewe kwamba vipaumbele vya watu vimetofautiana. Kuna mtu ndoto yake ni kumiliki gari nzuri, nyumba kama atajenga ni ya kawaida. Mwingine ndoto yake ni kuwa na ghorofa la maana hata ale majani yeye anataka ghorofa. Pia vitu vizuri kila mtu anapenda sio vya wafanyabiashara tu.
Ndoto isiyoingiza pesa ni bullshit.Unaotaje Ndoto ya kitu ambacho hakiingizi pesa Ila Kila pesa ? Hiyo Ndoto ni ya shetani la umaskin.malaika akikuotesha atakupa Ndoto ya jinsi ya kutajirika Na kuondokana Na ulofa
 
Ndoto isiyoingiza pesa ni bullshit.Unaotaje Ndoto ya kitu ambacho hakiingizi pesa Ila Kila pesa ? Hiyo Ndoto ni ya shetani la umaskin.malaika akikuotesha atakupa Ndoto ya jinsi ya kutajirika Na kuondokana Na ulofa
Nyumba yako uliojenga unaishi inakuingizia pesa?
 
WENZAKO WAKO TAYARI HATA KUKOPA HAYO MAGARI HILI WALETE FAKE IMPRESSION KWA WATU WALIOWAZUNGUKA, HILI WAONDOKANE NA HIYO HALI YA KUONEKANA BADO NI MASIKINI HATA KAMA NI KWA MUDA MFUPI... HIZI NCHI MASIKINI ZIMEJAA WATU HASIOKUWA NA FORESIGHT
usemacho ni kweli, wat wengi hawaishi kutokana na uhalisia wao, hawaishi maisha yao, ni kitu mbaya sana hii....
 
Naona ubishani upo hapa kula kulala wanasema gari ndio kila kitu, wanaolisha familia na kulipa kodi wanasema nyumba ndio kila kitu

MY TAKE
Acheni kufananisha nyumba na vitu vya kijinga mnafananisha nyumba na gari hivi mnadhani kujenga mchezo ukiwa na mawazo mepesi unapenda mawazo ya kinayasoki nk ya boost akili yako uwezi amini nyumba ni jambo la msingi kwa sisi familia za kibantu ni jambo la msingi.

Mjini ukiwa na million sita unapata gari haya jiulize je? hiyo million sita unaweza kumiliki nyumba kati kati ya jiji kwaiyo acheni kabisa sema kipi bora kati ya nyumba na gari gari kitu chepesi sana
 
Mojawapo kati ya tofauti za maskini na tajiri ni kuwa maskini anapenda sana "show off"! Yaani kujionyesha kwamba ana hiki au ana kile.

Ndiyo utajua kwanini wahenga walisema maskini akipata matako hulia mbwata.
 
Kua uyaone!
Kwa mtazamo wako uko sahihi kabisa. Anayejenga nyumba yuko sahihi na anayenunua nyumba yuko sahihi pia. Ila neno la kwamba kununua ardhi ni kuweka hela sehemu isiyozaa - hapo ndo nimedharau uwezo wako wa kufikiri.
Natoa mfano;
Mwaka 1998, nilinunua plot ndogo kwa Tshs. 280,000/= na nikajenga kibanda kidogo humo ... hadi sasa ipo lakini ilishapanda bei na kuna mtu aliniletea milioni 13,500,000/= mwaka 2010 nikaikataa.
Usijidanganye hata siku moja ... ardhi ni zaidi ya kitu chochote. Haya magari ni makaratasi tu ... after 5 years gari ni takataka ila ardhi ndo inakuwa inaendelea kuwa na dhamani.
We jamaa una akili sana!

Nmeshangaa mleta mada anasema eti nae alienda hadi chuo kikuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nikupe elimu kidogo ya biashara.Asset ni Mali yoyote inayoingiza kipato .Gari ya kutembelea sio Asset ,Wala nyumba ya kuishi ambayo isiyoingiza pesa hata iwe jumba la kifalme sio Asset ni Liability.Gari ya kutembelea Na jumba la kulala ni liability sababu kazi yao ni kutumia pesa .Kujua gari yako ni Asset au Liability Anglia linakuingizia shilingi ngapi ukilinganisha Na Matumizi unayotumia kwenye hilo.Ukiona linakula sana pesa kuliko kuingiza achana nalo.Biashara za matapeli ndizo hizo za kukutana maeneo makubwa makubwa Na suti za kuazima Na magari ya kuazima mtu aonekane super wakati lofa .Hiyo character ni ya wapiga dili.Fanya biashara Na waarabu au wapemba wenye hela uone anajivalia kanzu lake na miguuni kavaa makobasi au mayebo yebo lakini Ana malori 300 Na visima vya mafuta.Biashara mnafanyia hata msikitini au dukani kwake au sehemu ya kijiwe cha kahawa BIASHARA YA ya mabilioni ya shilingi.Waswahili matapeli ndio wenye hizo complication .Mleta mada Na wewe una sifa zote za utapeli
Umenena vyema mkuu
 
Acheni kufananisha Nyumba na mambo ya kijinga,,, Aise hamna raha Kama kulala kwenye nyumba yako hausumbuliwi kodi ,
 
Kila kitu kutokana na mahala ambapo unaishi na nn unafanya kwamfano mwenzangu na mm labda umeajiriwa na kamshara kako unaenda kununua kagari yakutokea nyumba ya kupanga hadi kazini kisha unarudinayo home hauna ishu nyingine hapo utakuwa unaweka mafuta bado bima nyumbani kodi ya watu inahitajika afu kagari ulichukua mkopo so mshahara unakatwa kila siku hapo utasema kwann maharagwe ni.mboga ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni kwelu, lkn hiyo 280,000 kipindi hicho sio ela ndogo, inaweza kuwa ina thaman na 13M ya sasa.

Hata fixed acc bank mpaka sasa pengine ingekuwa zaidi ya 20M sasa.

Nilichikuwa nachomaanisha, gari inaweza kukupa ela zaidi kuliko nyumba.

Kuna jamaa angu kanunua IST, kampa dogo afanye uber kwa siku hesabu ni 30k. Ile gari imezaa ist nyingine na bado iko vzr.

Just imagine gari ya 10M inakuletea around 700k kwa mwezi, wkt nyumba itakayokuletea 700k kwa mwezi thaman yake si chini ya 70M

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni gari kwa ajili ya biashara kama unavyosema hapa nipo naww ila kama nilakutembelea bora nyumba yakuishi ianze kuliko gari lakutembelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini gari na nyumba vyote ni muhimu, inategemea na yafuatayo;
1. Priority zako katika maisha.
2. Nature ya kazi yako.
3. Aina ya watu unaokutana nao.

Gari inahitaji kipato cha uhakika(though inategemea ni aina gani ya gari). Hizi vitz na jamii zake unaweza kuzimudu kwa kipato cha kawaida tu.

Ardhi haishuki thamani hata siku moja, ukinunua plot leo kwa 5M, baada ya miaka mitatu utaiuza kwa faida. Angalia tu usinunue kwenye hifadhi za barabara, unaweza kufwa kwa shambulio la moyo.
Hapo ni nature ya kazi inamatter sana aina ya watu haitakusaidia zaidi yakukupoteza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mojawapo kati ya tofauti za maskini na tajiri ni kuwa maskini anapenda sana "show off"! Yaani kujionyesha kwamba ana hiki au ana kile.

Ndiyo utajua kwanini wahenga walisema maskini akipata matako hulia mbwata.
Wewe usiejionesha ni tajiri kuliko Floyd Maywether anajionesha na kujitapa kila siku mitandaoni.!!??



Nijibu Basi tajiri wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom