Kwa dhuluma kubwa iliyopo sasa nchini kutoka vyombo vya dola, tunahitaji mabadiliko haya.

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
6,062
10,461
RAIS MPYA WA ZAMBIA AMFURUSHA OFISINI MKUU WA POLISI (IGP), MKUU WA MAJESHI (CDF) na DPP, AAHIDI KUMALIZA UTAWALA KANDAMIZI WA MTANGULIZI WAKE

RAIS mpya wa Zambia Hakainde Hichilema jana Jumapili August 29,2021 ameteua wakuu wapya wa jeshi na kuwaondoa wakuu wote wa polisi akiwemo IGP na Mkurugenzi wa Mashtaka na Makosa ya jinai huku akiahidi kumaliza utawala kandamizi wa mtangulizi wake.

Akitoa hotuba yake Rais amesema wakuu hawa wa vyombo vya dola walitupilia mbali weledi na kuikanyaga Sheria ili kumkandamiza mwananchi kwa manufaa ya Viongozi wachache huku wakijua wazi kuwa ni kinyume cha Sheria.

Rais ameongeza kuwa katika utawala wa mtangulizi wake IGP na wakuu wengine wa Polisi walitumia madaraka yao vibaya kula rushwa, kubambikia raia wasio na hatia kesi, kupora mali za raia, kutesa, na hata kuua raia wasio na hatia.

"Mimi mwenyewe nimepitia mateso makali ya polisi, wamenikamata mara kadhaa, wamenibambikia kesi na kunishitaki kwa UONGO mara kadhaa, nimetupwa gerezani kwa kesi ya kubambikiwa kuwa Mimi ni mhaini niliyetaka kumuua mtangulizi wangu Rais Edgar Lungu. Kwa haya yote nitakuwa MNAFIKI nikisema namuamini IGP na wakuu wengine wa vyombo vya usalama na ndio maana nimeamua kuwafuta kazi wote huku Sheria ikisubiri kufuata mkondo wake" amesema Rais Hakainde Hichilema.

"Sitaki kurithi na kufanya kazi na Viongozi ambao mikono yao inanuka damu, MATUMBO yao yameshibishwa na rushwa, watu ambao wanadhani kuwa unapokuwa na cheo sasa una fursa ya kutesa na kunyanyasa wananchi. Nataka kufanya kazi na watu ambao wana HOFU ya Mungu, watu wanaojua kuwa cheo ni dhamana ya kuwatumikia wananchi na sio dhamana ya kutesa wananchi. Watu wanaojua kuwa nje ya madaraka na vyeo vyao wao ni binadamu tu kama binadamu wengine." aliongeza Rais Hakainde.

IGP wa Polisi Nchini Zambia Afande Kakoma Kanganja tarehe 25.11-2019 aliwaonya wanachama wa Chama cha Upinzani nchini Zambia(UPND) kuwa wakijaribu kuandamana polisi wake WATAWAKUNG'UTA sawasawa pamoja na kiongozi wao Hakainde Hichilema watamvunja miguu kwa risasi. IGP huyo alienda mbali na kusema hawezi kukubali kuona vibaraka wa magharibi wakiiharibu Zambia au wakimharibia kibarua chake.

Katika uteuzi huo Rais Hakainde amewateua wafuatao kuchukua nafasi za waliofutwa kazi:

1. Rais amemteua Lieutenant General Dennis Alibuzwi kuwa Mkuu Mpya wa majeshi yote ya Zambia (CDF) na Naibu wake ni Major General Geoffrey Zyeele, ambaye pia kwa nafasi yake yeye ndiye mnadhimu Mkuu wa Jeshi "Chief of Staff."

2.Rais amemteua Lieutenant General Collins Barry mwenye asili ya Scotland kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Anga la Zambia "Zambia Air Force ZAF". Naibu wake ni Major General Oscar Nyoni.

3. Rais pia amemteua Remmy Kajoba kuwa Mkuu Mpya wa Polisi (IGP).

Wengine walioteuliwa ni Mkuu Mpya wa Jeshi la kujenga Taifa na jeshi la ardhini. Mkuu wa Jeshi la wana maji akihifadhi kiti chake

Aidha Rais Hakainde amewashukuru maafisa aliowafuta kazi kwa kipindi walichoitumikia Zambia katika nafasi zao.

Rais pia amewaonya wakuu wapya wa vyombo vya ulinzi na usalama akiwaambia kuwa " na ninyi niliowateua nataka niwaambie lazima muwatumikie watu kwa weledi na uadilifu usiotiliwa shaka, muwatumikie watu kwa HAKI na usawa kwa moyo wenu wote huku mkihakikisha kuwa HAKI za binadamu, UHURU wa watu vinaheshimiwa. Siku zote mkumbuke kuwa hakuna cheo wala madaraka vinavyokupa uhalali wa kumuonea mtu yeyote, ishikeni, Sheria, iishini Sheria na msimamie Sheria kwa HAKI bila kumkandamiza mwananchi. Polisi kataeni maagizo yanayoenda kinyume na kiapo chenu, kinyume na weledi na kinyume cha Sheria za Zambia" amesema Rais Hakainde.
Wewe unasemaje?
 
Back
Top Bottom