Kwa Dharura Serikali izuie haraka uuzaji wa mazao ya chakula nje ya nchi.

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
6,417
2,000
Kwakua hali inajionesha itakua mbaya hasa kuanzia miezi ya pili na walau soko la ndani limeimarika kidogo ni wakati sasa wa Serikali kufunga mipaka na kuzuia uuzwaji wa mazao ya chakula nje ya nchi ili kukabiliana na hali ya taharuki ya usalama wa chakula.

Jeshi la wananchi, jeshi la polisi, usalama wa taifa kazi yenu ni kuangalia usalama wa nchi na nchi ni mwananchi hakikisheni mnawashauri viongozi wenu juu ya haya kwani bila chakula hiyo amani mnayoilinda itatoweka binadamu akishakua na njaa hutomzuia kufanya lolote maana anakuwa kama amekufa tayari.

Viongozi naona wako kimya na tishio la njaa linalokuja tena bila wasiwasi wanaona ni kawaida kabisa sijui wanawaza nini hawa watu.

NJAA INAKUJA CHAKULA KITAPANDA BEI MARADUFU.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,578
2,000
Nani mwenye mawazo hayo??hata hivyo sio sawa, mtu anataka kuuza mazao yake ili pesa imsaidie kwa mahitaji yake, soko la ndani hakuna, NFRA, hawanunui kuwa wanayo mahindi ya kutosha, sasa unataka afanye nini?
Serikali yenyewe hii ambayo kwao kila kitu ni dharura?!!
 
Soko la ndani limeimarika mazao sio mengi nchini ni afadhali watu walalamike lakini usalama wa chakula uwepo na kumbuka hii ni kwa dharura tu, nchi za Rwanda, Uganda na Kenya wanapokua na uhaba wa chakula hutoa pesa kwa wafanyabiashara wa nchi zao hao huenda kununua mazao hitajika nchi nyingine tena hili hufanywa kwa ustadi na vitengo vyao vya usalama wa mataifa yao na mahindi huku hununuliwa kama wafanyabiashara binafsi kumbe ni mifumo inafanya kazi.
 
Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
6,417
2,000
Unajua gharama za kilimo ww,ungekua na akili kidogo ungeiomba serikali inunue chakula kwa wingi kiwekwe kwenye maghala

Serikali hii hii itoe bei nzuri kwa mkulima! Sijasema wanunue wao kwa sababu madhira ya wakulima wa korosho unayajua na by the way mkulima mdogo wa kitanzania kwa sasa amini usiamini hana mahindi ya kuuza mahindi yamebaki kwa wafanyabiashara wanaoweka stock na sio mkulima hakuna mkulima wa Tanzania anavuna mwezi wa tano au mwezi wa nne na muda huu awe na mazao hayupo iwe mpunga au chochote ni wachache sana
 
Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,387
2,000
Huyo mkulima wakati anahangaika na kilimo kuna msaada alipata toka Serikali ?? Ulimpangia alime hekari ngapi?? Kwanini umpangie mahali pa kuyauza mazao yake?? Nawe nenda kalime kisha utoe msaada Kwa Serikali.
 
Hao unaowaita Wafanyabiashara ndio wanaowasaidia Wakulima kwa kuwakopesha pembejeo na fedha wakati wa kilimo. Wakati wa mavuno hulipa madeni yale baada ya kufanya biashara. Sasa tatizo liko wapi??
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,768
2,000
Unajua gharama za kilimo ww,ungekua na akili kidogo ungeiomba serikali inunue chakula kwa wingi kiwekwe kwenye maghala
Anajiandikia tu
Jana wamemkamata mchina kisa anatumia maji mengi.
Mtu ahangaike kulima halafu pia umpangie wapi pa kuuza
 
Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,140
2,000
Mods futa uzi huu. Mleta Mada hajui kilimo ni nini na shida gani zinawapata wakulikma. Hovyo kabisa kuwa na mawazo kama haya
 
fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,768
2,000
Huyo mkulima wakati anahangaika na kilimo kuna msaada alipata toka Serikali ?? Ulimpangia alime hekari ngapi?? Kwanini umpangie mahali pa kuyauza mazao yake?? Nawe nenda kalime kisha utoe msaada Kwa Serikali.
Hili ndio jibu mujarabu
Mbolea imepanda bei wamekaa kimya watu wakivuna wanataka kuwapangia wapi pa kuuza
 
chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,087
2,000
Nani alikutuma usilime!?,uvivu wako wa kwenda shamba usitukele ss wakulima.si mnajifanyaga mkiwa dar mnatuona watu wa shamba tunachelewa maisha,Sasa mwaka huu tutaheshimiana tu.hiyo dar mtaikimbia mwaka huu wenyewe ,na mwaka huu nawaomba wakulima wenzagu tusikubali kulubuniwa na zawadi za mikate na kandambili,wakija kjjn waje na vyakula vyao kabisa ,kwa muda watakao kaa huku kjjn!
 
Juandeglo

Senior Member
Dec 20, 2014
170
500
Kwakua hali inajionesha itakua mbaya hasa kuanzia miezi ya pili na walau soko la ndani limeimarika kidogo ni wakati sasa wa serikali kufunga mipaka na kuzuia uuzwaji wa mazao ya chakula nje ya nchi ili kukabiliana na hali ya taharuki ya usalama wa chakula.
Jeshi la wananchi, jeshi la polisi, usalama wa taifa kazi yenu ni kuangalia usalama wa nchi na nchi ni mwananchi hakikisheni mnawashauri viongozi wenu juu ya haya kwani bila chakula hiyo amani mnayoilinda itatoweka binadamu akishakua na njaa hutomzuia kufanya lolote maana anakua kama amekufa tayari.
Viongozi naona wako kimya na tishio la njaa linalokuja tena bila wasiwasi wanaona ni kawaida kabisa sijui wanawaza nini hawa watu.NJAA INAKUJA CHAKULA KITAPANDA BEI MARADUFU.
Laiti watu wangekuelewa mkuu wasingeandika hivi walivyoviandika. Anyways sisi ndo binadamu. Cha kukushauri kama unayo fedha nunua weka stock ya chakula.
Hata nuhu alishaongea sana na hakuna aliyemuelewaga. Save your soul mkuu.
 
Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,894
2,000
Watu kama huyu mtoa mada ndo wale wenye tabia za kukaa ofisini kusubiria rushwa, wakifika vijijini wanazunguka kwa ndugu wawape chakula bure, wakiombwa msaada wa pesa kwa ndugu ni wagumu sana kutoa, wanakejeli wakulima kwamba ni wanyonge wameshindwa maisha.
Sasa kwa taarifa yenu siku hizi tunalima mazao yanayotutosha kula sisi wenyewe baada ya kejeli za wakulima wa korosho na kahawa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom