Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,681
- 149,880
Awamu hii ya tano tangu iingie madarakani imekuwa na agenda moja ya kuwatimua na kuwasimamisha kazi ma-CEO wa Mashirika na Taasisi mbalimbali za umma mtindo unaojulikana kama "kutumbua majipu".
Hata hivyo,kwa upande wa TANESCO sitarajii kusikia CEO wa shirika hili akiguswa kwa lolote na serikali ambayo yenyewe imeshindwa kutimiza wajibu wake wa kulipa bili zake kwa wakati kiasi kwamba sasa serikali inadaiwa na TANESCO jumla ya shilingi bilioni 33 huku serikali ya Zanzibar nayo ikidaiwa jumla ya shilingi bilioni 106!!
Madeni haya ya serikali ni sawa kabisa na kuhujumu shirika hili na kwa lugha nyingine ni sawa kabisa kuhujmu uchumi wa nchi hii maana hili ndio shirika nyeti katika kuendesha uchumi wa nchi hii.
Kwa deni hili,kabla Magufuli na waziri wake hawajatua TANESCO(kama wana mpango huo), walipe kwanza deni hili ndio wapate walau uhalali wa kuhoji mapungufu yaliyopo katika shirika hili.
Serikali ya ina hii tofauti gani na wafanyabiashara wanaokwepa kodi?
Waandishi wa habari kwa hili mna kazi ya kufanya na mkiifanya vizuri, Magufuli hawezi kwenda TANESCO leo,kesho wala mtondogoo.