Kwa dalili hizi, Mnyika kapoteza jimbo la Ubungo

Status
Not open for further replies.
Kunguru mweusi - mweusi tiiiiiiii! Kazi kunusa mizoga tu. Huo mzoga uliounusa hautishi, we endelea kujishibisha nao kwa kujifariji. Kwa taarifa yako, hata wakichakachua kesi, jimbo la Ubungo hawachukui, litabaki la CDM hata CCM wakimweka JK agombee.
Makazimapya; Acha mikwara, inamaana Handsome JK uwezo wake wa kuongoza unaishia kwenye Ubunge tu!, na sio Urais?.
 
nani tena ana hamu ya kusikia magamba akiongoza nchi?
miaka 50 hakuna mabadiliko afu tuwarudishe tena?
kweli una akili ya kunguru
 
Kunguru Mweusi hebu tuambie kama matokeo tayari wanayo hao uliowakuta wanafanya maandalizi.
Sitakupinga sana ukizingatia baadhi ya mahakama zetu zinavyotoa maamuzi kwa maelekezo ya ccm.
Mkuu hakuna shaka MUNGU yupo nasi
 
Hilo ongezeko la kura ni magamba walizipiga kabla kama kawaida yao. Walidhani wanavyuo hawangekuja kupiga kura. Hivyo wakachukua idadi ya wanachuo wa mikoani wakachua wakaweka pwaaaa!

Hiyo ni moja, pili hakuna ushahidi ulio wazi kwamba hizo kura zilienda kwa JJ Mnyika. Ni kwanini tusiseme pia zote zilienda kwa Huyu Gamba?

Jj anakwenda kuendelea na ubunge wake.
 
Makazimapya; Acha mikwara, inamaana Handsome JK uwezo wake wa kuongoza unaishia kwenye Ubunge tu!, na sio Urais?.

GEMBESON: Sijapiga mkwara wowote mkuu, ila huo ndo ukweli wenyewe. Kwani si nchi tunaiendesha wenyewe kwa utulivu wetu? Kila siku JK anazuga na safari za hapa na pale na hakai kwenye jimbo lake la uchaguzi ambalo ni Tanzania.
Mwisho mkuu naomba nisahihishe: Id yangu ni Maishamapya na siyo Makazimapya.
 
Kila ninapopita ktk Ofisi za CCM Ubungo siku 2 hizi, nahisi kuna jambo kubwa linaweza kutokea Jimboni hapo.
Furaha na maandalizi ya hapa na pale yanaandaliwa.
Ofisi zinaonekana kama zinasafishwa safishwa, matawi vile kama yanaanza kufufuliwa, hamasa za chama zinaanza kuonekana ambapo kwa kipindi kirefu kiltoweka.
kwa haraka haraka unaweza ukahisi kuna harakati kubwa za kisiasa zinaweza kutokea kipindi kifupi baadae

JEE HICHI NDICHO KITACHMUANGUSHA MNYIKA KTK KESI YAKE:
kukiri kwa Mnyika Mahakamani tofauti ya kura zaidi ya 14,000 inayoonekana katika fomu iliwasilishwa mahamani
Kutumika komputa yake kuhesabiwa kura

kukerwa kwa Jaji Msuya jinsi Mnyikai alivyokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Wakili wa mlalamikaji, Issa Maige,

Kunguru,

..mimi naomba uchaguzi wa ubungo urudiwe, halafu Mnyika na Nape wapambanishwe.
 
GEMBESON: Sijapiga mkwara wowote mkuu, ila huo ndo ukweli wenyewe. Kwani si nchi tunaiendesha wenyewe kwa utulivu wetu? Kila siku JK anazuga na safari za hapa na pale na hakai kwenye jimbo lake la uchaguzi ambalo ni Tanzania.
Mwisho mkuu naomba nisahihishe: Id yangu ni Maishamapya na siyo Makazimapya.
Maishamapya; nimekusoma.
 
Judicial deccision is not the feeling of Judge. Judge must deal with material fact and law this wll lead to judicial decision. Kwa hiyo jaji hatoi maamuzi kwa hisia zake kama akifanya hivyo Jaji wa Rufaa hataona hizo hisia za jinsi Mnyika alivyojibu maswali. Msiogope Ushindi waja
 
namuonea huruma sana rafiki yangu Mnyika,sijui ataishije hapa mjini maana ni wazi ili jimbo anapoteza.
 
Mie nilimpa kura yangu lakini bado nakerwa na hii biashara ya maji inayoendelea kutunyonya alituahidi kuimaliza......tunaumia sana ........tunasubiri 2015 asishangae
 
mtumishi wetu unaona mbali. mimi kesi ambayo sitamuelewa jaji ni ile ya segerea, kama kweli dr.mahanga akibaki.ila kwa upande wa pili naangalia gharama za marudio ya uchaguzi.
 
na haswa ukizingatia kwamba mpendazoe hataki utani, ameainisha makosa yote yaliyotendwa na ccm....mapingamizi ya chaguzi yanaweza kuwa kikwazo cha uharakishwaji wa maendeleo ya jimbo husika.
 
Mtanzania,..kwanza una jina nzuri hata kama sio jina lako halisi...neno Mtanzania nimeliandika katika moja ya gari langu hivyo ikafika hata watu kuniita "MTANZANIA", lakini unaudhalilisha kwa kusema "Mnyika atatuambia alilipwa ngapi na wafanyabiashara ya maji....kaombe ushauri huu kwa Mustapha Sabodo,au Kwanini usimwendee pale ofisini kwake umuweke kati...si mbunge wako?.. Kingine ni kwamba CDM katika mazingira ya rushwa sijui...labda kama wewe unafahamu zaidi kuwa Mnyika kapokea rushwa..Nikiwa na ushahidi wa kutosha kama kapokea, hata mimi nitakuwa wa kwanza kumtupia mawe.

Jingine kuwa mbunge si kwamba utatatua matatizo yote kwa mara moja, inahitaji muda kidogo, matatizo mengine inabidi mbunge huyo atumie sheria halali kung'oa kwanza mizizi ya kifisadi iliyokuwa imeota na kumea halafu hapo hapo ndio pachimbwe msingi wa maendeleo.

Nawasilisha hoja.
 
.....yaani wewe ni hamnazo kabisa!!?? na hapo unaishi mjini unakuwa ***** hivi,je ungekuwa kijijini tunako-assume ni mbumbumbu/waoga ungekuwaje? anakuuliza kadi ya kupigia kura yeye ni Tume ya Uchaguzi? mie ningemjibu ninayo anisubiri nimletee then ningemtoa baru na jambia au panga. wewe umemuacha aende bila maumivu hata ya buku?
 
Mtanzania,..kwanza una jina nzuri hata kama sio jina lako halisi...neno Mtanzania nimeliandika katika moja ya gari langu hivyo ikafika hata watu kuniita "MTANZANIA", lakini unaudhalilisha kwa kusema "Mnyika atatuambia alilipwa ngapi na wafanyabiashara ya maji....kaombe ushauri huu kwa Mustapha Sabodo,au Kwanini usimwendee pale ofisini kwake umuweke kati...si mbunge wako?.. Kingine ni kwamba CDM katika mazingira ya rushwa sijui...labda kama wewe unafahamu zaidi kuwa Mnyika kapokea rushwa..Nikiwa na ushahidi wa kutosha kama kapokea, hata mimi nitakuwa wa kwanza kumtupia mawe.

Jingine kuwa mbunge si kwamba utatatua matatizo yote kwa mara moja, inahitaji muda kidogo, matatizo mengine inabidi mbunge huyo atumie sheria halali kung'oa kwanza mizizi ya kifisadi iliyokuwa imeota na kumea halafu hapo hapo ndio pachimbwe msingi wa maendeleo.

Nawasilisha hoja.
Kama ungekuwa ni mpiga kura wa ubungo nadhani usingepata shida kunielewa. Tulimchagua Mnyika si kwa sababu yupo CDM. Tulimchagua kwa sababu tulidhani ni mbadala anayeweza kututatulia kero yetu kuu ya maji. Nina ushahidi tatizo la maji katika jimbo la Ubungo nila kutengenezwa. Dawasco ikishirikiana na wafanyabiashara wa maji hufunga makusudi huduma ya maji kwa wakazi ili waweze kufanya biashara hiyo. Miundombinu si tatizo tena ilikwishawekwa na wachina kwa gharama kubwa kutoka kwenye kodi zetu wenyewe. Hata hivyo mbunge wetu tuliyemuamini amekuwa akifumbia macho tatizo hili na kwa maono yangu sio kazi kubwa sana kwani ni kufunga vioski vya maji ili yaweze kwenda kwenye makazi. Inatuuma sana sana ukichukulia tuna lipa kodi kwa ajili ya hii huduma adhimu. sasa kwanini tusiamini kama hajawekwa sawa na hawa wafanya biashara???? haya ni mawazo yangu lakini nadhani yapo kichwani kwa kila mwanaubungo aliyempa kura yake.
La mwisho nitasikitika zaidi kama wewe ni mmoja wa wafanyabiashara magari ya maji mnaotulangua maji kwa kutuuzia maji mara 15 zaidi ya bei ya serikali.... nami nawasilisha
 
Mimi namwonya Jaji yeyote mwenye hii kesi awe makini sana. Litakuwa kosa kubwa sana kama la Arusha kutengua uchaguzi wa Mnyika bila sababu za msingi na haki. Tusipende kuongeza sympathy ya Umma kwa CHADEMA na hasira zaidi kwa CCM na Serikali yake kwa watu bila sababu!

Ehe Mh. Jaji, popote ulipo kama Pilato alivyoitwa na mkewe na kuambiwa kuwa Yesu hana hatia; sikiliza hii sauti na usikubali pressure yeyote tumia akili zako, elimu yako na zaidi ya yote sheria za nchi na hekima uliyopewa na Mungu na maisha yako na ya uzao wako yatabarikiwa vinginevyo utajuta kwa nini umeamua hivyo hata kama ni baada ya miaka 10 ijayo. Sikutishi lakini nakupa angalizo tokana na uzoefu wa harakati za kisiasa katika dunia yote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom