Kwa chama hiki ccm kutegemea serikali makini ni uwendawazimu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa chama hiki ccm kutegemea serikali makini ni uwendawazimu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Apr 22, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi yetu na nchi nyingi chama tawala ndio uunda serikali na mara nyingi matendo na maamuzi ya chama utekelezwa na serikali, kwa maana nyingine serikali ndio kioo cha chama.Baada ya kusoma mahojiano Katibu mpya wa idara ya Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, kuhusu mustakabali wa chama hicho NAPE: Kujivua gamba CCM kumezingatia utafiti, si vinginevyo nimefikia conclusion ya kwamba "KWA CHAMA HIKI KUTEGEMEA SERIKALI MAKINI YA KUWATUMIKIA WANANCHI NI UWENDAWAZIMU INATOSHA"Hapa ni baadhi ya nukuu za Mnauye katika mahojiano na Raiamwema

  Raia Mwema: Mabadiliko yamefanyika pengine kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati ya utafiti. Uongozi mpya mmeanza kazi. Je, mmekikuta chama katika hali gani kwa ujumla?

  Nape: Nikwambie ukweli, hali ilivyo ndani ya Chama watendaji wanafanya kazi kwa mazoea. Hali ya uchumi katika Chama ni mbaya. Huwezi kuamini kwamba kwamba katika mazingira ambayo tuna mali zenye thamani takriban Sh bilioni 50, kinachoingia kwa maana ya mapato ni takriban Sh. bilioni moja hivi. Ni lazima sasa tujiimarishe katika sehemu zote; sio tu kimaadili na kisiasa lakini pia kiuchumi.!!!!!!!!!!!!!

  Raia Mwema: Chama kina raslimali nyingi lakini kinayumba kiuchumu. Unazungumziaje hili?

  Nape: Mpango ni kusimama wenyewe kiuchumi kwa sababu tunavyo vyanzo vingi vya mapato lakini nadhani havikusimamiwa ipasavyo. Utaona kwa sasa hata Mweka Hazina wetu ni kijana mwenye upeo mkubwa kielimu kuhusu uchumi. Alikuwa akifanya kazi pale Benki Kuu ya Tanzania.

  Katika vikao hivi tulivyomaliza hivi karibuni tumekubaliana kujenga uchumi unaojitegemea katika chama, na tunazo rasimali za kutosha. Sasa lazima tujisimamie wenyewe na hicho ni kigezo cha kuonyesha kuwa tupo imara kuisimamia pia serikali ili kuimarisha uchumi wa wananchi kwa ujumla.

  Sasa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu hii tuliiagiza serikali ituambie kwenye kikao kijacho imefikia wapi katika mipango yake ya kiuchumi. Kwa hiyo, tutajisimamia kiuchumi kwenye chama lakini pia tutaisimamia serikali kwa manufaa ya wananchi wote.

  CCM NI MZIGO KWA TAIFA NIWAKATI WA KUJIKOMBOA MUNGU TUBARIKI.
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Na wakati huo wote nchi iwe imesimama tu inawasubiri wao???
  No no nooo CCM ni lazima wapishe, wakashughulikiane wao kwa wao na matatizo yao, na sisi tujenge Tanzania yetu tunayoitamani.
   
Loading...