Kwa Chaguzi zinazoendelea barani Afrika, ni kweli CCM haina maisha marefu

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Naona kuna changes kubwa sana barani Afrika juu ya chaguzi kuu za nchi mbali mbali barani Afrika,watu wameshavichoka vyana tawala na vikongwe,hawana imani navyo tena, wanaona kama ndivyo vilivyochelewesha maendeleo ya nchi hizo.

Tuliona Nigeria hali ilivyokua, tumeshuhudia chaguzi ndogo kule Afrika kusini chama cha ANC kilivyopoteza, tumeona Zambia walivyoponea chupu chupu japo nao walikua katika utawala wa upinzani juzi , Ya Gambia tumeyaona na Leo hii Ghana tunaona hali ilivyo.Vyama vikongwe vya muda mrefu kwa sasa havina Sera tena, viebaki kutegemea nguvu za dola kwa kutumia mabavu na vimebaki kuendelea kuogoza kwa mazoea tu.

Ikumbukwe kua huku kwetu Tanzania CCM imebebwa na jina la mtu mmoja tu na sio chama chenyewe,sijui akiondoka huyo mtu mmoja CCM watakua katika hali ipi, siuuoni uhai wa CCM tena.Inawezekana kabisa kua kuna watanzania ambao wamekwishachoshwa hata na jina lenyewe ambalo limekuwepo masikioni tangu nchi ipate Uhuru.

Nawapa moyo sana vijana ambao wanachipukia katika Sasa waliopo ndani ya CCM lakini wakae wakijua kua ni muda wowote Kamba inaweza kukatika, kama wewe bado ni damu mpya ya siasa ndani ya CCM na una maono marefu ya mbali, kwakweli uhai wa CCM u mashakani labda wabadili jina chama ili kionekane kipya. Matumaini yako ndani ya chama hiki kikongwe hayawezi kutimia, sio rahisi kutimia. Ni bora kuongeza nguvu kujenga vyama ambavyo havina muda mrefu ambayo wananchi wanayo matumani huenda vikawa na ukombozi kutoka shida wapatazo na sio CCM ambayo haijawahi kuleta mabadiliko yanayoridhisha toka nchi ipate Uhuru.

Kuna mwalimu Wangu mmoja wa biology aliwahi kiusema kua "ukizaliwa uapitia hatua zote za maisha,utazeeka na mwisho utakufa tu" Hivyo CCM kwa umri wa CCM sasa ni sawa na mzee,kimeshazeeka ni mzee ambaye sasa hata maradhi makali yakimkumba matumaini ya kuishi ni madogo sana.
 
Kuna kitu mnasahau, angalia matokeo ya Uchaguzi uliopita Ghana, huyu ambaye inasemekana ameshinda aligombea pia akashindwa kwa tofauti ya kura laki tatu tu sawa na 3% tu, sasa linganisha CCM vs ukawa, CCM ilishinda kwa tofauti ya kura milioni 2 000 000 au karibia 20%, sasa unawezaje kuliziba hilo pengo kwa miaka 4?
Hilo ndiyo swali, hivyo siku zote jaribu kulinganisha vinavyolingana, chadema au Chama chochote kile cha Siasa TZ hakiwezi kuinyang'anya CCM kura Milioni 2 ndani ya miaka 4 tu, hiyo ni kazi ya miaka 20 na kuendelea kama kila kitu kitabakia jinsi kilivyo, kumbuka hapa naongelea ukawa wala siyo Chama kimoja kimoja kama chadema, kama ukichukuwa chadema kama chadema pekee yake bila ya ukawa, CCM imepata kura milioni 4 sawa na zaidi ya 30% zaidi ya chadema, sasa unawezaje kuziba hilo pengo ndani ya miaka 4? Yaani kupata kura milioni 4 ktk CCM?

CCM itaendelea kushinda Uchaguzi TZ kwa uhakika kabisa mpka mwaka 2035, ni mpaka pale ambapo tofauti kati ya CCM na Upinzani ni kuanzia kura laki tano kushuka chini, hapo ndipo unaweza kuanza kuongelea CCM kuondoka madarakani lkn kura milioni 2 mpka 4 hiyo ni clear cut win haina hata mjadala!

Na hapo bado sijagusia Ubunge ambapo CCM mpaka leo hii imepata Wabunge 188 kati ya 252 wakati chadema imepata wabunge 34 tu, sasa unawezaje kuziba hili pengo ndani ya miaka 4?
 
Mmmhhh bado watnzania wengi vijijin wanaikubali yaan kuna kazi maana hizo nchi ulizotaja wasomi wwngi na awaeeeness kubwa
 
Sasa kikifa si ndio furaha yako sasa unamualert nani?
 
Kuna kitu mnasahau, angalia matokeo ya Uchaguzi uliopita Ghana, huyu ambaye inasemekana ameshinda aligombea pia akashindwa kwa tofauti ya kura laki tatu tu sawa na 3% tu, sasa linganisha CCM vs ukawa, CCM ilishinda kwa tofauti ya kura milioni 2 000 000 au karibia 20%, sasa unawezaje kuliziba hilo pengo kwa miaka 4?
Hilo ndiyo swali, hivyo siku zote jaribu kulinganisha vinavyolingana, chadema au Chama chochote kile cha Siasa TZ hakiwezi kuinyang'anya CCM kura Milioni 2 ndani ya miaka 4 tu, hiyo ni kazi ya miaka 20 na kuendelea kama kila kitu kitabakia jinsi kilivyo, kumbuka hapa naongelea ukawa wala siyo Chama kimoja kimoja kama chadema, kama ukichukuwa chadema kama chadema pekee yake bila ya ukawa, CCM imepata kura milioni 4 sawa na zaidi ya 30% zaidi ya chadema, sasa unawezaje kuziba hilo pengo ndani ya miaka 4? Yaani kupata kura milioni 4 ktk CCM?

CCM itaendelea kushinda Uchaguzi TZ kwa uhakika kabisa mpka mwaka 2035, ni mpaka pale ambapo tofauti kati ya CCM na Upinzani ni kuanzia kura laki tano kushuka chini, hapo ndipo unaweza kuanza kuongelea CCM kuondoka madarakani lkn kura milioni 2 mpka 4 hiyo ni clear cut win haina hata mjadala!

Na hapo bado sijagusia Ubunge ambapo CCM mpaka leo hii imepata Wabunge 188 kati ya 252 wakati chadema imepata wabunge 34 tu, sasa unawezaje kuziba hili pengo ndani ya miaka 4?
Siafiki sana hoja yako ya tofauti za kura na kwamba labda mwaka 2035 na msingi wa mashaka yangu ni mifano ya uchaguzi unaofanyika huko Zanzibar na idadi ya tofauti za kura. Niishie hapa.
 
Wekeni fair election grounds muone matokeo yake...kwa jinsi tulivyo watanzania, namna pekee ya kuitoa CCM ni kupitia uchaguzi. Lakini siyo kwa maigizo ya uchaguzi ambayo tumekuwa tukiyafanya tokea 1995.
Naona umesahau kuzungumzia ushindi wa zaidi ya asilimia 90 alioupata Shein kule Zanzibar akishindana na kivuli chake.
 
Siafiki sana hoja yako ya tofauti za kura na kwamba labda mwaka 2035 na msingi wa mashaka yangu ni mifano ya uchaguzi unaofanyika huko Zanzibar na idadi ya tofauti za kura. Niishie hapa.

Kama haufiki fuatilia chaguzi za Zanzibar za nyuma halafu uone CCM ilikuwa inashinda kwa tofauti ya kura ngapi labda utapata picha ninachokoingelea, kwa huku Bara safari bado ndefu sana kwa Upinzani kushinda Uchaguzi na sababu kubwa ni kwamba Upinzani wenyewe wanalinganisha TZ na nchi nyingine kama Kenya, Zambia au sijui Ghana bila ya kutambua kwamba TZ ni nchi tofauti sana kimuundo wa jamii yake kulinganisha na nchi nyingine za Kiafrika!

Ukichunguza nchi zote hizo kama Kenya au sijui Zambia Vyama vya Siasa wanaunda makundi ya Kikabila na Kabila kubwa huungana ili kupata kura nyingi sasa hapa wetu hakuna kitu kama hicho, kwanza hata kufanya Sensa tu ya Kikabila hairuhusiwi wkt Nchi nyingine zote za Kiafrika wanahesabiana Kikabila, hivyo njia pekee ni ya Vyama kuwashawishi Watanzania wawachague na hapo ndipo tatizo lilipo!
 
Back
Top Bottom