Kwa CCM tatizo si CHADEMA ni Mbowe

KALOKAZA

Member
Jan 3, 2013
95
135
NDUGUwasomaji, ninapenda sana kuwapa pole kwa kifo cha shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Nelson Ndlahla Mandela. Kila gazeti, runinga na redio zimeelezea wasifu wake kiasi cha kufurahisha. Hata hivyo, mimi niseme tu kwamba kwa Mandela tunajifunza neno moja dunia nzima;

"hakuna utawala dhalimu popote duniani utakaoruhusu haki ipatikane kirahisi."

Kwa hakika hawa wote wanaomsifia Mandela kwa namna alivyovumilia mateso akipigania haki za wanyonge Afrika Kusini na duniani kote kwa taathira yake, wengi wao kati ya wale wenye mamlaka wanawatesa sana wananchi wazalendo wanaopigania haki zao na za wenzao.

Hayo yapo sana Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi Afrika na duniani kote. Hivi leo sambamba na habari za kifo cha nguli huyu wa siasa duniani, hapa Tanzania kunaendelea habari za sakata la Zitto Kabwe na Dk. Kitila Mkumbo kunyang'anywa vyeo vyao CHADEMA na Kamati Kuu. Mengi yamesemwa kuhusu namna wanachama hawa wa CHADEMA walivyochukuliwa hatua hizo na jinsi walivyozistahili. Yametokeza makundi yakibishana sana kuhusu hatua hii ya Kamati Kuu.

Wapo waliofurahia na kupongeza hatua hiyo. Hapa baina yao wapo waliohoji ni kwa nini chama hicho kilichelewa kuchukua hatua hiyo kwani walikuwa wanajua ukweli kwamba watu hawa kwa ukosefu huo wa nidhamu walistahili kuondoka mapema zaidi. Wengine waliona mwenendo wa Zitto katika siasa za ukombozi ulivyobadilika na kujiaminisha kabisa kwamba kuna "kitu" kimemdhuru na kuharibu kabisa kasi yake ya awali.

Sitaacha kuwasemea wale walioamini kwamba matendo ya Zitto yanathibitisha wazi kwamba anasaliti harakati za ukombozi kwani amekuwa akihujumu shughuli za CHADEMA na pia yeye binafsi haonekani katika kukurukakara za chama. "Mbona wabunge wote wamekumbwa na kadhia nyingi dhidi ya polisi na lukuki wana kesi mahakamani, lakini Zitto yeye hana kesi hata moja na wala hatujasikia akiparurana na polisi?" mmojawao aliniuliza.

Haidhuru. Hebu leo nije na taarifa ya uchunguzi juu ya sababu hasa ya vita iliyoko CHADEMA. Haiwezekani chama cha siasa kiwe kinapigwa vita bila sababu. Hiki si ugonjwa wala si janga inakuwaje kipigwe vita kubwa namna hiyo? Inakuwaje vyama vingine havipigwi vita kama CHADEMA na ndani ya chama hicho kinachopigwa vita na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni nini?

Kihistoria kila chama cha siasa kilichopata nguvu katika enzi yake kilipigwa vita za aina mbalimbali na hatimaye kuporomoshwa kama si kuanguka kabisa. Ikumbukwe kwamba enzi za NCCR- Mageuzi chama kiliimarika na kuwa tishio kabisa dhidi nya CCM. Wengi waliamini kwamba CCM ilikuwa katika dakika zake za mwisho. Mwaka 1997, NCCR-Mageuzi ikapigwa dafrao. Wanachama wengi akiwepo mwenyekiti wake wa wakati huo wakaondoka.

Baada ya dafrao hilo, chama kilipoteza umaarufu na hakikuwa masikioni wala machoni mwa Watanzania kama ilivyokuwa kabla ya dhoruba. Nyota ya Chama cha Wananchi (CUF) ilianza kung'ara sana, watu walikiona ndiyo mbadala wa CCM. Uhai wa CCM ulikuwa shakani. CUF kilipigwa vita sana. Zilipigwa propaganda nyingi dhidi ya CUF. Serikali na CCM walipiga propaganda nyingi kwamba chama kile kilikuwa cha Kiislamu.

Ilifikia hatua Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) wa wakati huo Omari Mahita, akaenda kwenye vyombo vya habari akionyesha majambia yaliyoletwa nchini na kutangaza kwamba yalikuwa mali ya CUF. Kelele nyingi zilipigwa dhidi ya Maalim Seif aliyekuwa akiwania urais wa Zanzibar kwa lengo la kukidhoofisha chama hicho. Walifanikiwa kabisa kuimaliza CUF huku Tanzania Bara na kule Unguja, lakini bado kule Pemba huwaambii lolote wananchi juu ya chama hicho.

CHADEMA kilikuwa chama kipole. Kilisifiwa sana na viongozi wa serikali na CCM. Aliyeanza kukisifia alikuwa Baba wa Taifa, hayati Julius Nyerere. Wengi ndani ya serikali katika miaka ya 1990 waliitamka CHADEMA kwamba ni chama kinachoongozwa kwa busara nyingi.

Viongozi wake walisifiwa sana kwamba hawana hata tamaa ya kugombea urais. Ikumbukwe kwamba katika uchaguzi mkuu wa 1995 hakikuweka mgombea urais na hata majimboni waligombea sehemu chache sana. CHADEMA kilivishawishi vyama vingine viunganishe nguvu na kuachiana majimbo kama njia ya kuiondoa CCM. Mwaka huo 1995 nguvu za chama hicho katika urais ziliwekezwa kwa mgombea urais wa chama cha NCCR Mageuzi. Kiliamua bila ajizi kumpigia kampeni mgombea urais huyo kila walipokuwa wakiamini kwamba hiyo ndiyo ilikuwa njia njema ya kuishinda CCM.

Mwaka 2000 CHADEMA haikuweka mgombea urais pia. Ilijipima na kuona kwamba haijakua vya kutosha. Kipindi hiki nguvu yake ikazihamishia kwa mgombea wa urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. Kipindi hiki pia CHADEMA kiliamini katika kuhakikisha kwamba kinaachiana majimbo ili kuishinda CCM. Mwaka 2005 CHADEMA kiliamua kuweka mgombea urais. Aligombea kijana mkakamavu Freeman Mbowe.

Katika kinyang'anyiro kile cha moto, Mbowe aliyekuwa mwenyekiti wa chama kipindi hicho alikuja na mbinu ya kutumia helkopta katika kampeni zake. Hii ilimfanya afanye mikutano mingi kwa siku na hivyo kuwakimbiza sana wagombea wenzake, akiwepo mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete. Inakadiriwa kwamba Mbowe alifanya mikutano ya kampeni 582 wakati wagombea wenzake 9 kwa pamoja hawakufikisha mikutano 300.

Kwa kampeni zile ambazo kwa hakika CCM hawakujua mpango nyuma ya pazia wa CHADEMA, ndizo zilizokifanya chama kikawa maarufu na kuanza kufahamika nchini kote. Hii ilikuwa mbinu iliyowekwa na watu wachache chini ya kamanda Mbowe. Alijua wazi kwamba CCM haijajiandaa kuachia madaraka hata kama itashindwa kwa uhalali kiasi gani.

Mbowe alijua kwamba atapata kura nyingi na pia atawasaidia wagombea wengi wa ubunge na udiwani kushinda kutokana na kishindo cha chama. Jambo hili lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Kura za urais alizozipata Mbowe hadi leo hakuna ajuaye nini kilitokea. Ilikuwaje akapata laki sita tu? Eti alishindwa hata na Lipumba wa CUF. Ushahidi wa uongo mkubwa uliofanywa katika kutoa matokeo ya uchaguzi wa rais mwaka ule 2005 ni matokeo ya chaguzi ndogo zilizofuata. Kule Kiteto, CHADEMA ilipata kura 24,000 ikitanguliwa na CCM iliyokuwa na kura 29,000.

CUF haikugombea kabisa kwa kushindwa hata kupata mgombea. Kule Busanda, CCM ilipata kura 25,000 hivi wakati CHADEMA ilipata kura takriban 21,000. CUF haikupata kura 1,000. Hayo yalitokea pia kule Tarime, Biharamulo ambako tofauti kati ya kura za CCM na CHADEMA zilikuwa 880 tu. Kila mahali CHADEMA kilishika nafasi ya pili karibu sana na CCM kikifuatiwa na vyama vingine kwa mbali sana.

Huu ndiyo uthibitisho kwamba matokeo ya urais mwaka 2005 ambapo Kikwete alishinda kwa mbali akifuatiwa na Lipumba wa CUF na wa tatu alikuwa Mbowe wa CHADEMA aliyepata takriban nusu ya kura za Lipumba hayakuakisi hali halisi ya umaarufu na uthabiti wa vyama vilivyoingia katika kinyang'anyiro. Kiukweli tuseme wazi matokeo yale yalikuwa na uongo mwingi.

Hoja yangu kwenu wasomaji leo ni kuchimbua sababu za chuki kubwa ya CCM kwa CHADEMA na ukweli wa kile wanachokichukia CHADEMA. Tumejiridhisha kwamba kila chama cha siasa kilichoshika kasi na kuimarika kiasi cha kutishia usalama wa CCM kilikumbwa na mshikemshike mkubwa kutoka kwa chama hicho tawala ambao ulikifanya chama hicho kuyumba sana na vyote viliporomoka.
Baadhi ya mbinu zilizotumika kuporomosha vyama hivyo ni kuingizwa kwa migogoro baina ya viongozi wa ngazi za juu (hasa Mwenyekiti na Katibu Mkuu), matumizi ya fedha kupoza kasi za viongozi wa juu wa vyama hivyo na bakshishi zilizowafanya wakubali kuachana na mpango wa kuviimarisha vyama vyao.

Kusema kweli kwa mujibu wa CCM ni lazima chama chochote cha siasa kikipata nguvu kifanyiwe kila mbinu kukiporomosha. Hii ni mbinu pekee iliyobaki kwa CCM kubaki salama. CCM kimejithibitishia kwamba hakiwezi tena kuwatumikia wananchi na kuwaondolea matatizo waliyo nayo. CCM si chama cha kuwatumikia Watanzania tena bali ni chama cha kila kiongozi kujitajirisha na kupora mali za umma.

Ili wasihojiwe na ili kupunguza nafasi ya kushindwa katika uchaguzi wanafanya kwa bidii kubwa kuua upinzani. Wanataka wabaki wao wenyewe wakiwa na nguvu ya kufanya siasa na kuwanyima wananchi chama mbadala chenye hadhi ya kuchagulika. Mbowe alikabidhiwa chama kama mwenyekiti akikikuta kina wabunge wanne wa kuchaguliwa na idadi ya madiwani wasiofika 100.
Miaka sita baadaye chini ya uenyekiti wake tayari chama kina wabunge 49, madiwani zaidi ya 500 na wenyeviti kwa maelfu wa vijiji na mitaa. Chama kimejenga mtandao katika vijiji vyote nchi nzima.

Kuanzia kaskazini hadi kusini mashariki hadi magharibi CHADEMA inafahamika. Kikubwa zaidi ni kwamba inafahamika kama chama mtetezi wa wanyonge na kinachopambana na ufisadi na rushwa.

Ugunduzi wa kutumia helkopta katika uchaguzi nchini uliofanywa na Mbowe umefanya watoto na watu wazima nchini wakiona helkopta hata kama ni ya Msalaba Mwekundu au ya Jeshi la Polisi wanajua hiyo ni "CHADEMA inapita".
 
Uchafuzi wa Mbowe unaoendelea Bungeni leo unajidhihirisha kuwa CCM tatizo kwao sio CHADEMA ni Mbowe wanamsakama usiku na mchana, na kila kukicha wanasema hili wanamaliza na lile, kwa sasa kila mwana CCM anashadidia masuala ya ndoa ya Mbowe, utadhani wote wameolewa na Mbowe. Mwigulu yeye kufumaniwa anaona kawaida, kubaka kwa kapuya na kutaka kuua kwa CCM ni kawaida. Mbowe na Mukya wote ni watu wazima, vipi masuala hayo yaliyo kinyume cha sheria ya CCM? na je ikibainika Mwigulu anachosema ni uongo itakuwaje?


 
na je ikibainika Mwigulu anachosema ni uongo itakuwaje?
Mkuu tayari imeshabainika kuwa ni uongo na siyo tu kuwa ni uongo bali ni masuala binafsi yasiyopaswa kujadiliwa bungeni. Ila kuna taratibu fulani ya proffesion fulani; wakati mwingine unamwacha mtu aseme ukimsilkiliza halafu humjibu. Hii inamfanya ajione mpumbafu bila kuambiwa. Ila kwa CCM hapo wameendesha siasa za tija na speaker hana kanuni ya kusitisha mambo kama hayo.
 
Ni wanafiki tu wasio tambua kazi kubwa aliyo ifanya Kamanda huyu.Nchi hii ilikuwa na utawala wa kifalme wa ccm.Hawakuwa na tishio lolote.mpaka wakajitangazia kuwa ccm itatawala milele.Lakini Mbowe ametokea na kuipindua hali hiyo.Hivi sasa akina Mwigulu wanaogopa hata kivuli chake.Pamoja na ugaidi alio nao ameshindwa kabisa kumsambaratisha Mbowe.Amejaribu kumnunua Zito ili ammalize wapi! imeshindikana.Leo bila aibu ananza kuzungumzia tabia binafisi ya mtu.Badara yakukemea wizi na hujuma na rushwa iliyojaa katika serikali yake na kuporomoka kwa elimu anazungumzia Kivuli cha Mbowe.Mbowe hana serikali,hayuko katika ofisi yoyote ya serikaali wao wanatumia muda wote kupambana naye.Watakwisha tu,watanzania siyo wajinga kudanganywa kwa hoja dhaifu kama za Mwigulu
Wakati Mbowe anasafiri na binti inakuzuia nini ccm kutu letea maendeleo?Kwani yeye Mwigulu mboana alifumaniwa Igunga kwa mke wa mtu kwa kuhonga kodi za Watanzania.Acheni siasa za ubabaishaji na mipasho,hamna lolote mnachezea tu Nchi yetu na kutuchelewesha maendeleo.
 
Duuu mleta uzi ubarikiwe sana, maana hii thread ni mwiba mkali mno na mchungu sana kwa magamba Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha
 
Mbowe alimwita Mukya kujinafasi Dubai kama mbunge au hawala? Mwenye akili ataelewa kuwa aliyestahili kufuata taratibu ni Mukya maana yeye ndo alikuwa anajua ratiba na safari kwa ujumla inahitimika lini.

Sasa mlitaka Mwenyekiti achukue mabinti wa casino, usalama ni mdogo sana, maana kwa network ya Nchemba angewatumia kumdhuru mwenyekiti. Hapa namsifu Mbowe na aendelee kujipooza kwa aliyo na uhakika nao. Asiige kabisa tabia ya Nchemba ya kukwepa mapanga ya kufumaniwa.
 
Watanzania wameshagundua ulaghai wa CHADEMA.

wayaona aya malaanifu pia malofa machache yalobaki bila hoja za kuitetea ccm?

sasa apo umeongea nini? ati watanzania wamegundua ulagai wa chadema!!! so what? mchumia tumbo mkubwa we...
 
Ni wanafiki tu wasio tambua kazi kubwa aliyo ifanya Kamanda huyu.Nchi hii ilikuwa na utawala wa kifalme wa ccm.Hawakuwa na tishio lolote.mpaka wakajitangazia kuwa ccm itatawala milele.Lakini Mbowe ametokea na kuipindua hali hiyo.Hivi sasa akina Mwigulu wanaogopa hata kivuli chake.Pamoja na ugaidi alio nao ameshindwa kabisa kumsambaratisha Mbowe.Amejaribu kumnunua Zito ili ammalize wapi! imeshindikana.Leo bila aibu ananza kuzungumzia tabia binafisi ya mtu.Badara yakukemea wizi na hujuma na rushwa iliyojaa katika serikali yake na kuporomoka kwa elimu anazungumzia Kivuli cha Mbowe.Mbowe hana serikali,hayuko katika ofisi yoyote ya serikaali wao wanatumia muda wote kupambana naye.Watakwisha tu,watanzania siyo wajinga kudanganywa kwa hoja dhaifu kama za Mwigulu
Wakati Mbowe anasafiri na binti inakuzuia nini ccm kutu letea maendeleo?Kwani yeye Mwigulu mboana alifumaniwa Igunga kwa mke wa mtu kwa kuhonga kodi za Watanzania.Acheni siasa za ubabaishaji na mipasho,hamna lolote mnachezea tu Nchi yetu na kutuchelewesha maendeleo.

U HAVE SPOKEN IT ALL KAKA, ILA MWIGULU KUMNUNUA ZITTO? DAH ZITO NI HOPLESs SANA PIA MUENDEKEZA NJAA, MIMI NAMDHARAU SANA ZITO,

MWIGULU ALIWEZAJE KUMRUBUNI ZITO KABWE? TABIA HII YA ZITO UKO DUBAI AH WANAUME WANAKUPULIA KISOGONI KIULAINI TENA DAILY
 
Watanzania wameshagundua ulaghai wa CHADEMA.

Nilishasema wewe ni sawa na kile kiungo cha Wanawake kinachotumika kukojolea.
Hakuna hata siku moja uliwahi kuandika kitu chenya maana.

Mbowe ni JABALI ktk siasa za Tanzani kiasi kwamba hata Baba yako Kikwete anamsalute sembuse wewe Kikojoleo. Mtabakia kumshabikia huyo Mzinzi Mwigulu huku Chadema na Mbowe wakiendelea kuchanja mbuga.

Mwaka 2015 sio mbali tutajua nani Zaidi kati ya Mwigulu Mzinzi na Jabali Mbowe?
 
Ni wanafiki tu wasio tambua kazi kubwa aliyo ifanya Kamanda huyu.Nchi hii ilikuwa na utawala wa kifalme wa ccm.Hawakuwa na tishio lolote.mpaka wakajitangazia kuwa ccm itatawala milele.Lakini Mbowe ametokea na kuipindua hali hiyo.Hivi sasa akina Mwigulu wanaogopa hata kivuli chake.Pamoja na ugaidi alio nao ameshindwa kabisa kumsambaratisha Mbowe.Amejaribu kumnunua Zito ili ammalize wapi! imeshindikana.Leo bila aibu ananza kuzungumzia tabia binafisi ya mtu.Badara yakukemea wizi na hujuma na rushwa iliyojaa katika serikali yake na kuporomoka kwa elimu anazungumzia Kivuli cha Mbowe.Mbowe hana serikali,hayuko katika ofisi yoyote ya serikaali wao wanatumia muda wote kupambana naye.Watakwisha tu,watanzania siyo wajinga kudanganywa kwa hoja dhaifu kama za Mwigulu
Wakati Mbowe anasafiri na binti inakuzuia nini ccm kutu letea maendeleo?Kwani yeye Mwigulu mboana alifumaniwa Igunga kwa mke wa mtu kwa kuhonga kodi za Watanzania.Acheni siasa za ubabaishaji na mipasho,hamna lolote mnachezea tu Nchi yetu na kutuchelewesha maendeleo.

Kazi gani aliyofanya ya kucheza disco
 
Chadema ni chama cha kichaga. Wanaoshabikia mafanikio ya mbowe ni wachagga wenzake
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom