Imekuwa kama ada kwa wanaCCM kuanza kumshambulia kila anayejiengua CCM, kuzusha pengine kusema ukweli mambo aliyofanya angali akiwa bado CCM, yakiwemo ya ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma nk, mwisho utawasikia wakimtishia kuwa atafunguliwa mashitaka, atafilisiwa, mali zake kutaifishwa, TRA watambambikia kodi nk. binafsi sijui hasa lengo la kufanya hivyo ni nini.
Inavyoonekana CCM huwa wanajua kabisa fulani ni fisadi wanamuacha aendelee kuihujumu nchi bila kutoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika wakisubiri siku atakapohama chama. Huo ni uzalendo gani, wanaCCM mnatupa picha gani ya humo ndani, ni matendo maovu makubwa kiasi gani mnayovumilia, ina maana unapokuwa CCM ni ruksa kuhujumu taifa?
Picha ya karibu inayoonekana ni kuwa CCM wote wanajuana wanalindana, kwahiyo wanajua kabisa kuna makosa rais Magufuli alifanya na anaendelea kufanya bali wanavumilia likiwemo la uuzwaji holela wa nyumba za serikali, ununuzi wa boti mbovu, leo wanajua anavunja katiba, anabagua kikanda, wanajua anafanya uonevu kwa wasiomchagua, wanajua analipiza visasi kwa mahasimu wake na mengine mengi, ila wanavumilia kwa kuwa bado ni Mkiti wao na yuko CCM, najua kuna siku wanaCCM hao hao wanaomshangilia leo watatuwekea wazi makosa yake yote kama wanavyofanya kwa wengine.
Wakati ni Mwalimu mzuri sana.