Kwa CCM hii, Hata Hayati Nyerere wangemwambia kama Dkt. Bashiru

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,551
11,881
Kama Mungu angemjalia Nyerere Uhai kama kina "Warioba" na "Butiku"
Kwa hii CCM-asali.

Na kama ingetokea Nyerere kuwakosoa CCM hii.
Kama wafanyavyo kina.. Ndugai,Bashiru,Butiku na Warioba!

Yangempata kama yanayowapata hao Makada wakongwe na Watiifu maisha yao yote imekuwa CCM.

Ambao sasa tunaona Michango yao ndani ya uwepo wa CCM mpaka sasa!

Ikisahaulika kwa kasi ya 4G,na badala yake wanatumiwa wahuni wa kisiasa!

Wasio na rekodi yoyote ya maana ndani ya nchi hii.
Na pia ndani ya CCM kwenyewe!

Kwamba kina
Kihongosi -Kashfa ya ubadhirifu mke wake huko Arusha.

Kigwangalla!-Kadhfa ya ubadhirifu Wizarani Maliasili,Pamoja na kumsusa matibabu Baba yake mzazi.

Wewe Musukuma-kashfa ya kumtapeli Bilionare wa Kahama Mbegesera,kwa kulitumia vibaya jina la JPM.
Kwamba angemsaidia kuongea naye.(Mh Hussen mbunge wa Nyangh'wale CCM .alimtumia busara kulimaliza hili

Kibajaji- Anatumia mbinu hii ili arudi na kuingia kundi jipya la Asali Boys.
Ikiwa ni baada ya kulikoroga enzi za JPM kwa kutoa lugha kejeli kwao.
Na alipofariki JPM, Kibajaji akajikuta yuko njiapanda.
Sasa ni kama alipewa upenyo kwa kumtumia Dkt Bashiru ili wamtakase na kumkubali.

Eti hawa ndio wanapata Uthubutu wa kuwakemea watu kama kina Bashiru...bosi wao sliewapigania na kufanikiwa kurudi Bungeni 2020,Chini ya uratibu wake kama katibu Mkuu!

Kwamba wanawaambia kina mzee Butiku na Warioba,wakae pembeni sababu muda wao ulikwisha pita!

Ndio maana kumbe Serikali imeipa kisogo Taasisi ya Mwalimu Nyerere "Foundation"

Sasa tumeijua sababu ni kwamba haikubaliani na Maovu ya watawala.

Alamsikhi.
10101.

JamiiForums1301822419.jpg
 
Kwani nyerere ana maajabu gani kwenye uongozi!!?..kipindi chake watu walipanga foleni ya unga,tembea uchi nguo hakuna,sukari guru,gwanji...acha kumkuza,mwenyewe alikiri alifeli,alikua tu hodari wa kuhutubia
 
KWA hiyo mtaiondoa na kukipa kingine madaraka!!?mtuambie tuchukue kadi!

Ni rasmi Bashiru ni sauti ya NYERERE kupitia Mwl NYERERE foundations!
 
Hata bila sapoti ya wazee, Lowasa asinge mshinda Magufuli tuache kujidanganya.
Sasa kwanini ile ofisi ya masaki ilitumika kudivert matokeo ya Urais ? Halafu Magufuli angewezaje kumshinda Lowassa yaani , kwa lipi hasa ? unadhani waliokuwa wanaiba zile kura walikuwa na akili ndogo kuliko wewe ?

Kwa taarifa yako iliamriwa kura ziibwe baada ya matokeo kuonekana
 
Sasa kwanini ile ofisi ya masaki ilitumika kudivert matokeo ya Urais ? Halafu Magufuli angewezaje kumshinda Lowassa yaani , kwa lipi hasa ? unadhani waliokuwa wanaiba zile kura walikuwa na akili ndogo kuliko wewe ?

Kwa taarifa yako iliamriwa kura ziibwe baada ya matokeo kuonekana
Yaani kama mwana ccm aliyeko upinzani angemshinda mwana ccm aliyeko ccm basi ningeamini usemi wa watu kwamba katika kila watanzania 10, 4 ni vichaa
 
Hata bila sapoti ya wazee, Lowasa asinge mshinda Magufuli tuache kujidanganya.

Ndugu yangu BUSH BIN LADEN

Hao kina johnthebaptist ni ngumu kuwaeleza jambo na wakakuelewa!

Wakati Sisi tunachangia Hoja na hatutafuti vi-hoja kama wanavyofanya vijana wa Ufipa!

Wao wamebaki kuwa chama cha visasi na kugombea vitu maalumu!
Kugombana na kila mtu mwenye mawazo tofauti nao!

Tabia ambayo wamewaambuk8za CCM kwa sasa!

Sasa hawafanyi kazi za msingi kujenga chama,badala yake wamekazania kushinda Mahakamani kugombana na wanawake 19 wale!

Waambie wajenge Hoja waache kukaa wakitabiria mabaya na kugombana na Marehemu!

Wao waliumaliza mwendo na kutuachia Dunia hii tuliopo hai.

Kukaa wakikumbuka mambo ya waliokufa hakuwafanyi kuwa wanasiasa bora!

Wala hakuwezi kukusaidia kupata kura,eti marehemu alikuonea!

Ni juu yao kuuhakkishia Umma kwamba hawajadhoofika na wala hawajasahau kuutetea dhidi ya dhulma za watawala!

Kuendelea kumuita "JIWE" inaonyesha wasivyoaminika na wananchi,sababu hatuna imani na yaliyoko mioyoni mwao

Maana wote wanaugua Maradhi Mabaya Sana.

Yako Ubelgiji!
Yako Canada!
Yako Ufipa na pia humu JF!


Nayo ni Maradhi ya .....



"MAGU-PHOBIA"

Alamsikhi ndugu Yangu...

Erythrocyte
Wafikishie Ujumbe huko UFIPA!

10101.
 
Back
Top Bottom