Kwa "Breaking News", Hongera ITV/Radio One!, Hongera Mtangazaji!.

Wanabodi,
Linapofanyika jambo la kustahili pongezi, tutoe pongezi, na linapofanyika la kustahili shutuma, tuponde.

Leo katika mapumziko yangu ya Sikukuu ya Maulid, nimetokea kuisikia "Breaking News" ya ITV/Radio One kuhusu Vurugu za Dumila huko Morogoro, hivyo nimejikuta ninawiwa kutoa pongezi kwa Kituo hiki cha ITV/Radio One.

Pongezi kuu ni ile tuu walipopata taarifa ya kuwepo vurugu, mara moja wametuma ripota wake wa rredio na TV hivyo ana tu update live kutoka neo la tukio. Morogoro pia kuna reporter wa TBC, Star TV na Channel Ten, nacheza na remote yangu, ni ITV/Radio One tuu ndio wameweza kutupatia update hii, ukiondoa hii ya humu kwenye jf.

Pongezi za pili na kubwa zaidi ni kwa mtangazaji wa zamu anaye tu link na huyo reporter aliyeko eneo la tukio!.
Japo sijaweza kumtambua ni nani kwa jina, ila ni miongoni mwa watangazaji wenye uwezo na kipaji cha hali ya juu ambacho sijabahatika kumsikia mtangazaji mwingine yoyote wa ITV/Radio mwenye uwezo huo!.

Tasnia ya utangazaji, zaidi ya mtu kusomea pia inahitaji kuwa na uwezo na kipaji cha eneo mahsusi, mfano habari, michezo, vipindi vya muziki na eneo la mahojiano!. Karibu vituo vyetu vyote vya TV, havina watangazaji wazuri wenye uwezo wa kuendesha mahojiano ikiondoa wale wa Star TV wanaoendesha "Tuongee Asubuhi" wakitokea Mwanza.

Licha ya ITV kuendesha vipindi kadha vya mahojiano, bado ITV, haina watangazaji mahiri wa mahojiano, ila baada ya kumsikia huyu mtangazaji wa leo, nimemkubali kuwa angalau sasa ITV/Radio One, inae mtangazaji mmoja mahiri wa mahojiano!.

Umahiri wa mtangazaji huyu, umejidhihirisha kwenye mahojiano yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, na kama Rais Kikwete angekuwani kama Nyerere, na akayasikia mahojiano yale, pale pale angenyanyua "Hotline" na kumuamuru Mkurugenzi wa RTD kutangaza kuwa Rais amemfukaza kazi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuanzia saa hiyo!".

Mtangazaji baada ya kupata update ya eneo la tukio, akampandia Mkuu wa Mkoa kwenye mobile!.
Kwanza Bendera alikubali kupokea taarifa za tukio lile.
Mwandishi akamuuliza sababu za vurugu Bendera akajibu sijui!.
Mwandishi akauliza wewe mkuu wa mkoa mzima usijue, sasa nani ajue?,
Bendera akamwambia mwandishi awaulize wale walioko kule!.
Bendera akajitetea niko Dodoma kwenye kikao cha wakuu wa mikoa hivyo asimuulize yeye.
Mwandishi akamng'ang'ania kuwa kwa vile yeye ndiye mkuu wa mkoa, laz`ima kuna maofisa wake wamesha mbrief nini kinaendelea.
Mkuu wa Mkoa akahamaki, kuwa ndio yuko njiani anaelekea Morogoro kujua nini kinaendelea.
Mwandishi akaendelea kumbana Bendera, kwa vile umesema taarifa mlizipata kabla, mlifanya nini kuzuia mpaka vurugu zimetokea?.
Mkuu wa Mkoa anaanza kugomba na ku shout, FFU wamekwenda, jeshi limekwenda, wananchi wako kwa mamia, utawadhibiti vipi?.
Mtangazaji kwa kugundua amemprovoke mkuu wa mkoa na amekasirika, akampooza kwa kumweleza kuwa katika mkoa wa Morogoro, yeye ndiye rais, hivyo kila jambo likotokea, lazima aulizewe yeye.
Mkuu wa mkoa akapoa, akatoa ushirikiano kuwa sasa amevunja mkutano wake wa Dodoma, anakuja neo la tukio kuona hali halisi ndipo wajue cha kufanya. Wakaagana vizuri.

Kitendo cha mtangazaji kumbana mkuu wa mkoa na kisha kumtuliza na kumrudisha kwenye mstari, ni kipaji na uwezo!. Mtangazaji wa mahojiano anapaswa kuwa top ya anamhoji, hata ukimhoji rais, wewe mtangazaji ndio the boss!. Vipindi vingi vya mahojiano, kwa vile wahojiwa ni mawaziri au mabosi fulani, mtangazaji hujisikia "small" hivyo kufanya mahojiano bila "authority" na matokeo yake kushindwa kuwabana wahojiwa na mahojiano kuonekana ni "PR Stunt" with "no impact!".

Hongera sana Mtangazaji wa ITV/Radio One. Hongera Kituo cha ITV/Radio One.

Wasalaam.

Pasco.

NB. Pasco wa JF ni Mtangazaji wa zamani wa Vipindi vya Mahojiano, "Mada Moto", "Kiti Moto" na Ulingo wa Siasa".
Kwa sasa ni Mtayarishaji/Mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea kupitia PPR.

Sasa subiri nini kitatokea kwao ,kwani hilo halitowafurahisha wenye mamlaka ya mamuzi ya Nchi.
 
Pasco kipindi cha Kiti Moto ulichofanya na Mch. Kakobe hakikurushwa baada ya kuwa umerekodi, kuna taarifa kwamba TISS walikuchimba mkwara....funguka
 
Last edited by a moderator:

Afunguke!!Mabwepande akujui?Nimeshauri akirudishe au atafute jina lingine arudi na maudhui yaleyale!Ila na Mikingamo Ya RTD nayo ya Kipozi ilipotezwa!
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi vurugu kila sehemu. Mtwara, Kigamboni, Zanzibar, Dumila, Kibiti...

Usipoziba ufa, utajenga ukuta.

Nchi inawashinda watwawala.

Nyamongo, Byankulu, Geita, Kariakoo ... Inatia wasi wasi sana. Viongozi wanapokuwa wapo wapo tu.
 
Licha ya serikali kukipigia debe kwa nguvu zote king'amuzi matokeo yake mikoa inayo tumia kifaa hicho hawatizami muchuano ya AFCON huko A.Kusini cha kushangaza na cha kulitia aibu Taifa hili ni kwa kastation kadogo ka TV pale Morogoro karusha AFCON mechi zote LIVE bila chenga nako ni ABOOD TV au ATV nashangaa TBC chombo cha taifa kinashindwaje kurusha mawimbi ili kila mlipa kodi afaidi? Badala yake station ndogo Moro inawapa raha wakazi wa mji huo. Ndo maana michezo inadorola katika nchi watendaji wapo kwenye usingizi mzito badilikeni jamani.
 
Wanabodi,
Linapofanyika jambo la kustahili pongezi, tutoe pongezi, na linapofanyika la kustahili shutuma, tuponde.

Leo katika mapumziko yangu ya Sikukuu ya Maulid, nimetokea kuisikia "Breaking News" ya ITV/Radio One kuhusu Vurugu za Dumila huko Morogoro, hivyo nimejikuta ninawiwa kutoa pongezi kwa Kituo hiki cha ITV/Radio One.

Pongezi kuu ni ile tuu walipopata taarifa ya kuwepo vurugu, mara moja wametuma ripota wake wa rredio na TV hivyo ana tu update live kutoka neo la tukio. Morogoro pia kuna reporter wa TBC, Star TV na Channel Ten, nacheza na remote yangu, ni ITV/Radio One tuu ndio wameweza kutupatia update hii, ukiondoa hii ya humu kwenye jf.

Pongezi za pili na kubwa zaidi ni kwa mtangazaji wa zamu anaye tu link na huyo reporter aliyeko eneo la tukio!.
Japo sijaweza kumtambua ni nani kwa jina, ila ni miongoni mwa watangazaji wenye uwezo na kipaji cha hali ya juu ambacho sijabahatika kumsikia mtangazaji mwingine yoyote wa ITV/Radio mwenye uwezo huo!.

Tasnia ya utangazaji, zaidi ya mtu kusomea pia inahitaji kuwa na uwezo na kipaji cha eneo mahsusi, mfano habari, michezo, vipindi vya muziki na eneo la mahojiano!. Karibu vituo vyetu vyote vya TV, havina watangazaji wazuri wenye uwezo wa kuendesha mahojiano ikiondoa wale wa Star TV wanaoendesha "Tuongee Asubuhi" wakitokea Mwanza.

Licha ya ITV kuendesha vipindi kadha vya mahojiano, bado ITV, haina watangazaji mahiri wa mahojiano, ila baada ya kumsikia huyu mtangazaji wa leo, nimemkubali kuwa angalau sasa ITV/Radio One, inae mtangazaji mmoja mahiri wa mahojiano!.

Umahiri wa mtangazaji huyu, umejidhihirisha kwenye mahojiano yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, na kama Rais Kikwete angekuwani kama Nyerere, na akayasikia mahojiano yale, pale pale angenyanyua "Hotline" na kumuamuru Mkurugenzi wa RTD kutangaza kuwa Rais amemfukaza kazi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuanzia saa hiyo!".

Mtangazaji baada ya kupata update ya eneo la tukio, akampandia Mkuu wa Mkoa kwenye mobile!.
Kwanza Bendera alikubali kupokea taarifa za tukio lile.
Mwandishi akamuuliza sababu za vurugu Bendera akajibu sijui!.
Mwandishi akauliza wewe mkuu wa mkoa mzima usijue, sasa nani ajue?,
Bendera akamwambia mwandishi awaulize wale walioko kule!.
Bendera akajitetea niko Dodoma kwenye kikao cha wakuu wa mikoa hivyo asimuulize yeye.
Mwandishi akamng'ang'ania kuwa kwa vile yeye ndiye mkuu wa mkoa, laz`ima kuna maofisa wake wamesha mbrief nini kinaendelea.
Mkuu wa Mkoa akahamaki, kuwa ndio yuko njiani anaelekea Morogoro kujua nini kinaendelea.
Mwandishi akaendelea kumbana Bendera, kwa vile umesema taarifa mlizipata kabla, mlifanya nini kuzuia mpaka vurugu zimetokea?.
Mkuu wa Mkoa anaanza kugomba na ku shout, FFU wamekwenda, jeshi limekwenda, wananchi wako kwa mamia, utawadhibiti vipi?.
Mtangazaji kwa kugundua amemprovoke mkuu wa mkoa na amekasirika, akampooza kwa kumweleza kuwa katika mkoa wa Morogoro, yeye ndiye rais, hivyo kila jambo likotokea, lazima aulizewe yeye.
Mkuu wa mkoa akapoa, akatoa ushirikiano kuwa sasa amevunja mkutano wake wa Dodoma, anakuja neo la tukio kuona hali halisi ndipo wajue cha kufanya. Wakaagana vizuri.

Kitendo cha mtangazaji kumbana mkuu wa mkoa na kisha kumtuliza na kumrudisha kwenye mstari, ni kipaji na uwezo!. Mtangazaji wa mahojiano anapaswa kuwa top ya anamhoji, hata ukimhoji rais, wewe mtangazaji ndio the boss!. Vipindi vingi vya mahojiano, kwa vile wahojiwa ni mawaziri au mabosi fulani, mtangazaji hujisikia "small" hivyo kufanya mahojiano bila "authority" na matokeo yake kushindwa kuwabana wahojiwa na mahojiano kuonekana ni "PR Stunt" with "no impact!".

Hongera sana Mtangazaji wa ITV/Radio One. Hongera Kituo cha ITV/Radio One.

Wasalaam.

Pasco.

NB. Pasco wa JF ni Mtangazaji wa zamani wa Vipindi vya Mahojiano, "Mada Moto", "Kiti Moto" na Ulingo wa Siasa".
Kwa sasa ni Mtayarishaji/Mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea kupitia PPR.
Nashukuru kwamba leo hujaikana hii ID yako. Huwa nakukubali sana japo mara nyingi tunatofautiana kimtazamo humu jamvini .Namini ipo siku utarudi na kipindi kama kile cha Kiti Moto .

Kuhusu huyo mwandishi wa ITV kweli anastahili pongezi, pia kuna jambo la kustaajabisha limetokea la Mkuu wa Mkoa kutofautia maelezo na DC wake ,ule ni udhaifu wa dola, HAKUNA UTAWALA BORA pale .
 
Ametimiza wajibu wake

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hizi vurigu zinaashiria hali si salama kabisa, tunakoelekea si kwema kabisa, hivi usalama wa taifa wako wapi?, huwa hawaoni haya mpaka yanatokea, sasa wanafanya nini?
usalama wa taifa kazi yao huishia kuchakachua kura ili ccm washinde, baada ya hapo wao ni kupumzika mpaka uchaguzi mwingine.wakijitahidi sana basi utawakuta wakati wa mitihani ya Taifa.wewe si unaona wanyarwanda wanaingia na kufanya vitu vyao wanavyo taka na kuondoka, hapo utasema tuna usalama wa taifa kweli.
 
Mkuu hapo kwa semunyu nadhani umeteleza. Nitakukumbusha watu wachache aliowahi kuwahoji akawa anababaika kuwadhibiti ni pamoja na episodes za Lowasa, Juma Duni, Philip Mulugo, Membe na Wasira!
Kama ulifuatilia mahojiano yao katika kipindi chake cha Dk. 45 utakubaliana nami.
Nadhani ilikuwa bahati mbaya sana nilikumbana na Semunyu akiwahoji hao, toka hapo nilikosa radha kumfuatilia.
 
Back
Top Bottom