Kwa "Breaking News", Hongera ITV/Radio One!, Hongera Mtangazaji!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Linapofanyika jambo la kustahili pongezi, tutoe pongezi, na linapofanyika la kustahili shutuma, tuponde.

Leo katika mapumziko yangu ya Sikukuu ya Maulid, nimetokea kuisikia "Breaking News" ya ITV/Radio One kuhusu Vurugu za Dumila huko Morogoro, hivyo nimejikuta ninawiwa kutoa pongezi kwa Kituo hiki cha ITV/Radio One.

Pongezi kuu ni ile tuu walipopata taarifa ya kuwepo vurugu, mara moja wametuma ripota wake wa rredio na TV hivyo ana tu update live kutoka neo la tukio. Morogoro pia kuna reporter wa TBC, Star TV na Channel Ten, nacheza na remote yangu, ni ITV/Radio One tuu ndio wameweza kutupatia update hii, ukiondoa hii ya humu kwenye jf.

Pongezi za pili na kubwa zaidi ni kwa mtangazaji wa zamu anaye tu link na huyo reporter aliyeko eneo la tukio!.
Japo sijaweza kumtambua ni nani kwa jina, ila ni miongoni mwa watangazaji wenye uwezo na kipaji cha hali ya juu ambacho sijabahatika kumsikia mtangazaji mwingine yoyote wa ITV/Radio mwenye uwezo huo!.

Tasnia ya utangazaji, zaidi ya mtu kusomea pia inahitaji kuwa na uwezo na kipaji cha eneo mahsusi, mfano habari, michezo, vipindi vya muziki na eneo la mahojiano!. Karibu vituo vyetu vyote vya TV, havina watangazaji wazuri wenye uwezo wa kuendesha mahojiano ikiondoa wale wa Star TV wanaoendesha "Tuongee Asubuhi" wakitokea Mwanza.

Licha ya ITV kuendesha vipindi kadha vya mahojiano, bado ITV, haina watangazaji mahiri wa mahojiano, ila baada ya kumsikia huyu mtangazaji wa leo, nimemkubali kuwa angalau sasa ITV/Radio One, inae mtangazaji mmoja mahiri wa mahojiano!.

Umahiri wa mtangazaji huyu, umejidhihirisha kwenye mahojiano yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, na kama Rais Kikwete angekuwani kama Nyerere, na akayasikia mahojiano yale, pale pale angenyanyua "Hotline" na kumuamuru Mkurugenzi wa RTD kutangaza kuwa Rais amemfukaza kazi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuanzia saa hiyo!".

Mtangazaji baada ya kupata update ya eneo la tukio, akampandia Mkuu wa Mkoa kwenye mobile!.
Kwanza Bendera alikubali kupokea taarifa za tukio lile.
Mwandishi akamuuliza sababu za vurugu Bendera akajibu sijui!.
Mwandishi akauliza wewe mkuu wa mkoa mzima usijue, sasa nani ajue?,
Bendera akamwambia mwandishi awaulize wale walioko kule!.
Bendera akajitetea niko Dodoma kwenye kikao cha wakuu wa mikoa hivyo asimuulize yeye.
Mwandishi akamng'ang'ania kuwa kwa vile yeye ndiye mkuu wa mkoa, laz`ima kuna maofisa wake wamesha mbrief nini kinaendelea.
Mkuu wa Mkoa akahamaki, kuwa ndio yuko njiani anaelekea Morogoro kujua nini kinaendelea.
Mwandishi akaendelea kumbana Bendera, kwa vile umesema taarifa mlizipata kabla, mlifanya nini kuzuia mpaka vurugu zimetokea?.
Mkuu wa Mkoa anaanza kugomba na ku shout, FFU wamekwenda, jeshi limekwenda, wananchi wako kwa mamia, utawadhibiti vipi?.
Mtangazaji kwa kugundua amemprovoke mkuu wa mkoa na amekasirika, akampooza kwa kumweleza kuwa katika mkoa wa Morogoro, yeye ndiye rais, hivyo kila jambo likotokea, lazima aulizewe yeye.
Mkuu wa mkoa akapoa, akatoa ushirikiano kuwa sasa amevunja mkutano wake wa Dodoma, anakuja neo la tukio kuona hali halisi ndipo wajue cha kufanya. Wakaagana vizuri.

Kitendo cha mtangazaji kumbana mkuu wa mkoa na kisha kumtuliza na kumrudisha kwenye mstari, ni kipaji na uwezo!. Mtangazaji wa mahojiano anapaswa kuwa top ya anamhoji, hata ukimhoji rais, wewe mtangazaji ndio the boss!. Vipindi vingi vya mahojiano, kwa vile wahojiwa ni mawaziri au mabosi fulani, mtangazaji hujisikia "small" hivyo kufanya mahojiano bila "authority" na matokeo yake kushindwa kuwabana wahojiwa na mahojiano kuonekana ni "PR Stunt" with "no impact!".

Hongera sana Mtangazaji wa ITV/Radio One. Hongera Kituo cha ITV/Radio One.

Wasalaam.

Pasco.

NB. Pasco wa JF ni Mtangazaji wa zamani wa Vipindi vya Mahojiano, "Mada Moto", "Kiti Moto" na Ulingo wa Siasa".
Kwa sasa ni Mtayarishaji/Mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea kupitia PPR.
 
Dah, kama ndio yule mtoto wa Mayala basi, heshima kwako kaka...nakukubali sana, hasa kwenye zile mbwembwe zako za kusifia kila bila kwenye maonesho yenu ya biashara/kilimo i.e 7/7, 8/8....we mbbayaaaaah!
 
pasko unanikumbusha mahojiano yako nilikuwa mdogo sana wakati huo, sijui darasa la ngapi, ulikuwa unamuhoji bwana mapesa, basi akaanza kukungangania na lafudhi yake ya kisukuma "wewe mayala wewe wewe mayala wewe embu sikiliza" mpaka leo bado nakumbuka siku ile
 
Hizi vurigu zinaashiria hali si salama kabisa, tunakoelekea si kwema kabisa, hivi usalama wa taifa wako wapi?, huwa hawaoni haya mpaka yanatokea, sasa wanafanya nini?
 
Kwa hiyo hapa unachopongeza kwa maneno meeeengi yote hao ni nini. ITV si ni chombo cha habari? Kazi yake ni nini. Walichokifanya ni wajibu wao wa kila siku, wa kutoa habari. Binafsi mimi nakushangaa uliyeleta post na nadhani unafanya kazi ITV!
 
Nimepata bahati ya kusikia hayo mahojiano, kwa kweli jamaa kambana sana Bendera.
Ila jamaa kawaka mpaka ikabidi jamaa ampoze tena kama ulivyoeleza hapo juu.
Ila yale si majibu ambayo mtu kama mkuu wa mkoa alitakiwa kujibu, dah.
 
Kwa hiyo hapa unachopongeza kwa maneno meeeengi yote hao ni nini. ITV si ni chombo cha habari? Kazi yake ni nini. Walichokifanya ni wajibu wao wa kila siku, wa kutoa habari. Binafsi mimi nakushangaa uliyeleta post na nadhani unafanya kazi ITV!
Kwani, mtu huwa anapongezwa kwa
kutekeleza wajibu wa mwingine? Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni...
 
Ni kweli kabiasaa pasco uliyoyasema ndiyo maana mimi hupinga tabia yako ya kupenda bahasha kwani kama umepokea bahasha kwa mtu unaeenda kumhoji ni vigumu sana mkubana naamini sasa wewe Pasco umejifunza kitu...huwa na huzuria baadhi ya press waandishi huwa wanyonge sana kwa watakao wahoji yaani wanabaki kumsikiliza atakacho kisema kisha kusubili chai au lunch na kama utamubana hiyo lunch utaisikia tu...
 
Pasco na wewe hujajua chanzo cha vurugu!
kwa kuwa umeishia kusifia tuu bula kutujuza na sisi

Wafunga barabara kuu ya kuelekea dodoma na kufanya fujo kama inavyoonekana katika picha msururu wa magari ya abiria na mizigo yakiwa upande wa kutoka Dumila kwendaa Kilosa yakisubiri kufunguliwa kwa Barabara ya Kilosa – Dumila,Wilaya ya Kilosa, baada ya wananchi wenye
hasira kufunga njia hiyo kwa kuweka mawe makubwa na magogo ili kushinikisha kusikilizwa na kutekelezewa madai yao dhidi ya wafugaji kama yalivyokutwa Msowero

Ni vurugu za wakulima na wafugaji!

HASARA YA FUJO..JPG HASARA YA FUJO..JPG

MSURURU WA MAGARI..JPG

KUPITA KWA SHIDA..JPG
KUBEBA BAISKERI KUFUNGA NJIA..JPG

BANGO..JPG
 
Pasco sijafanikiwa kusikiliza, lakini mambo uliyosema hapo ni sahihi ITV na redio one wanatakiwa wapate watu wanaoweza kuongoza mahojiano. Kwa sasa ITV na Redio one ndio kama vyombo vya habari vya taifa kwa sababu vinafuata misingi na wamekuwa wakijitahidi kuminimize bias.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo hapa unachopongeza kwa maneno meeeengi yote hao ni nini. ITV si ni chombo cha habari? Kazi yake ni nini. Walichokifanya ni wajibu wao wa kila siku, wa kutoa habari. Binafsi mimi nakushangaa uliyeleta post na nadhani unafanya kazi ITV!

Uwezo wako wa kufikiri ni mfupi sawa na urefu wa pua yako!
 
Aah kumbe Pasco wa Jf ni wewe yule wa PPRT? Kaka punguza mbwembwe kwenye maonesho ya 77 na 88! Yaani hii bidhaa imezalishwa hapa hapa Tz? Umefanya vizuri kuwapa somo hao waandishi uchwara wa siku hizi! Eti TBC wanamtegemea Gabriel Zakaria!
 
Pasco ukipata wadhamini vipi?
utakubali kuendesha kipindi mfano wa LARRY kING LIVE?
 
Haiwezekani kwamba humjui jina. Kwani wakimalizia si huwa wanasema, nikiripoti toka ... ni mimi... Kama ulitaka kumpaisha ungempaisha na jina kabisa
 
Back
Top Bottom