Kwa binadamu wengi, siku za maisha(hata ya kisiasa) zikifika mwisho hukimbilia kwa Mungu

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Hii ni kawaida,pale binadamu anapofikia kikomo cha jambo fulani,iwe maisha au chochote,huwa mtu wa imani sana na kumrudia muumba wake

Kwa wakristo,basi kama mtu ni mgonjwa sana hubatizwa, na kurudishwa katika imani,na hata yeye mwenyewe husali sana.

Kusali huku ni kutafuta divine intervention

Hiki ndicho nakiona kwa bashite, BASHITEGATE imemfanya akose majibu ya kisayansi ya kidunia na hivyo kutafuta "cover" kwenye imani ya dini bila kujua wakati mwingine vitu hivi huingiliana na hata maneno ya Mungu hayaku-rule out kuyatimiza yale ya duniani,maneno ya Mungu yanatutaka tuyatimize ya duniani.

Kuna mahala imeandikwa "mpe kaisari (mtawala wa dunia)yaliyo yake, na Mungu mpe yaliyo yake"

Kaisari anataka vyeti vya elimu vya bashite,na hata Mungu anajua ni haki kwa kaizari kudai vyeti vya elimu kutoka kwa bashite.Nadhani Mwenyezi Mungu anamwambia Bashite "nenda kwa kaizari.....malizana naye kwanza (mpe vyeti) ndipo uje useme nami......"

Sakata la madawa ya kulevya litashughulikiwa kwa weledi na walio na mamlaka kama kaisari alivyowateua na kuwapangia,kuondoka kwake ni sawa na kuvunjika kwa kwa mpini,haituzuii kuendelea kulima,jembe lipo,na mpini(Tume ya kushughulikia madawa)ipo, na watu wa kuziba nafasi ya mkuu wa mkoa wapo

Hakuna aliye juu ya mifumo ya nchi,wote tunaishi chini ya,na kuongozwa na mifumo hiyo,ukijiinua juu ya mifumo,mifumo itakushusha hadi katika nafasi yako au "itakucheua" ukiingilia mifumo ya nchi iliyowekwa kwa mujibu wa sheria,mifumo INA tabia ya kujitetea na yenyewe itabaki,wewe utaondoka
 
Kuna mahala imeandikwa "mpe kaisari (mtawala wa dunia)yaliyo yake, na Mungu mpe yaliyo yake"

Kaisari anataka vyeti vya elimu vya bashite,na hata Mungu anajua ni haki kwa kaizari kudai vyeti vya elimu kutoka kwa bashite.
siku hizi jamaa anapiga roots za kwa mashekh na kanisani kuombewa ili Mungu atende muujiza kuyabadili matokeo ya Daudi Bashite kwenye cheti kua kama ya Paul Muyenge. Hatari sana
 
Yuko mtegoni......anajua hii kashfa ikipenya sawa sawa,atakosa identity(utambulisho) manake atakuwa hana jina

Kama huna jina linalotambulika,utaombaje kazi?

Utagombea ubunge kwa jina lipi?

Uhamiaji na watu wa RITA wamekaa mkoa wa kula kichwa

Polisi wanasubiri,takukuru wanasubiri kuona alivyopata mshahara kwa utambulisho feki

Kimsingi huyu ndugu yuko njia panda .....hasa katika kazi zinazohusisha 'umma" cha kufanya atafute mambo binafsi tu kama biashara
siku hizi jamaa anapiga roots za kwa mashekh na kanisani kuombewa ili Mungu atende muujiza kuyabadili matokeo ya Daudi Bashite kwenye cheti kua kama ya Paul Muyenge. Hatari sana
 
  • Thanks
Reactions: 999
Yuko mtegoni......anajua hii kashfa ikipenya sawa sawa,atakosa identity(utambulisho) manake atakuwa hana jina

Kama huna jina linalotambulika,utaombaje kazi?

Utagombea ubunge kwa jina lipi?

Uhamiaji na watu wa RITA wamekaa mkoa wa kula kichwa

Polisi wanasubiri,takukuru wanasubiri kuona alivyopata mshahara kwa utambulisho feki

Kimsingi huyu ndugu yuko njia panda .....hasa katika kazi zinazohusisha 'umma" cha kufanya atafute mambo binafsi tu kama biashara
kwakweli hili swala ni zito kwake. ila haina haja ya kumbeba kwani haitakua haki kwa wazito kubebwa huku wanyonge wakinyongewa.
sheria iwe msumeno
 
Mkuu iparamasa nimekusoma sawia na napatana kiasi kikubwa na mang'amuzi yako.
Nimefuatilia kwa makini mwenendo wa mambo yanavyomwendea huyo dogo (napenda kumwita Dogo Misifa). Hivi majuzi Waziri anayehusika na masuala ya wasanii ametokeza mfululizo ktk media akisema kwa ustadi mkubwa, kwa ufasaha na kwa kujiamini kuhusiana na mwenendo vita ya madawa ya kulevya ilivyochezewa ngoma na dogo, na waziri huyu akatoa maoni yake kwa ufasaha na hekima ambayo huwa sipendi kuamini kuwa anayo.

Huwa sijawahi kumsifia kwa lolote huyu waziri kijana kutokana na historia yake kama mpiga debe wa kundi tawala (na naomba radhi, huenda nina chuki binafsi na huyu bwana). Lakini hoja aliyoitoa huyu waziri kijana kuhusiana na dogo alivyo kurupuka na suala la vita ya madawa ya kulevya bila sheria, busara na kulifanya kisiasa, ilinifanya nifikiri kuwa yumkini alikuwa anatoa dokezo ya kinachoendelea nyuma ya pazia kuhusiana na hatima ya dogo.

Ikumbukwe kuwa ktk awamu ya pili ya utawala uliopita wakati huyu waziri kijana akiwa mpiga debe (vuvuzela) wa watawala aliwahi kutoka katika medi na kusema kwa uhakika kuwa 'kuna mawaziri wazembe ktk serikali na lazima wawajibishwe'. Muda si mrefu kweli mzee wa kaya (wakati huo) akawamwaga kundi la mawaziri.

Nikiwa bado nasikilizia maoni ya huyu waziri kijana ghafla dogo katokezea kanisani na akachukua significant coverage in a very inappropriate forum akilialia tu bila hoja yenye mashiko mintarafu ktk mazingira ya ibada. Sasa nikiunganisha mbili na mbili naona yumkini mstakabali si shwari kwa Dogo Misifa.
Nawaza kwa sauti tu.
 
Yuko mtegoni......anajua hii kashfa ikipenya sawa sawa,atakosa identity(utambulisho) manake atakuwa hana jina

Kama huna jina linalotambulika,utaombaje kazi?

Utagombea ubunge kwa jina lipi?

Uhamiaji na watu wa RITA wamekaa mkoa wa kula kichwa

Polisi wanasubiri,takukuru wanasubiri kuona alivyopata mshahara kwa utambulisho feki

Kimsingi huyu ndugu yuko njia panda .....hasa katika kazi zinazohusisha 'umma" cha kufanya atafute mambo binafsi tu kama biashara

Still Bashite lazima aingie lupango siyo chini ya miaka saba kwa kutumia cheti cha rafiki yake, rafiki kwa sababu original Makonda hakuripoti polisi kama aliibiwa au kapotelewa na cheti cha kidato cha nne unless mfumo wa serikali haupo sawa, yaani TAKUKURU, Police- DPP na vetting committee haifanyi kazi kwa weledi! hapa kazi tu!!!!
 
Vetting committee ina shida,inakuwaje jina la mtu linapenya mpaka magogoni bila kujua undani wake? Hawa jamaa wameshamuingiza chaka mkuu mara ngapi?

TCU na NECTA ,NACTE wajiandae kutoka Maelezo ya kina kwa nini hii ilitokea na wana mkakati gani wa kudhibiti suala hili ....detailed kabisa.

Kama mkuu wa kaya "anaingizwa mjini" na kijana aliyezaliwa kolomije, hawa waliozaliwa na kukulia Dar watamuingiza chaka baya zaidi
Still Bashite lazima aingie lupango siyo chini ya miaka saba kwa kutumia cheti cha rafiki yake, rafiki kwa sababu original Makonda hakuripoti polisi kama aliibiwa au kapotelewa na cheti cha kidato cha nne unless mfumo wa serikali haupo sawa, yaani TAKUKURU, Police- DPP na vetting committee haifanyi kazi kwa weledi! hapa kazi tu!!!!
 
sasa hapo sijaelewa... yule kiumbe ameenda kanisani halafu huku akateuliwa huyu jamaa kushika nafasi au?
 
Attachments

  • Screenshot (8).png
    Screenshot (8).png
    90.5 KB · Views: 35
Kwa % kubwa wengi huwa hivyo, huona 'nimeona na kufanya yote kilichobaki nijihakikishie makao huko niendako' lakini hii si kwa kesi ya RC, RC anatafuta huruma za raia alianzia pale alipoonesha vitoto kwenye mkutano na baadaye vyombo vya habari.

Akaanza kwenda kwa mashehe na kudai anataka kutupiwa majini, picha zake na mashehe, wahindu na mapadri zimekua nyingi siku hizi kushinda akiwa na viongozi wa GSM, akaenda kwenye mkutano wa RCC akaanza kuhusisha matatizo yake na swala la kufoji vyeti.

Jana imekuja video jamaa analia, hivi kwa roho mbaya yake ya kuagiza watu wakutane central, kuwalaza watu mahabusu, kufungua kesi za visasi na kuita watu vichaa huyu ni wa kulia? Ana machozi yamebaki? Alikua ana sababu ya kututangazia kila anapofanya safari ya kwenda kufanyiwa maombi?

Siku hizi interview anazikimbia, ila nahisi kuna namna tunaweza kuoneshwa vyeti, mtu mwenye tuhuma kama hizi asingekaa kimya isipokua akiwa anashughulikia hilo swala chini chini.

Huyu anaomba huruma ya wananchi, siyo kweli kwamba anafika mwisho hivyo anamtafuta Mungu anamtafutaje na alishajiona yeye ni mungu.
 
Ndio maana mtoto wangu vyeti vyangu simuonyeshi kamwe, nasisitiza tu mwanangu soma, maana baada ya kuzungusha nimempa majina ya ukoo yote mawili such that Mwakiposta mpya Mwakiposta mpya, ahaaa Sasa Daudi bashite amelikoroga ,Ningempa jina langu kwa mbwembwe zangu ningeumbuka maana walimu wanaomfundisha wananifahamu, Sasa Koromije ndio shidaa kwa bashite anafahamika huko
 
Mkuu iparamasa nimekusoma sawia na napatana kiasi kikubwa na mang'amuzi yako.
Nimefuatilia kwa makini mwenendo wa mambo yanavyomwendea huyo dogo (napenda kumwita Dogo Misifa). Hivi majuzi Waziri anayehusika na masuala ya wasanii ametokeza mfululizo ktk media akisema kwa ustadi mkubwa, kwa ufasaha na kwa kujiamini kuhusiana na mwenendo vita ya madawa ya kulevya ilivyochezewa ngoma na dogo, na waziri huyu akatoa maoni yake kwa ufasaha na hekima ambayo huwa sipendi kuamini kuwa anayo.

Huwa sijawahi kumsifia kwa lolote huyu waziri kijana kutokana na historia yake kama mpiga debe wa kundi tawala (na naomba radhi, huenda nina chuki binafsi na huyu bwana). Lakini hoja aliyoitoa huyu waziri kijana kuhusiana na dogo alivyo kurupuka na suala la vita ya madawa ya kulevya bila sheria, busara na kulifanya kisiasa, ilinifanya nifikiri kuwa yumkini alikuwa anatoa dokezo ya kinachoendelea nyuma ya pazia kuhusiana na hatima ya dogo.

Ikumbukwe kuwa ktk awamu ya pili ya utawala uliopita wakati huyu waziri kijana akiwa mpiga debe (vuvuzela) wa watawala aliwahi kutoka katika medi na kusema kwa uhakika kuwa 'kuna mawaziri wazembe ktk serikali na lazima wawajibishwe'. Muda si mrefu kweli mzee wa kaya (wakati huo) akawamwaga kundi la mawaziri.

Nikiwa bado nasikilizia maoni ya huyu waziri kijana ghafla dogo katokezea kanisani na akachukua significant coverage in a very inappropriate forum akilialia tu bila hoja yenye mashiko mintarafu ktk mazingira ya ibada. Sasa nikiunganisha mbili na mbili naona yumkini mstakabali si shwari kwa Dogo Misifa.
Nawaza kwa sauti tu.
Unganisha hapo mwenye ikulu alimsifia sana huyo waziri kijana mbele ya wananchi akimtaja kuwa ni jembe lake linalofanya kazi nila mfano. Tangua ameingia Ikulu huyu mkuu sana hajawahi kumsifia waziri yyt kwa kiwango hicho. Hvy naunga mkono hoja mkuu
 
Jamaa naona amemkamata punda mkia kinachofuatia ni punda kupiga mateke kwa miguu yake yote miwili
 
Jamaa naona amemkamata punda mkia kinachofuatia ni punda kupiga mateke kwa miguu yake yote miwili
 
Pale mungu anapo mtafuta Mungu,Jamaa ni bonge La comedian anatafuta huruma ya wananchi na anajua kucheza na mind na matukio ,yeye ana kifua atulie moto ukiuanzisha ujue na kuuzima,unajua kuurudisha brand,CV,image,iliyochafuliwa sio Kazi rahisi sana.
 
sasa hapo sijaelewa... yule kiumbe ameenda kanisani halafu huku akateuliwa huyu jamaa kushika nafasi au?
Wakuu wa wilaya wana utaratibu wa kukaimu nafasi ya ukuu wa mkoa kama mkuu wa mkoa ametoka kidogo au yuko na tatizo.

Ni kawaida hiyo!
 
Back
Top Bottom