Kwa bei hizi ni akina nani hununua bidhaa kutoka maduka ya Street Soul ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza?

Mkuu funzadume umeongea ukweli nakuunga mkono mitumbani kunakuwaga na 'mabelo' yanapofunguliwa tu kuna nguo original unadaka kwa bei chee....Kuna kipindi nilipata new balance Kali ya mtumba naamini ilikuwa grade ya juu Kama sio OG kabisa ......!!
 
Mimi huagiza mavazi nje. Bei ya chini ya Mkanda niliowahi kuchukua ilikuwa dola 60 pasipo gharama za kusafirisha wala ushuru TZ. Hivyo nikinunua mkanda kama huo, na kuusafirisha, jumlisha na kodi gharama zake zitakuwa ni zaidi ya 180,000/=. Hivyo sioni tatizo hapo. Kila mtu huona majani ni yale yaliyopo kwenye urefu wa kamba yake.
 
Kungekuwa hakuna wateja wangekuwa washafunga maduka yao.

Nadhani hatufanani, mtu kama Mo hawez kwenda kupanga folen kkoo kununua mkanda, au hawez kusubir masai apitishe ndo anunue.
Masai ndio mikanda yangu hiyo kuna siku nilienda karume kununua mkanda wa ngozi wananiambia 30k mara 50k nikaona isiwe tabu mikanda yenyewe imeshavaliwa bhana ngoja nipitie kwa masai
 
Back
Top Bottom