Kwa bei hizi ni akina nani hununua bidhaa kutoka maduka ya Street Soul ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza?

Namkubali Magu awamu hii katunyoosha. Maduka haya wengi walikua watakatisha fedha. Huwezi kuuza sidiria milioni moja. Wengi wamefunga sponsors wapo juu ya mawe.
Utakufa masikini unamshukuru Mungu maduka ya matajiri kufungwa badala uombe Mungu uwe Tajiri ukafanye shopping kwenye hayo maduka.

Endelea kuishi kifukara Tofari la udongo wewe.
 
Wakuu nimekuwa nikiona matangazo ya bidhaa zinazouzwa na maduka ya STREET SOUL yaliyopo Kijitonyama na Mlimani City hapa Dar es Salaam. pia Street Soul ya AIM Arusha na CITY MALL Mwanza.

Bei za bidhaa kutoka maduka haya zinanifikirisha bila majibu.

Ni Watanzania gani wenye uwezo wa kununua mkanda wa kiunoni kwa laki mbili na elfu hamsin (250000)? Open shoes kwa 295000?
kibaiskeli kwa 950,000?

Je ni akina nani hununua bidhaa kutoka duka hili? Chupi ambayo ukienda kariako inauzwa 1000 yeye anainadi kwa 15000 ahahah wonders shall never end kwakeliView attachment 1642875View attachment 1642874View attachment 1642876View attachment 1642873View attachment 1642872View attachment 1642877

View attachment 1642879View attachment 1642878
Hapo sijakuelewa, Unaongelea bei au ubora kwa bidhaa? kwani kama ubora ni mzuri hizo bei ni za kawaida, ukitaka bidhaa bora na bei yake itakua juu.
 
Sio AK's tu. Hata lile duka lao la viatu tulilotegemea miaka nenda SERVICE LTD limefungwa. Yule mhudumu wa pale ndio kaliridhi lkn Hana mapigo ya Service ltd.
Hapakua na kiatu Cha chini ya laki hata ndala.

Yani wale jamaa bidhaa zao zilikuwa za ubora haswa!
Mashati hayachoki wala kupauka, mabegi yao nayo yalikuwa MashaAllah,

Bidhaa zao kwa ujumla zilikuwa ghali lakini ubora nao ulikuwa wakuridhisha!
 
Sio AK's tu. Hata lile duka lao la viatu tulilotegemea miaka nenda SERVICE LTD limefungwa. Yule mhudumu wa pale ndio kaliridhi lkn Hana mapigo ya Service ltd.
Hapakua na kiatu Cha chini ya laki hata ndala.

Inasemekana walipigwa makodi ya hatari , wakalipa na kurudi zao Ulaya!

Ni kama wakasema ule wimbo wa “wenye kwenu kwa kheri “ nawatakia maisha mema!
 
Baada ya AK’s kwa bongo duka gani lingine linaweza kuuza bidhaa zenye ubora kama ule?

Tuambiane machimbo jamani
 
Kuna watu kununua kitu chenye bei kubwa sehemu classic kwao ndio fahari,

Anafika hakuna foleni, Sio huku kwetu umeshika tuu shati unasikia hukoo "Achaaa hio yangu nshachagua", Ananunua huku anapigwa na kiyoyozi, Anawekewa kwenye package nzuri, anaokota business card anasepa.

Sisi wa K.KOO unanunua huku unaaficha waleti vibaka wasije pita nayo, pembeni ashasimama kijana kukuuzia mfuko mbadala(Super sokoni), ukitoka nje unakutana na muuza maji baridi ya mia 300 kwenye boksi maana anakuona unavyotoka jasho, Hujakaa vizuri ushapigwa kikumbo na wabeba Maroba, halafu bora anyamaze, akugonge yeye lkn anaenda huku anakushushia matusi wewe, ukitoka sasa barabarani ndio unakutana na wauza mikanda ya Buku Jero, sababu ndio level zako unanunua, Ukifika nyumbani ukivaa kua mstaarabu, maana ukicheka tuu au kukohoa umekatika.

Ha hahahahaha. Tena wanoenda izo special shops hamna hata kupatana......hakuna ooohhhh punguza bei kdg.
 
Hapo sijakuelewa, Unaongelea bei au ubora kwa bidhaa? kwani kama ubora ni mzuri hizo bei ni za kawaida, ukitaka bidhaa bora na bei yake itakua juu.
Bei hizo haziendani na thamani ya bidhaa.
 
Hawa Wana target market yao kabisa(high income earners),watu wanaofanya conspiques (prestige) purchase

Yaani self concept (manunuzi) yao ina reflect personality yao

Wanatumia psychological pricing (cost of production should not necessarily reflect the price list) ,kwakua watu Wana associate high price na high quality kwahiyo bei zao zinatumika Kama indicator ya quality
 
niliomba nafasi ya kufanyia biashara stendi mpya ya mabus mbezi Luis, baada ya majibu kutoka nikatumiwa pdf ya majina, wakati natafuta jina langu nikakutana mule ndani Kuna watu wanalipa hadi milion 20 kwa mwezi
Na mimi nahitaji hii pdf. Napataje?
 
Wananunua watu a.k.a binadamu.

Kuna watu ndani wanaweka masofa ya laki 5 ila nenda pale GSM Mall Kuna masofa ya milion 15 mpaka 30.

Narudia tena Kama huna hela sio wote
siku nilipojua mm ni maskini wa kutupa, nilikua nyumbani kwa eng. mmoja hv pale moro..mke wake akawa analalamika kochi lao limeanza kuchoka (wakati mm naliona liko poa tu) mzee akasema "fulan si alisema analeta kontena lake huku kwa nini asinitupie kasofa hapo ndani"

akampigia simu akamuagiza amnunulie sofa aliweke kwenye hiyo kontena.... kwa hela za tsh ilikua linagarimu kama mil 9 hv
yaan kaagiza sofa uingereza ndani ya mda mfupi tu kwa sh mil 9... na upuuzi

shubaamit
 
Angalieni series ya Breaking Bad.. ukiona sehemu watu wanauza vitu bei extra ordinary kuna kam three possibilities

1. They are cleaning money
2. They might be involving in illegal business parallel to the business you are seeing.

So wanatumia hiyo room ya kuuza kwa bei kubwa kama means ya kutakatisha pesa.

Kwa mfano kama begi umeona linauzwa 750,000 ina maana mtu anaweza kuuza mabegi hewa 10 kwa siku na hapo inakuwa imemsaidia kutakatisha kama 7.5 million.

Anyway, but hiyo ni opinion yangu..
Umesema 3 possibilities ila umeelezea mbili tuu..
 
Hapo Posta mimi mwezi uliopita nilikuwa nasimamia ndoa ya jamaaangu flani tukaingia kwenye duka moja hivi ili nichukue shati jeupe, kuuliza bei naambiwa 110,000 alafu halina maajabu, nikatoka bila kujibu chochote nilipofika nje ndio nikaangua kicheko.
 
Back
Top Bottom