G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Katika historia ambayo nilijikuta nakasirika baada ya kuisoma basi ni ya Kinjekitile Ngwale na vita yake ya majimaji mwaka 1905 hadi 1907. Ni historia inayochefua mno ukiisoma. Na kwakweli sijui hata ni kwanini inafundishwa kwenye mitaala.
Tunaambiwa kuwa Kinjekitile aliwaambia watu wake endapo risasi zikifyatuliwa na wajerumani basi waseme "maji" na risasi ile papo hapo itageuka kuwa maji hivyo hawatadhurika nazo. Watu wake wakamuamini wakaingia vitani kwa miaka miwili huku wakiteketea.
Leo miaka takribani zaidi ya mia moja tunashuhudia kiongozi wetu wa kitaifa akituambia kuwa tukimtanguliza Mungu mbele na kuendelea na mishe zetu basi hatutadhurika na COVID 19. Matokeo yake ni vifo vya kuogofya vinavyofululiza ambavyo hata hatujui vinakotoka.
Ajabu anao wafuasi wake wanamtetea mchana kweupeee eti kiongozi wetu yupo sawa! Hapana! Tunampotosha na kuzidi kujidanganya wenyewe! Wapo wanaosema eti anasifiwa mpaka kimataifa! Wapi?
Yani kwa haya wanayofanya baadhi yetu tena tukiwa peke yetu inadhihirisha kuwa watanzania wameongezeka uwezo wa kufikiri kwa ratio ndogo sana huku wengi wetu wakiwa hawana tofauti yoyote kifikra na wale wakazi wa kusini wa mwaka1905. Ni aibu kubwa kwetu.
Emb tujitafakari, the tupo mahali sahihi kwa haya tunayofanya? Yanakubalika kijamii? Nini hasa kinaisumbua jamii yetu?