Kwa anayemfahamu Hassan Mpambije, tajiri wa Sengerema tuwasiliane

EdwardC8

Senior Member
Nov 2, 2017
181
257
Kwema wandugu?

Hassan Mpambije, tajiri wa Sengerema, aliyewahi kuwa na biashara ya gari za Cruiser kutoka Kamanga hadi Sengerema, na ana maduka kadhaa ya nguo pamoja na Mpambije Complex iliyoko pale Sengerema mjini ni Baba yangu mdogo niliyepotezana nae miaka 7 sasa.

Sina mawasiliano yoyote upande wa ndugu wa baba baada ya kwenda nje masomoni na nimerudi hivi majuzi nimefikia Dar. Natamani kwenda Sengerema Mwanza nikatembee kidogo, lakini ni lazima niwe nae in-touch kwanza kwasababu sifahamu mtu kule.

Naomba kama unamfahamu, unijulishe pa kuanzia kumtafutia au unisiadie namba yake. Karibu PM
 
Kwanini usiende direct sengerema ,ukawaulizie wakazi wenyeji wa kule kuliko kuulizia humu
 
We safiri mpaka Sengerema utampata.ungekua nje ya nchi sawa lakini upo hapa hapa nchini,hata ukifika tu Mwanza mjini nenda pale Kamanga ferry hutakosa magari ya kule yenye kubeba abilia watakusaidia kupata namba yake

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Vipi nikikuta ameshahama? yaani niende mahali bila taarifa sahihi?!!
Kwa uwekezaji huo alionao kuhama ni vigumu na kama kahama hapo ndipo utakapopata clue,wenyeji wapo watakupa story vizuri na mambo mengine watakueleza,miaka 7 mliopotezana mbona ni michache sana
 
hata kama amehama kwani hana ndugu , watoto ambao ni ndugu zako pia.Utakaribishwa.Humu JF hutapata msaada sana kwa issue yako.Naoona bado unafikiri kizungu KARIBU TANZANIA Utakayemkuta huyo huyo atakupokea na ugali utasongwa utakula.Au unataka ukakae kwa Tajiri tu huyo mjomba wako? Au tumia RADIO FREE AFRICA huwa wanakipindi cha KUTAFUTANA Wasukuma wanakipenda sana kinaitwa CHAT LINE!!
 
Huyu jamaa namfahamu ila sina namba yake.
Nimeishi Sengerema miezi 2.
Kweli ni tajiri wa pale.
Nenda tu utawakuta hata ndugu wengine.
 
Ulitaka tujue kwamba una ba mdogo ambaye ni mambo safi; na wewe ulikuwa ulaya masomoni ndo umendondoka majuzi juzi - haya tumekusoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom