kwa anayemfahamu CHARLES MIANO mkuu wa kituo cha polisi himo

Master jay

Senior Member
May 28, 2012
194
29
ni baba yangu, ni mtoto wake wa nje, aliponipa jina la JOSEPH alihamishwa kikazi (alikuwa mkuu wa kituo cha polisi HIMO mwishon mwa mwaka 1979). Ila nasikia alihamishiwa TAZARA. Baadae ndo haitambuliki alirudi kijijin au la. Kwa kifup alikuwa amemwoa mama flan wa kimachame na mpaka wakati nazaliwa alikuwa anawatoto wa 4 wa kike. Hivyo simjui sura ya baba wala hao dada zangu wa kimachame. Ni msukuma ila sijui ni shinyanga au mwanza au tabora. Kupotezana na baba kunaweza kuwa ni makosa ya wazaz kama wao ila sitak kuyaingilia. Wana jf kama kuna mwenye details yoyote mwenye tetes naomba uwasiliane nam kwa cm no 0715288927
 
Pole sana Mkuu!

Hapa ni JF! Kuna kila aina ya raia humu!
Nategemea utapata majibu mazuri!
 
Kwa ushauri tu nenda wizara ya mambo ya ndani kuna details zote za askari polisi hata waliostaafu utaelezwa walipo
 
Kwa ushauri tu nenda wizara ya mambo ya ndani kuna details zote za askari polisi hata waliostaafu utaelezwa walipo

nimeshakwenda huko, ni njoo kesho, subir kutwa nzima. Mara hailioneka, utashughulikiwa ukiwa tayar tutakufahamisha kwa simu, yaan kuanzia 2007 nimesubir mpaka leo sijapokea sim ya wizara ya mambo ya ndan.
 
Kwa ushauri tu nenda wizara ya mambo ya ndani kuna details zote za askari polisi hata waliostaafu utaelezwa walipo

kaka unamtesa bure... akifika kule watamyayusha tu na kuomba chai ya maziwa tena hasa wakijua sababu ya kumtaftia

kesi ya nguruwe ukimpa ngiri ni balaa
 
nimeshakwenda huko, ni njoo kesho, subir kutwa nzima. Mara hailioneka, utashughulikiwa ukiwa tayar tutakufahamisha kwa simu, yaan kuanzia 2007 nimesubir mpaka leo sijapokea sim ya wizara ya mambo ya ndan.
Ngoja nimwasiliane na jamaa yangu wa kitengo cha Intelijensia, nitaku-PM nikipata majibu........................
Lakini nina wasiwasi na kumbukumbu za Polisi kwa miaka hiyo ya 1979, sidhani kama zinaweza kupatikana, hasa ukizingatia kwamba alihamishiwa TAZARA...............!
 
Kuna kipindi fulani cha RFA sikijui jina but huwa pia kinahusika na hzi mambo za kumtafuta mliyepotezana..
Kwa kesi yako nadhani unaweza kukitumia kipindi hicho pia kwa kuwatafuta hata mashangazi au ndugu za babaako wengine..
Ninao mfano wa mtoto wa dadaangu ambaye pia aliwahi kukitumia kipindi na kufanikiwa kuwapta baadhi ya ndugu upande wa babaake..
 
DINGI yangu kafanya kazi TAZARA miaka 31 mpaka akastaaf. Alikuwa huko toka 1983 hadi alipostaaf 2005. Nikuulizie?
 
Kama huyu jamaa angetangaza kwamba ni tajiri mkubwa hapa nchini na anamiliki viwanda kadhaa pamoja na majengo makubwa huko Masaki jijini Dar na Njiro jijini Arusha, lakini hamjui baba yake ila tu aliwahi kusimuliwa kwamba baba yake anaitwa CHARLES MIANO, hakika saa hizi wangeshajitokeza wana ukoo wa the so called MIANO haraka sana wakiwepo hata wale wa undugu wa kuunganisha kwa gundi............... chezea utajiri wewe.....................!
 
Mi nashauri angetumia hiyo janja..Kama alivyosema Mtambuzi. Ninauhakika angewapata tu dada zake na hata baba yake..maana wabongo wanapenda kujipendekeza kwa mtu mwenye fweza.
 
Mi nashauri angetumia hiyo janja..Kama alivyosema Mtambuzi. Ninauhakika angewapata tu dada zake na hata baba yake..maana wabongo wanapenda kujipendekeza kwa mtu mwenye fweza.
Nakumbuka kuna mtoto alichukuliwa kutoka katika nyumba za kulea watoto yatima na mzungu na kwenda naye Ughaibuni, alirudi nchni akiwa na huyo mzungu aliyemlea akiwa na umri wa miaka kama sikosei 20 hivi akijaribu kumtafuta mama yake au wazazi wake..... alivyoonekana kwenye TV usiku, mpaka inafika asubuhi walikuwa wamejitokeza mama zake kama kumi hivi na mashangazi kibao.............
It works, namshauri abadilishe jukwaa kisha atumie mbinu hii.........................
 
Du pole Master Jay km Mama Mzazi bado yupo hawezi kukusaidia hata kijiji alichotokea huyo askari? ukaanzia na ukoo wao.
Ila bado nina imani na pale Wizarani usichoke uende na TAZARA mwisho kabisa km sio RFA tangaza gazetini unamtafuta huyo Cherles Miano atapatikana tu
 
Back
Top Bottom