Kwa anayejua kireno/kibrazil njoo utoe shule

Nahitaji kukifahamu hiki kilugha ntakupataje unifundishe
Uko wapi? Hii lugha kiasi fulani ina ugumu wake na ugumu unakuja kwa sababu kila sekta inajikita kwenye ujinsia na jinsia hizo utazijua utapojifunza na sikufuata mkumbo na kwenye unyambuaji WA vitendo ni mgumu kiasi na zaidi kwenye irregular verbs, huona jamaa humu wanaandika tu lakini muda mwengine inakuwa ngumu kufuata grammar tujifunzeni kwa sababu mimi mwenyewe najifundisha na nakosea Lakin nakuwa mwepesi WA kujua kosa langu.

Ukishajikubalisha kwa vitendo zaidi utafannikiwa hakuna ugumu kwenye jitihada yoyote.

Mfano ukichukua kitendo FALAR hiki kinakuwa na ubadilikaji kutokana na viwakilishi vyake. Na vitendo mara nyingi huishia na:-
AR mfano falar(kuongea).

ER beber (kunywa).

IR. abrir (kufungua).

Mfano WA hicho kitendo FALAR(KUONGEA) hii ni regular verb ukinyambua kutokana na viwakilishi vyake halisi utapata.

EU (mimi)= FALO = naongea.

ELE/ELA (yeye me/ke)= FALA = anaongea.

VOCÊ (wewe)= FALA= unaongea. kiwakilishi hiki kinakuwa na sifa ya unyambulishaji WA ele/ela.

TU (wewe) =FALAS = unaongea.

NÓS(sisi)= FALAMOS = tunaongea.

ELES/ELAS(wao me/ke)= FALAM =wanaongea.

VOCÊS (nyinyi)= FALAM = mnaongea. Hii pia kwenye unyambuaji inabeba ya eles/elas.

VÓS (nyinyi)= FALAIS = mnaongea.

Kwa upande WA irregular verb utapata hivi kwenye mnambuliko wake

Kitendo PÔR(por) ikazie mdomo kidogo kwa hicho kichoro juu na jina lake inaitwa O circunflexo (KUINGIZA/KUWEKA).

EU PONHO(PONYU)= mimi naingiza.

ELE/ELA PÕE = wewe unaingiza. isemee puani unapoitamka. Na hii O inaitwa O acento til.

TU PÕES (poesh) = wewe unaingiza. Itamkie puani.

VOCÊ PÕE= wewe unaingiza.

ELES/ELAS PÕEM = wao wanaingiza. itamkie puani na M usiifumbie mdomo.

VOCÊS PÕEM = nyinyi mnaingiza.

NÓS POMOS(pomosh) = sisi tunaingiza.

VÓS PONDES (pondesh) = nyinyi mnaingiza

Kwenye mabano unatamka neno kwa kufuata kama nilivyoeleza hapo.

Utaona maneno yaliobeba vialama(acentos) kwenye vowels na jina la kila alama hiyo inaitwa:

`a - hii inaitwa a acentuado Grave.
ã - hii inaitwa a acentuado Til.
â - hii inaitwa a acentuado circunflexo.
á - hii inaitwa a acentuado agudo.

Na nyengine ni hivyo hivyo kulingana na irabu na utaipa jina hilo.
Hayo ni machache tu.

Ikiwa kuna makoseo naomba marekebisho kwa wale wanaojua.

Uliza.

Tenha um bom dia.
 
Uko wapi? Hii lugha kiasi fulani ina ugumu wake na ugumu unakuja kwa sababu kila sekta inajikita kwenye ujinsia na jinsia hizo utazijua utapojifunza na sikufuata mkumbo na kwenye unyambuaji WA vitendo ni mgumu kiasi na zaidi kwenye irregular verbs, huona jamaa humu wanaandika tu lakini muda mwengine inakuwa ngumu kufuata grammar tujifunzeni kwa sababu mimi mwenyewe najifundisha na nakosea Lakin nakuwa mwepesi WA kujua kosa langu.

Ukishajikubalisha kwa vitendo zaidi utafannikiwa hakuna ugumu kwenye jitihada yoyote.

Mfano ukichukua kitendo FALAR hiki kinakuwa na ubadilikaji kutokana na viwakilishi vyake. Na vitendo mara nyingi huishia na:-
AR mfano falar(kuongea).

ER beber (kunywa).

IR. abrir (kufungua).

Mfano WA hicho kitendo FALAR(KUONGEA) hii ni regular verb ukinyambua kutokana na viwakilishi vyake halisi utapata.

EU (mimi)= FALO = naongea.

ELE/ELA (yeye me/ke)= FALA = anaongea.

VOCÊ (wewe)= FALA= unaongea. kiwakilishi hiki kinakuwa na sifa ya unyambulishaji WA ele/ela.

TU (wewe) =FALAS = unaongea.

NÓS(sisi)= FALAMOS = tunaongea.

ELES/ELAS(wao me/ke)= FALAM =wanaongea.

VOCÊS (nyinyi)= FALAM = mnaongea. Hii pia kwenye unyambuaji inabeba ya eles/elas.

VÓS (nyinyi)= FALAIS = mnaongea.

Kwa upande WA irregular verb utapata hivi kwenye mnambuliko wake

Kitendo PÔR(por) ikazie mdomo kidogo kwa hicho kichoro juu na jina lake inaitwa O circunflexo (KUINGIZA/KUWEKA).

EU PONHO(PONYU)= naingiza.

ELE/ELA PÕE isemee puani kwa hiyo O
Hayo ni machache tu.

Ikiwa kuna makoseo naomba marekebisho kwa wale wanaojua.

Uliza.

Tenha um bom dia.
Niko dar kama utojali nipatie namba yako tuongee kabisa whatsap
 
Oí, tudo bom os meus amigos quem estão aqui? Ao lado de me estou bem graças a deus!

Quando vi estas informações gostei muito bem. Parabéns.

Sent using Jamii Forums mobile app
peraberns amigo.

mkuu najua napitia michango yako najifunza kabisa.
maana nilikuwa nategeshea niwqpate wadau kama nyie nianze kuiva.
ninasikiliza nyimbo na lylics tu natamani sasa niweze kuonhea japo sentensi kadhaa.

ngoja nisome kwanza kisha nitaendelea kukuhoji.
mfumo wako wa kuelekeza uko bomba sana.

Deus te abencoe -- Mungu akubariki
 
Back
Top Bottom