itagata
JF-Expert Member
- Sep 4, 2011
- 210
- 71
Nimekua natumia gari aina ya Pajero kwa Muda sasa na imejitokeza likapata matatizo ya Injini yake (4D56), nimejaribu kununua injini zimefika 3 mpaka sasa lakini zote zinasumbua baada ya miezi miwili au mitatu toka kuzifunga. Imefika kipindi sasa nimekata tamaa nafikiria kuweka injini aina nyingne tu, lakn kuna mdau mmoja kaniambia kuwa kuna injini kama hizo (4D56) za kichina zinakuwa mpya kabisa zinauzwa kwa bei ya chini ambazo naamini naweza kudumu nayo hata kwa miaka 3 hivi. Hivyo basi naomba kama mtu anataarifa sehemu zinakopatikana hizo injini anijuze ili nifanye mchakato wa kuzitafuta. Asanteni.