Kwa amani ya nchi hii, tume mnao mchango mkubwa, msituangushe

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,822
35,817
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Kama ilivyo kwa polisi na mahakama. Tume ya uchaguzi mnayo nafasi kubwa sana katika kuhakikisha kutotetereka kwa amani ya nchi hii.

Hii ikiwa ni kwa kuhakikisha tu kuwa haki inatendeka. Yaani kwa kutekeleza tu ulio wajibu wenu.

Haihitaji akili za ziada kumtambua nani ni mshari, fedhuli, jahiri, bazazi, mwenye kututakia vurugu, nk, katika harakati za uchaguzi huu ulioko usoni.

Busara iliyotumika hadi sasa kuepusha mengi na ikaendelee kutamalaki. Ikibidi kuhamasisha maridhiano baina ya vyama.

Chama kimoja kinalazimisha vipi kupendwa kwa kuhujumu vingine huku kikitumia vyombo vya dola kufanikisha hayo?

Mambo haya ya kuhujumiana baina ya vyama ni ya kukemewa. Tume mnayo nafasi kubwa tu ya kutuondolea upuuzi huu ili haki ionekane kuwa inatendeka.

Si haki kwa chama kimoja kutumia dola kwa makusudi ili kuwaengua wengine kimzengwe mzengwe nia ikiwa wabakie wao tu kwa kile wanacho kiita kupita bila kupingwa!

IMG_20200820_093436_378.jpg


Tume tutendeeni haki japo sisi tulio wapiga kura tu, kwa nyie kutokuwa sehemu katika ghiliba hizi zisizokuwa na ustaarabu.

Fomu zenye kuvitaka vyama kuzingatia maadili ya uchaguzi zina nini kama ghiliba na ufedhuli huu unaendelea hivi?

Tume fanyeni kazi yenu kwa uadilifu mkawarejeshe wagombea wote walioenguliwa kwa agenda zozote zile za siri. Tokea kwa majaliwa, kabudi, aboud, na hata kwa nape. Na mkaturejeshee wagombea wote walioenguliwa kimzengwe mzengwe. Yasiangaliwe makunyanzi ya mtu katika hili.

Macho na masikio yetu yapo kwenu.

Mnayo nafasi ya kututendea haki. Hebu msisahau kuwa historia pia itakuwapo macho kuchukua mkondo wake.

Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu

Eeh mola wetu ukazisikie dua zetu.
 
NEC inapaswa kupitia majimbo yote yenye utata na kuhakikisha haki inatendeka la sivyo hali itakuwa ngumu.
 
NEC ni ya hovyo kabisa

Mkuu maumivu yako si tofauti na ya wengi wetu.

Kazi ya tume huru ni kuwawezesha (to facilitate) wagombea siyo kuendekeza janja janja, ghiliba, dhuluma na yote ya namna hiyo tokea kokote.

Ni vyema tume wakajitathmini kabla hawaja pwelewa. Dunia inakwenda kwa kasi mno.
 
Mkuu maumivu yako si tofauti na ya wengi wetu.

Kazi ya tume huru ni kuwawezesha (to facilitate) wagombea siyo kuendekeza janja janja, ghiliba, dhuluma na yote ya namna hiyo tokea kokote.

Ni vyema tume wakajitathmini kabla hawaja pwelewa. Dunia inakwenda kwa kasi mno.
Mechi ya Simba na Yanga mwamuzi ni Dr Msola unategemea nini kwa Simba?
 
Tume tungali kusikia kauli yenu kuhusu hii engua engua ya wagombea.

Kuna mtu anakotaka kutupeleka siko.

Kuna shari inatafutwa. Nachelea kuiona njiani ikitujia kwa kasi sana.

Kwa hakika pana watakaowajibika kwa yote.
 
Back
Top Bottom