Kwa aliyetumia dawa ya netragen (ya vidonda vya tumbo) ya herboworx corporation limited je umepona?

Je ulifanya kipimo gani kuhakiki ni vidonda vya tumbo?

Kipimo pekee kinachiweza kuthibitisha kikamilifu (confirmatory test) ni Upper GI Endoscopy, yani unawekewa camera kupitia mdomoni kuangalia njia ya chakula ikoje na kuona hivyo vidonda vipoje, vipo wapi na vimefikia hatua gani. Vyengine vyote si confirmatory tests. Je ulifanya hivi?

Wengi wanadhani wana vidonda vya tumbo kumbe magonjwa mengineyo kama Pancreatitis, Inflammatory bowel diseases, Esophagitis, Mallory Weiss Syndrome na mamia ya magonjwa mengine hata Cancer ya Mfuko wa chakula (Gastric Carcinoma).

Onana na daktari, fanya vipimo stahiki kisha tumia dawa kwa umakini, ukiona bado rudi kwa daktari wako.
Mkuu umeongea na kushauri kitu cha msingi sana, watu wengi sana wanaanza kutafuta nakutumia madawa ovyo , kutokana na kuona dalili zinazofanana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo bila kupima kipimo kikubwa, inashangaza sana, hata hosp mgonjwa anapoeleza shida zake madaktar hukimbilia kupima damu na choo asipokuta kitu anasema haumwi chochote, mgonjwa anarudi nyumbani akiwa na shida ileile, hali hiyo huwapelekea kuanza kutumia madawa ovyo bila matokeo chanya na kusingizia vidonda haviponi.
 
Je ulifanya kipimo gani kuhakiki ni vidonda vya tumbo?

Kipimo pekee kinachiweza kuthibitisha kikamilifu (confirmatory test) ni Upper GI Endoscopy, yani unawekewa camera kupitia mdomoni kuangalia njia ya chakula ikoje na kuona hivyo vidonda vipoje, vipo wapi na vimefikia hatua gani. Vyengine vyote si confirmatory tests. Je ulifanya hivi?

Wengi wanadhani wana vidonda vya tumbo kumbe magonjwa mengineyo kama Pancreatitis, Inflammatory bowel diseases, Esophagitis, Mallory Weiss Syndrome na mamia ya magonjwa mengine hata Cancer ya Mfuko wa chakula (Gastric Carcinoma).

Onana na daktari, fanya vipimo stahiki kisha tumia dawa kwa umakini, ukiona bado rudi kwa daktari wako.
When MD speaks
 
Back
Top Bottom