Kwa aliyepta daraja la tatu kwa alama ya 13 hstry E, geo E na kiswhil C vip anawez kupta chuo kikuu

Kuna watu wanampotosha huyu ndugu, tena nakuomba kama huja apply mkopo acha kabisa usiliwe hiyo hela ya application fee. Iko hivi kwa matokeo hayo HUPATI chuo..

Unatapaswa kuwa na D mbili ambazo ndizo principal pass. Chuo HUPATI ndugu angalia mishe zingine
 
Hupati yani pamoja na kufikisha cut points ya 4.0 bado unakosa sifa za principal pass mbili ambazo ni DD yani hata uwe na AEE huendi chuo kwa sababu una cut points lkn principal pass hazijatimia
Mbona mambo hakaeleweki wengine CES unapata na wengine hupati nani anamajibu sahihi tuache kuhangaika hivyo
 
Watoto hebu mkasome huko! Jamiiforums inashuka hadhi kumbe mitoto imejaa humu!
 
Mkuu sema umekosa point ya kuzungumza kama vipi wewe lala tu kuliko kuniita mtoto wakati nina kijiti tena cha science si ajabu ww ulikosa hata two na art yako maana watu wa science sio wagumu kuelewa kama wewe
Mimi nilishamaliza shule nyakati za mkoloni wakati huo wewe ukiwa maji maji yaliyochanganyika na hewa kwenye kiuno cha baba yako!

I was the best student. Got the best education EVER.

Kwenye hizi shule zenu za kata za siku hizi kwanza huwa mnasoma nini ninyi watoto?

Maxence Melo hebu angalia utaratibu wa kufanya screening utuondolee watoto humu!
 
Habari wakuu Nina ndugu yangu alisoma enzi hizo FTC in mechanical engineering DIT walikuwa wana fanya Mitihani ya Necta masomo sita Kati ya hayo masomo alipata D masomo matano na C Somo mmoja kwa walio soma FTC minimum inter qualification ya kusoma degree ni C flat masomo yote sita.Kaisha fanya kazi miaka mingi hivyo ana uzoefu wa kutosha kwenye field yake ana hitaji kusoma degree ya mechanical engineering kwa kujilipia mwenyewe chuo ana weza kupata ?naombeni uzoefu wenu kwenye hili.
 
Ili uweze kudahiliwa katika chuo chochote kile kikuu TANZANIA lazima uwe na minimum points of 4 katika masomo yako mawili kwa kozi ambazo ni NON-HEALTH RELATED.


Mfano; HKL ,ili uwe na sifa za kwenda chuo kikuu lazima uwe umepata atleast D D katika masomo yako,hii inamanisha kwamba ili uwe na sifa za kwenda chuo kikuu kwa kiwango cha chini lazima uwe umepata A E,B E,C E LAKINI D E HUTAKUWA NA SIFA.


(NOTE:HUWA WANAANGALIA MASOMO MAWILI TU,AMBAYO YATAKUPA MINIMUM TOTAL OF 4 PTS.)

kozi za afya lazima uwe na minimum points of 6 katika masomo yako yote matatu yanayobeba combination yako.

Mfano, PCB lazima uwe na C D E ambapo C lazima iwe ya chemistry,D ya biology na E ya physics (NI LAZIMA) kwa point hiyo kama umepata div 2 pts 12 PCB na umepata D D D(hauna sifa ,kwa sababu lazima uwe na C ya chemistry)


Angalizo, tunapenda kukuhakikisha kuwa ushauri wa kozi tulizokupa ,zitakufanya upate mkopo kwani 98% ni kipaumbele cha serikali.


KAMA UMESOMA PCB HII INAKUHUSU
Najua na ninatambua kwamba ndoto kubwa ya wanafunzi waliosoma PCB huwa ni kusomea udaktari chuo kikuu.lakini ndoto zao wengi hupotea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo matokeo mabaya,kuchagua vyuo kimakosa n.k.


Kwa mwaka huu wa masomo ili uwe na sifa ya kusomea udaktari chuo kikuu chochote kile TANZANIA lazima uwe umesoma PCB na umepata

Physics-D,Chemistry-C,Biology-C which gives a minimum points of 8;Hii inamaana kwamba mwisho kusomea udaktari mwaka huu lazima uwe umefaulu kiwango cha DIV 2 PTS 10.


Kama umesoma PCB na haujapata vigezo hapo juu tafadhali ninakuomba usisumbuke kuomba udaktari kwani huwezi chaguliwa.


Kama umepata Div 2 pts 11 hadi Div 3 pts 13 ,kuna kozi nyingi za kuomba tofauti na udaktari,kama nilivyoziorodhesha hapo chini-
Bsc. Pharmacy (lazima uwe na C ya chemistry,D in
biology na E in phys)

Bsc. Nursing (lazima uwe na C ya chemistry,D in biology
na E in phys,Nutrition or mathematics)

Bsc. Medical laboratory science (lazima uwe na C ya
chemistry,D in biology na E in phys)
Bachelor of Science in Optometry((lazima uwe na E ya
chemistry/mathematics,D in biology na C in phys)

Bachelor of Sciences in Health Laboratory
and
Bachelor of Science in Physiotherapy((lazima uwe na C ya chemistry,D in biology na E in phys)

Bachelor of Medical Laboratory Sciences in Clinical Chemistry,

Bachelor of Medical Laboratory Sciences in Hematology and Blood Transfusion,

Bachelor of Medical Laboratory Sciences in Histotechnology,

Bachelor of Medical Laboratory Science in Microbiology and Immunology,

Bachelor of Medical Laboratory Sciences in Parasitology and Medical Entomology and

Bachelor of Medical Laboratory Sciences General
((Kozi 7 hapo juu lazima uwe na C ya chemistry,D in biology na E in phys)

Bachelor of Science in Environmental Health Sciences (BSc EHS) (lazima uwe na C ya chemistry,D in biology na E in phys/Nutrition,mathematics or agriculture,geography)


Kozi zifuatazo lazima uwe na minimum of 4 pts
Bsc. Microbiology
Bsc. Molecular biology & Biotechnology
Bsc. Biotechnology & Laboratory science
Bsc. Food science & Technology
Bsc. Agronomy
Bsc. Animal science & production
Bsc. Wildlife management
Bsc. Veterinary medicine
Bsc. Forestry
Bsc. Agricultural general
Bsc. With Education


KAMA UMESOMA CBG
- Wanafunzi wanaosomea CBG a level wengi wao huwa na ndoto za kusomea nursing,pharmacy na kozi mbalimbali za afya,lakini kwa mwaka huu mambo yamekuwa tofauti sana,wanafunzi walioma CBG wataruhusiwa kusoma kozi moja tu ya afya ambayo ni Bachelor of Science in Environmental Health Sciences (BSc EHS) (ambayo lazima uwe na C ya chemistry,D in biology na E in phys/Nutrition,mathematics or agriculture,geography).


MUHIMU
- Ninakuomba kama hauna sifa ya kusomea kozi ya afya hapo juu tafadhali usiombe kwani itakugharimu baadae kwa kukosa chuo.

- Kozi nyingine ni kama zilivyoainishwa katika wanafunzi waliosoma PCB.


KAMA UMESOMA PCM /PGM
All field of Engineering hasa
Civil Eng,
Mechanical Eng,
Electronics & Telecommunications Eng,
Electrical Eng,Computer Eng,
Agricultural Eng, Irrigation & Water resource Eng,
architecture, Quantity Survey, Geomatics,
Actuarialscience, Computer science, ICT,
Chemical & Processing Eng
Industrial engineering
Petroleum geology, petroleum engineering, petroleum chemistry
Geology,
Engineering geology
Bsc. With Education


KAMA UMESOMA EGM,ECA NA HGE
Bsc. Agricultural economics & Agribusiness
Bsc. Building Econmics
Bsc. Actuarialscience
Bsc. Irrigation & Water res Eng, Agricultural Eng (O level Science)
Bsc. Architecture
Bsc. Geomatics
B. A Economics & Statistics
Bsc. Computer science , Bsc ICT
B.A land management & Valuation
B. A Economics
B. A Accounting & Finance
Bsc. With Education
Procurement
statistics


KAMA UMESOMEA HGL, HGK & HKL

LL. B (B. Law)
B. Land management & Valuation
B. A Human resource management


All course relate with community development & Planning

B. A with Education
B.LAW ENFORCEMENT UDSM


KAMA UMESOMEA CBN ,CBA
- CBN wamepata bahati kwani wao wameruhusiwa kusoma kozi mbili za afya ambazo ni nursing na environment health ambapo inawabidi wawe ni minimum points of 6 in three subjects.Kati ya hayo masomo lazima uwe na C in chemistry,D in biology na E in nutrition.

- Kwa upande wa CBA yeye ameruhusiwa kusoma kozi ya environmental health.

- Kozi nyinginezo ni kama nilivyoainisha hapo juu katika sehemu ya CBG.



MWISHO
Napenda kumalizia kwa kuwakumbusha wanafunzi wote mnaotaka kufanya maombi ya vyuo vikuu mwaka huu kwamba application zote zinafanyika chuo husika unachotaka kusoma, maana yake maombi yote itakubidi uyatumie katika chuo unachotaka kusomea.
Mkuu umekosea ni chuo gani Tanzania kinachukua pharmacy ambayo ina chini ya point 8???? ili uwende pharmacy lazima uwe na Div 2 ya 10....
 
Back
Top Bottom