Kwa aliewahi kuiskia stori ya Ondiek John, Mwenye nguvu kama Samson

Gaddy Fazzy

Member
Jan 16, 2021
54
125
Mimi natokea mkoa wa mara (rorya) nilkuwa naskia sana habari za kuwahi kuwepo Jamaa mwenye nguvu sana kama samsoni (biblia).

Nikajaribu kufuatlia zaidi kisa chake kwa wazee tofauti tofauti lakini story ikawa ndo ile ile inafanana!! Inasemekana jamaa alikuwa miraba minne, mkono wake tuu kama paja la malaya, ngumi yake akiikunja na kukutupia hapo hapo unapoteza maisha!. Aliwasumbua sana wahindi ,maana alkuwa anaingia kwenye maduka yao na kuchukua bidhaa kwa nguvu na walimuacha hawakuwa na cha kufanya.

Inasemekana siku moja alikuwa anakwenda kijiji jirani sasa ikabid ipite njia ya shortcut ,mbele kidogo akakutana na wakulima fulani wapo shambani wanalima wakamwambia arudi asiipite hiyo njia kwan mbele kidigo kuna chui ambae hujerui watu wapitapo njia hiyo. Jamaa akawaambia "huyo chui hanifanyi chochote" kisha akasonga mbele, huku nyuma wale watu wakaanza kumfuatilia kimya kimya ili washuhudie kitakacho tokea.

Basi bwana, Ondiek John akatembea mpaka akafika kwenye mto ile anavuka tuu chui huyu hapa(chui alkuw na watoto maeneo hayo) , akamrukia Ondiek ili amjeruhi lakini wapi ,Ondiek akamdaka yule Chui na kumsukumia Konde la nguvu kichwani hadi Chui akapasuka na kufa palepale.

Wale raia hawakuamini maana walijua Ondiek atauawa, ndipo wakarudi na kuwasilimulia watu kisa chote. Lakini Tatizo la Ondiek John alikuw mtukutu sana, hakupenda kuoa yaan alkuw anakamata mwanamke yeyote na kulala nae iwe kwa nguvu au la,awe mke wa mtu au la. Ukichukuliwa mkeo na ukaleta kibesi konde la maana linakuhusu. Basi bwana ikatokea wakoloni wa kiingereza wakazipata hizi habar, jamaa aliwachachafya sana, lakin mwishoni walifaulu kumkamata na kumpeleka ulaya kwenye mapambano!.

Inasemekana huko nako aligawa dozi sana, baadae wakamrudisha tena huku Mara ila walikuwa tayari washamkata mishipa na hakuwa na nguvu tena.

Akawepo tuu bila mtoto wala mke hatimae alifariki bila kuacha uzao wowte. Huenda watoto wake au wajukuu na vitukuu wangekuwepo yupo ambaye angerithi. Katika jamii zetu kuna stori nyingi sana zilizowahi kutokea ila hazikuandikwa maana wazungu siku zote hawapendi kuonyesha kuwa mwafrika yupo juu(inferior).

Wanaandika vitu ambavyo vinaonyesha "Superiority" yao tuu .

Haya ndo niliyobahatika kuyapata kama yupo anaejua hii stori ya huyu jamaa "ONDIEK JOHN" namkaribisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom