Kwa alichokifanya huyu Traffic Police, anastahili Pongezi

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,891
2,367
Jana nilikuwa natokea kwenye mihangaiko yangu ya kutafuta ugali, ilikuwa ni nyakati za jioni hivyo nikasogea kituo cha daladala na kusubiri Usafiri( Najua mtanishangaa member wa JF kupanda daladala maana humu wengi wenu mnamiliki Ford Ranger na wachache wanamiliki Prado)

Sasa ikaja daladala nikaingia na kuanza safari mbele kidogo kama mita 20 hivi kwa nyuma ikatokea Toyota Hilux ya Police ikiwa imewasha zile taa za juu za blue na nyekundu (sijui maitaje wenyewe)

Ile gari ya police ikaja mpaka ubavuni mwa daladala na kumwambia dereva aweke gari pembeni.

Kisha zikasimama zote, kama kawaida, dereva wa daladala akashuka kwenda "kumalizana" na yule traffic police.

Sisi abiria tukiwa hatujui kinachoendelea mara ghafla tunaona yule traffic ameshuka kwenye gari anakuja huku anamfokea dereva kwa kutaka kumpa rushwa na matokeo yake ile hela aliyopewa na dereva akaitupa upande wa pili wa barabara kisha akavua na kofia yake.

Then akatoa sijui camera au nini akapiga picha ile gari akampa maelezo dereva then akaenda kupanda gari yake na kugeuza na kurudi alipotoka.

Hicho kitendo ni cha dakika chache kilijaza watu na pia ilimfanya dereva kama kufadhaika fulani.

Hii inaonesha madereva waache kuishi kwa mazoea, sio kila mtu anaendekeza rushwa za kijinga.
 
Hakufika bei tu.

Kama Yesu Kristo aliuzwa kwa vipande 30 vya pesa na myahudi Yuda Eskariote sembuse huyo konsitebo au sajenti wa polisi

Hakuna polisi asiyekura rushwa, hakuna.

Wapo wasiopekea rushwa bhana acha kudhalilisha watu.
 
Hakufika bei tu.

Kama Yesu Kristo aliuzwa kwa vipande 30 vya pesa na myahudi Yuda Eskariote sembuse huyo konsitebo au sajenti wa polisi

Hakuna polisi asiyekura rushwa, hakuna.
Kila mtu na utaratibu wake aliojiwekea katika kazi mkuu. Nakumbuka kuna mwaka fulani niliuwa nasafiri natoka Dar kwenda Moro na basi fulani hivi (sitaji jina msije kusema naipigia promo) ila humo ndaini nid abiria na dereva tu haina konda.

Sasa kufika Vigwaza kuna jamaa alipungia ili apande, dereva akasimamisha akamuuliza wapi unaenda jamaa akajibu Moro. AKaruhusiwa kupanda akakaa pale kwenye mfuniko wa injini pemebeni ya dereva.

Jamaa akatoa pesa na kumpa dereva, lakini dereva akakataa akamwambia utalipia mbele. Sasa sijui yule mtu hakuelewa au vipi akawa analazimisha, mwisho wa siku dereva akamjibu "usiniharibie kazi nimekuambia utalipa mbele"

Kufika chalinze akapanda wakala wa ahyp mabasi na dereva akamwambia yule wakala huyu nimemchukua Vigwaza. Jamaa akalipa nauli kwa wakala kisha wakala akashuka tukaendelea na safari.

Lakini kampuni hiyo hoyo ina madereva ambao uchukua abiria na kuwaweka pale kwenye mfuniko wa injini kisha wanakusanya nauli kutoka kwa hao abiria na kuzitia mfukoni.

Point yangu ni kuwa kila mtu ana utaratibu wake na insi anavyofanya kazi zake.
 
Tuambie kwanza dereva alifanya kosa gani au gari alikua na makosa gani kabla ya kuanza kutupa mkasa wa rushwa.
Sijui huko walipotoka inaonekana jamaa alifanya kosa huko alipotoka na ile gari ilikua inamfuatilia maana baada ya kupiga picha akageuza na kurudi alipotoka. Lakini hata kama kile kitendo cha kumfuata police kule kwenye gari wangeweza kumalizana kule kule sio mpaka kuja kutupa pesa barabarani huku watu wanatazama.Na toka hapo dereva alikuwa kafadhaika sana tofauti na alivyokuwa kabla ya hilo tukio.
 
Ilikuwa bei gani kwani iliyotupwa chini?inawezekana hakufika kiasi kilichokuwa kinatakiwa
 
Gari zina camera hizo ,pili huyo inspector angemjibuje hela yenyewe ilikua 4000,utaatibu kazi kwa 4000
 
Gari zina camera hizo ,pili huyo inspector angemjibuje hela yenyewe ilikua 4000,utaatibu kazi kwa 4000
Sikutaja mwaka mkuu
Wakati huo hizi gari za kichina hazijaingia bado. Na nilikuwa nasafiri mara kwa mara tu Dar to Moro madereva wengine wanabeba abiria kama kawaida na ela wanatia mfukoni na inspector yupo pembeni.
 
Ninahisi huyo 'Dereva' wa hilo 'DalaDala' atakuwa alitoa tu 'Rushwa' ya Tsh 2,500/= Shenzi Taimu zake, ila angetoa Tsh 10,000/= angeshukuriwa.
 
Back
Top Bottom