Kwa akina Baba tu wenye watoto................

Msiri

Member
Jan 10, 2010
97
83
Jamani, kutokana na ushuhuda mwingi ambayo nimesikia toka kwa watumishi wa Mungu, nawashauri akina baba wenye watoto wafanye DNA test za watoto wao, hasa kama watoto kama hawafanani kabisa na baba yao, ila wanasingiziwa kufanana na babu wa babu au bibi wa bibi etc.

Nimegundua kuwa kuwa akina baba wengi wanalea watoto wasio wao kutokana na kuwaamini sana wake zao, na baadhi yao (akina mama) baada ya kumjua Mungu wanashindwa waanzie wapi kuwafahamisha waume zao. Unaweza kufanya test tu hata bila ya kumwambia mama yao. Mtoto ana haki ya kumjua baba yake wa damu.
 
hizo ni heresay tu kaka. ukitaka kufa haraka, anza hako kamchezo
 
Ukishamjua what next! Mie naona yaliyopita bora kuyaacha yaende km yalivyo ni kujipanga kwa yanayokuja. Hivi mtoto ana 15 yrs ukampime DNA kisa ushuhuda. Huyo ni vyema kumuona mwanao tu na kujipanga na wadogo zake.
 
Zamani, kuzaliana ilikuwa ni kawaida tu, na kulikuwa na amani sana. Nawafahamu watu kibao ambao wamekulia kwa mzee fulani, kumbe masikini si watoto wa mzee husika!
Ukianzisha huo mchezo hapa kwetu, utangulize kwanza nafasi za magereza na makaburi, maana watu watachinjana sana!
 
Msiri, vipi kuhusu wewe mwenyewe, umeshathibitisha kwamba huyo unayemtambua kama baba ni baba yako kweli? Au wewe huna haki ya kumjua baba yako wa damu?

Annina
 
Duh kwa ninavyompenda mwanangu halafu nikaambiwe sio wangu ntafia huko huko DNA room. Acha tu niendelee kuamini ni wangu
 
nashauri kama maisha ni shwari nyumbani hakuna haja ya DNA. That should be considered only and only if unaona kuna conspirancy kati ya mtoto na Mama. Otherwise hakuna sababu ya kutafuta ugonjwa wa moyo.
 
Zamani, kuzaliana ilikuwa ni kawaida tu, na kulikuwa na amani sana. Nawafahamu watu kibao ambao wamekulia kwa mzee fulani, kumbe masikini si watoto wa mzee husika!
Ukianzisha huo mchezo hapa kwetu, utangulize kwanza nafasi za magereza na makaburi, maana watu watachinjana sana!

Mkuu Nadhani suala la DNA ni la mtu binafsi, either kwa makubaliano na mwenza au hata yeye mwenyewe kama anahisi kawa dume Bwegge!!!

ila hilo la mambo ya zamani liko tricky kidogo maana kila jambo lina wakati wake, kumbuka pia zamani kupiga nje haikuwa issue, lakini siku hizi jaribu kupiga nje uone... hata madereva teksi wa durban watajua yule jamaa anacheat mkewe!!!

Cha maana hapa ni kimoja tu, to live with the outcome, sio unampima mtoto DNA halafu akiwa sio wako basi unalialia kwa wakwe.... Kabla ya kupima, dawa ni kujiandaa kwa kila kitu na kuwa tayari ama sivyo, usipime!!!
 
Hizi ni unnesesari presha hazijatulia.....umeambiwa wako; amini wako tu....
 
Ni jukumu letu kulea watoto wote walio kwisha zaliwa. Muda utumike kuhamasisha familia zenye uwezo wa ''adopting'' na ''fostering'' kufanya hivyo. ukipita kwenye orphanages zetu nyingi utaona umuhimu wa jambo hili. Na mifano ya watu waliotunzwa na wazazi wa kufikia ni mingi tu!
 
Jamani, kutokana na ushuhuda mwingi ambayo nimesikia toka kwa watumishi wa Mungu, nawashauri akina baba wenye watoto wafanye DNA test za watoto wao, hasa kama watoto kama hawafanani kabisa na baba yao, ila wanasingiziwa kufanana na babu wa babu au bibi wa bibi etc.

Nimegundua kuwa kuwa akina baba wengi wanalea watoto wasio wao kutokana na kuwaamini sana wake zao, na baadhi yao (akina mama) baada ya kumjua Mungu wanashindwa waanzie wapi kuwafahamisha waume zao. Unaweza kufanya test tu hata bila ya kumwambia mama yao. Mtoto ana haki ya kumjua baba yake wa damu.

Please leave me alone.They are my kids....mama yao kaniambia hivyo and that is it.Period.
 
Ni jukumu letu kulea watoto wote walio kwisha zaliwa. Muda utumike kuhamasisha familia zenye uwezo wa ''adopting'' na ''fostering'' kufanya hivyo. ukipita kwenye orphanages zetu nyingi utaona umuhimu wa jambo hili. Na mifano ya watu waliotunzwa na wazazi wa kufikia ni mingi tu!

Thanks Daktari, lakini tunaomba mchango wako kuhusu kama kufanya DNA kuna tija au la... maana naona umeelemea zaidi kwenye malezi ya foster children, which is a little bit off-topic
 
hata kama si mtoto wako wa kweli si atakuwa kapitia kila kitu through wewe kama huyo mtoto wa kweli kasoro mbegu tu? tafuta wa pili kama una wasi wasi sana lakini kama uko powa chukulia kama ume-adopt tu ndio maisha hayo.
 
AW, haya yote ni sababu ya male "ego" hakuna chochote... hata wanaoenda kufumania utawakuta mioyo inaenda mbio kama mota ya feni!!!!!!!!!
 
nashauri kama maisha ni shwari nyumbani hakuna haja ya DNA. That should be considered only and only if unaona kuna conspirancy kati ya mtoto na Mama. Otherwise hakuna sababu ya kutafuta ugonjwa wa moyo.

Sawa mzee usijitafutie pressure bure we amini tu kuwa ni wako labda mama akutamkie
 
Ukishamjua what next! Mie naona yaliyopita bora kuyaacha yaende km yalivyo ni kujipanga kwa yanayokuja. Hivi mtoto ana 15 yrs ukampime DNA kisa ushuhuda. Huyo ni vyema kumuona mwanao tu na kujipanga na wadogo zake.

Seconded mia kwa Mia. Kama wewe si Biological father basi ni Legal father na inaruhusiwa/ inakubalika. Uwe na amani, Mtunze mtoto wako maana umeisha wekeza sana kwake tangu siku ya kuzaliwa hadi umri alionao; na yeye pia anakutambua kama baba tangu apate fahamu na hamujui baba mwingine. Kwa nini unataka kumvurugia mwanao maisha. Ebu fikiria unwe wewe leo umri wa Miaka 30 au 40 unaambiwa kuwa huyo unayemuita baba si baba yako bali baba yako ni fulani na ambaye aliuzini mama yako wakati akiwa kwenye ndoa ya huyo baba. Utajisikia je siku hiyo? Nasema hivi kama Mama alijichanganya hiyo imekula kwake. Haki ya Mtoto kumjua baba naamini ubaba unaokusudiwa si ule wa kutundika mimba na kujificha; naamini ni ule wa kuwajibika kulea na kumtunza mtoto. Huo ndio UBABA. Hayo mengine ni hadithi. By the way hizo DNA test nazo haziaminiki. Angalia Sinema ya Shades of Sin inayoendelea ITV utaona jinsi results zinavyoweza kuhujumiwa na iwapo ikakutokea unaweza ukakosa raha maishani mwako. Ya nini ufe mapema bwana! Kisa ... eti mtoto!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom