Kwa akili zetu ilibidi tupitie haya ili tujifunze na tujue hadata

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Wengine tulipoamua kumuunga mkono Lowassa kupitia UKAWA baadhi ya watu hawakutuelewa na waliona ni bora Magufuli alie ndani ya CCM kuliko Lowassa alie ndani ya UKAWA.

Wengi walishindwa kuona mbali na kugundua kuwa adui mkubwa wa nchi hi si Lowassa bali ni CCM na mfuno wake na wakasahau kuwa hakuna chama kinachoweza kubadilika ghafla na kuthamini wananchi bila kwanza kupoteza dola kisha kikaa pembeni kikajitathimi na kujirekebisha kabla ya kutaka kurudi madarakani.

Wengi walishindwa kuelewa ni bora mara mia moja Lowassa ndani ya UKAWA kuliko Magufuli ndani ya CCM.

Chama tawala, tena kilichokaa madarakani muda mrefu, hakiwezi kuijrekebisha mpaka kwanza kishindwe katika uchaguzi ndio kitaheshimu wapiga kura tofauti na hapo ni kujidanganya tu.

UKAWA,wanaotaka kujitengenezea jina na kukubalika kwa wananchi na kujitofautisha na CCM,kamwe wasingefanya haya iwapo wangekuwa madarakani leo hii:

1.Wanafunzi wa vyuo vikuu wangesoma bure(serikali ingewalipia) na leo hii kungekuwa hakuna kilio cha watu kukosa mikopo.

Serikali ya UKAWA chini ya Lowassa isingesitisha ajira bali ingejikita katika kuongeza ajira na fursa za watu kujiajiri

Serikali ya Lowassa chini ya UKAWA isingeongeza makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilimia 8 mpaka kufikia asilimia 15.

Serikali ya UKAWA chini ya Lowassa isinge handle issue ya tetemoko kule Kagera kwa style hii ya serikali ya CCM.

Lowassa asingesema serikali yake haina shamba na angefika kuwafariji wafiwa mapema sana(nafikiri alikwenda kuwafariji)

UKAWA waliokuwa wanapinga wanafunzi kukosa mikopo,kamwe wasingesitisha ufadhili wa serikali wa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi.

UKAWA waliokuwa wanapinga mishahara duni ya watumishi wa umma,wasingeacha kuboresha mishahara ya watumishi wa umma kwa kuanza na kuongeza kima cha chini.

Lowassa alieitwa fisadi asingetaka kujichafua kwa kujenga uwanja wa ndege wa kimtaifa huko Monduli


Lowassa alietwa fisadi,asingekubali kuendelea na utaratibu wa mikataba ya siri kama tunavyoona sasa bali angetaka kuonyesha ni mtu tofauti na alikuwa anasingiziwa na mikataba yote ingekuwa inapita Bungeni.

Lowassa aliechafuliwa na mkataba wa Richmond serikali yake isingeacha kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma katika kutangaza tender mbali mbali za serikali.

Serikali ya UKAWA iliyokuwa ikililia uhuru wa vyombo vya habari kamwe isingethubutu kufuta utaratibu wa kurusha live vikao vya Bunge.

Serikali ya UKAWA kamwe isingeweza kuja na sheria zisizo rafiki kwa vyombo vya habari na baadhi ya sheria ama zingekuwa zimefutwa kabisa au kufanyiwa marekebisho mfano ile ya magazeti ya mwaka 76.

Lowassa kama Raisi lakini asie mwenyekiti wa chama Taifa,kamwe asingeweza kuwa anafanya maamuzi bila kwanza kushirikisha wenzake.

Loswassa asingukuwa na nguvu ndani ya serikali na kwenye chama kwani asingekuwa na kofia mbili.

Leo hii tungekuwa tuna-enjoy freedom of speech na zaidi tungekuwa tuna -enjoy busara na uvumilivu wa mzee Lowassa katika ku-deal na wale ambao wangekuwa wapinzani wake.

Hizo ni baadhi ya fursa tulizopoteza kwa kuchagua chama kile kile kwa kukariri na kilichokuwepo madarakani kwa miaka mingi kiasi kwamba kimepoteza hofu ya kutoheshimu na kujali wapiga kura.

Majuto ni mjukuu!

Ni wakati wa sisi sasa ku-behave kama binadamu na sio watu(watu kwa maana ya kuwa kama viumbe wengine ambao hawakujaliwa akili,maarifa na utashi).
 
:D:D:D unataka kusema tungekuwa nchi ya kwanza africa wanafunzi kusoma bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu???????? :D:D:D aisee
kwa uchumi huu huu tunaozidiwa na hata Kenya tu.
 
tz}ccm.gif

"Kidumu chama cha mapinduzi"
 
Ili tuamini unayoyazungumza, mwambie mzee apande daladala za Gongo la Mboto to Chanika maana kero za dqladala hazijaisha. Hapo nitaamini nusu ya kile unachozungumza.
 
Back
Top Bottom