Kwa akili ya kawaida, itawezekana nchi za Ulaya Magharibu na Marekani kuiruhusu Russia kuikalia Ukraine au kuweka kibaraka wake?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Nitakuwa wa mwishi kuamini hili litatokea kwa usalama wa nchi za NATO na Marekani maana kufanya hivyo, ni kuweka usalama wa nchi hizo rehani jambo ambalo kamwe hawatalikubali na ndio maana wanalazimika kumsaidia Ukraine wazi wazi hivi sasa.

Hii vita inaweza kuchukua muda mrefu kinyume na matarajio ya Russia walioamini nchi za NATO zingeogopa kuingilia hii vita(waliamini wangepigana na Ukraine tu tena kwa muda mfupi) na kuna hatari huko mbeleni Russia kuingia vitani na mojawapo ya nchi za NATO na automatically kuingia vitani na NATO.

Wakiingia vitani na NATO, basi tutarajie matokeo haya:

1.Vita kusimama na wakaingia makubaliano mapya yatayomaliza vita kwa mashariti yatayoilazimisha Russia kuondoa majeshi yake Ukraine na Ukraine kutojiunga NATO.

2. Vita kuwa kubwa na kuwa chanzo cha WW3( sio rahisa sana ila inaweza kutokea).

3. Matumizi ya nuclear ili kumaliza kabisa vita na kufunika aibu ya kushindwa kwa ataekaanza kuona vita imemshinda na hapa zaidi atakuwa Russia.

Russia hawezi kukubali aibu ya kushindwa kama ambavyo Marekani na washirika wake wanaoisaidia wazi wazi Ukraine hawatokubali kushindwa na matokeo yake ni vita kuchukua muda mrefu mpaka mojawapo ya hayo mambo matatu yatapotokea ili vitaa iishe au iwe ni vita ya dunia nzima kama sio vita ya kupigana nuclear.

NB:
Vitendo vya Russia kama kuztisha nchi za NATO na Marekani, kusitisha uuzaji wa gesi kwa nchi baadhi ya nchi za Ulaya, na kuzilazimisha kununua gesi yao kwa kutumia sarafu yao, kunazifanya nchi za Ulaya na Marekani kuona umuhimu wa kumshughulikia Putin kuliko ilivyokuwa wakati vitaa inaanza na hata kabla ya vita yenyewe kuanza.

Muda utathibitisha.
 
... ila ifahamike sio Russia pekee mwenye nyuklia. Akijaribu kuitumia ajiandae for the consequences.
Ni wazi Russia hawezi kupigana na nchi za NATO akazishinda, hivyo anaweza kutumia silaha za nyuklia au sila zingine zilizopigwa marufuku katika kutafuta ushindi au kuficha aibu ya kushindwa na hapa nyuklia ndio itahusika zaidi.
 
Putin anatumia nyuklia kutishia watu ili wamuogope atimize uovu wake lakini wameshamshtukia kwani kuna nchi tisa zenye silaha za nyuklia duniani na sio Russia peke yake na vita vya nyuklia havina mshindi.

Putin atapigwa tu bila kujali cha nyuklia wala cha Hypersonic Missiles na Putin yuko kwenye hatari kubwa kwani akilazimisha watumie nyuklia "he will run the risk of stopping an assassin's bullet."
 
Nitakuwa wa mwishi kuamini hili litatokea kwa usalama wa nchi za NATO na Marekani maana kufanya hivyo, ni kuweka usalama wa nchi hizo rehani jambo ambalo kamwe hawatalikubali na ndio maana wanalazimika kumsaidia Ukraine wazi wazi hivi sasa.

Hii vita inaweza kuchukua muda mrefu kinyume na matarajio ya Russia walioamini nchi za NATO zingeogopa kuingilia hii vita(waliamini wangepigana na Ukraine tu tena kwa muda mfupi) na kuna hatari huko mbeleni Russia kuingia vitani na mojawapo ya nchi za NATO na automatically kuingia vitani na NATO.

Wakiingia vitani na NATO, basi tutarajie matokeo haya:

1.Vita kusimama na wakaingia makubaliano mapya yatayomaliza vita kwa mashariti yatayoilazimisha Russia kuondoa majeshi yake Ukraine na Ukraine kutojiunga NATO.

2. Vita kuwa kubwa na kuwa chanzo cha WW3( sio rahisa sana ila inaweza kutokea).

3. Matumizi ya nuclear ili kumaliza kabisa vita na kufunika aibu ya kushindwa kwa ataekaanza kuona vita imemshinda na hapa zaidi atakuwa Russia.

Russia hawezi kukubali aibu ya kushindwa kama ambavyo Marekani na washirika wake wanaoisaidia wazi wazi Ukraine hawatokubali kushindwa na matokeo yake ni vita kuchukua muda mrefu mpaka mojawapo ya hayo mambo matatu yatapotokea ili vitaa iishe au iwe ni vita ya dunia nzima kama sio vita ya kupigana nuclear.

NB:
Vitendo vya Russia kama kuztisha nchi za NATO na Marekani, kusitisha uuzaji wa gesi kwa nchi baadhi ya nchi za Ulaya, na kuzilazimisha kununua gesi yao kwa kutumia sarafu yao, kunazifanya nchi za Ulaya na Marekani kuona umuhimu wa kumshughulikia Putin kuliko ilivyokuwa wakati vitaa inaanza na hata kabla ya vita yenyewe kuanza.

Muda utathibitisha.
Leo umeandika fact kabisa kuliko ushabiki ulokuwa nao hapo awali.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom