Kwa akili hii ya TANROAD na watawala wetu sioni foleni zikisha Dar

Nimesema Juu pale kama huna ufahamu na jambo bora utulie ndugu.. Kila nchi ina design standard zake.. na hata contractor aje wa nchi gani hatakiwi kuvunja hizo standards zinavyohitaji.. Kwa Tanzania Barabara ya Lami design standard yake ni miaka 20, na barabara ya Kiwango cha Zege (Rig Pavement) ni Miaka 50.. na kwa utaalamu wangu wote hakuna pahala duniani wanaweka barabara kwa design standard ya miaka 1000, Hakuna!
unaandika wewe harafu aibu naona mimi
 
Hii Hii mada siyo yako ww. Una jifanya mjuaji huku ni Zero.
Nyie ndio mtufikisha hapa na tu degree twenu twa kukariri notes. Design mnachora kwa Penseli tu.
Aisee.. binafsi nashukuru umeanza kuelewa.. kwa kiasi flani upopoma utapungua!
 
Ring road zenyewe zinajazwa matutaa! Zamani nilikuwa natumia dk 15 kutoka Kinyerezi mpaka Mbezi Louis kabla bara bara haijawekwa lami, lakini tangu iwekwe lami, sasa hivi natumia zaidi ya nusu saaa... Yale matuta ukiruka utavunja chasis ya gari ndani ya miezi sita.
Kuna siku wamama wawili wakajichanganya kuomba lift pale Kinyerezi eti wanaelekea Malamba mawili... Walijuta kupanda ile gari... Maana nadhani ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kupanda gari ya kwenye "Rally'...

Mkuu wangu unajaribu kutuongopea watu wazima mara matuta mara gari ya rally kumbe hata ringroad hauifahamu! Uwe unasikilizia kidogo ujifunze kwa wanaofahamu mkuu
 
Mkuu wangu unajaribu kutuongopea watu wazima mara matuta mara gari ya rally kumbe hata ringroad hauifahamu! Uwe unasikilizia kidogo ujifunze kwa wanaofahamu mkuu

A ring road is a road or a series of connected roads encircling a town, city, or country.

1564428462801.png

1564428522040.png
 
Mkuu hata kwa wenzetu,nenda Washington, nenda New York, nenda Chicago huduma muhimu zipo down town,ila ukishatoka down town,kwa mfano Kwa Dar useme ukishafika pale Jangwani ukutane na highway ya ukweli ambayo hakuna Zebra crossings, hakuna magari yanayokatiza barabara na barabara zote zinazoingia atleast zina lane yake angalau ya kilometa moja.Bahati mbaya barabara zetu zinajengwa kiccm ccm na kwa standard wanazojua ccm pekee
... umenikumbusha zebra crossings! Kuna ujinga fulani umefanyika hivi karibu hususan kwenye round-abouts yaani pande zote 4 ni zebra-crossings! Zimesababisha foleni ya ajabu sana on top of the existed! Kwa mfano, mzunguko wa pale Kigogo Dar ni balaa tupu siku hizi; ukienda mbele baada ya mzunguko kuelekea Kigogo kwenyewe kila baada ya hatua 20 ni zebra crossings!

Ni jambo la kawaida sana siku hizi foleni ya Kawawa Road kuanzia Magomeni Mataa kwa yanayoelekea Ilala na yanayoelekea Magomeni foleni huanzia Ilala. Kwa yanatokea Tabata foleni huanzia Tabata Dampo simply kutokana na Mzunguko wa Kigogo! Anyway, ndio ubunifu wa wataalamu wetu huo!
 
Foleni kuisha Dar bado sana. Kwa kutumia uzoefu wangu wa kutembea nje zilizoendelea naweza kusema bila wasiwasi kuwa foleni Dar itaendelea kuwa tatizo mpaka hapo hatua nzuri zaidi zitakapochukuliwa.
1. Kuwe na ring roads na Flyovers za kutosha
2. Vyombo vya kubebea abiria viwe vikubwa (kama tunashindwa kuweka trams, trains na metro basi angalau tutumie mabasi makubwa kama ya ya zamani ya Ikarus
3. Vijengwe vituo vizuri na packings nzuri na madereva wavitumie
3. Kuwe na ratiba inayoeleweka na mabasi yaziheshimu
5. Madeveva waheshimu sheria za barabarani (hili ni muhimu sana kwani linachangia zaidi ya asilimia 50 ya foleni)
Vipi kuhusu vivuko vya watu kupita juu au chini,maana hili janga inaonekana kama vile si tatizo wakati linachangia kwa kiwango kikubwa kusababisha foleni...
 
... umenikumbusha zebra crossings! Kuna ujinga fulani umefanyika hivi karibu hususan kwenye round-abouts yaani pande zote 4 ni zebra-crossings! Zimesababisha foleni ya ajabu sana on top of the existed! Kwa mfano, mzunguko wa pale Kigogo Dar ni balaa tupu siku hizi; ukienda mbele baada ya mzunguko kuelekea Kigogo kwenyewe kila baada ya hatua 20 ni zebra crossings!

Ni jambo la kawaida sana siku hizi foleni ya Kawawa Road kuanzia Magomeni Mataa kwa yanayoelekea Ilala na yanayoelekea Magomeni foleni huanzia Ilala. Kwa yanatokea Tabata foleni huanzia Tabata Dampo simply kutokana na Mzunguko wa Kigogo! Anyway, ndio ubunifu wa wataalamu wetu huo!
Hahahahah na TRA wa sasa hawachezi mbali,usiposimama tu na bahati mbaya kuwe na mtu alikuwa anazisogelea hizo zebra basi 30,000 lazima ikutoke au utoe rushwa ya 10,000
 
waseme tu ukweli tujue maana kila siku wanainanga ccm sasa hawatuambii mbadala wa ccm ni chama gani tuchague ..

Ufipa hawana hoja iliyoonyooka na uchaguzi ndiyo huooo
Mkuu unataka kuambiwa mbadala,mimi nilidhani miaka 55 inatosha kukuambia kwamba unafaa kuendelea na ccm au la au ni faida gani au hasara utapata au utakosa kwa kuachana na ccm,na kama ni hasara au faida tumeshapata au kama ni kudumaa tumesha dumaa kwa hiyo kuwe na mbadala au tusiwe na mbadala sioni kama watanzania wanalakupoteza.Ila hoja yako inaonesha kuwa unaona upuuzi wa ccm ila unahangaika nao au kuvumilia Mateso yao kwa kisingizio kwamba huoni mbadala na huo ndo upumbavu wenyewe unaosemwa Kule Lumumba
 
Back
Top Bottom