Kwa akili hii ya Prof. Sospeter Muhongo, nadhani yeye sasa ndiyo wa kujengewa sanamu upesi sana

Ukimtukana mwana Mkoa wa Mara ( Musoma ) Mwenzangu jua umetutukana wana Mara ( Musoma ) kwani huo 'Ujiniasi' wake Profesa Muhongo ndiyo upo Kwetu wana Mara ( Musoma ) wote. Kuwa makini sana na hujachelewa kutuomba Radhi Mimi GENTAMYCINE nikiwa Mwakilishi wao wa Kutukuka hapa JamiiForums sawa?
Bora hata Mkono amefanya kazi inayoonekana. Huyu mtu amefanya nini cha maana zaidi ya kuwauliza wenzake kama wanajua hesabu?
 
Hakika Mara bado ina vichwa vinavyotoa madini. Yaani mtu unatoa wazo la kutumia milioni 420 kutengeneza DUBWASHA lenye sura ya mtu badala ya kutengeeza kitu kitakachoacha kumbukumbu na manufaa kwa jamii?
Ambalo halina hata faida yoyote.
 
Bora hata Mkono amefanya kazi inayoonekana. Huyu mtu amefanya nini cha maana zaidi ya kuwauliza wenzake kama wanajua hesabu?
Acha Uwongo na Chuki zako Kubwa kwa Profesa Muhongo sawa? Bahati nzuri Yeye ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Mzee wangu Mkono alikuwa wa Kwetu Butiama ila kwa sasa Profesa Muhongo amefanya Maendeleo makubwa mno huko Jimboni Kwake ambayo Mnafiki na Hasidi Wewe huyajui na hujayaona pia.
 
Simchukii wala sisemi uongo. Akili zake zinawafaa watu wa jimbo lake. Na wanafunzi wake. Sisi kwenye public anaona tunafaa kufuga kuku tu anatusaidia nini?
Ukiona anapambania jambo ujue amekuwa dalali. Kuna wanaomtuma.
Nakubaliana naye hatuhitaji sanamu. Ila yeye pia hatuhitaji kama mnataka sanamu mjenge huko huko jimboni
 
Mwendazake tumesha mjengea kaburi lake .

Katutia hasara sana kama nchi ndani ya muda mfupi aliohudumu kama Kiranja Mkuu.

Ameua BIASHARA, sekta BINAFSI iliathirika sana, shughuli zote za kufanya WATU BINAFSI aliwapa SUMA JKT, Hadi tenda za kusafisha barabara.

SUMA JKT wana hadi boti za uvuvi ili tu kuua nguvu wafanyabiashara.

Alinunua mindege mingi isiyo na faida.

Alijenga ukuta kwa gharama kubwa na hauna faida yoyote, WATU wanabeba mawe vilevile.

Kila kitu alitaka kipelekwe kwao kwa gharama za serikali.

Tenda zote za kujenga vivuko aliipa kampuni yake.

Hee! Yako mengi Sana aiseee
Mama anapiga pasi za kijerumani
 
Vyote vifanyike, sanamu lake na shule na hata Zahanati kwa jina lake vijengwe

Kwanza huyo liprofesel lilikuwa jizi tu, lilinyimwa fursa ya upigaji kwenye madini na gas, siliamini, usikute linaongea hayo, kumbe ndani limebeba chuki za kijinga

Mwambieni na yeye ajenge heshima yake tutamuenzi aache upigaji, kwani ukiwa msomi lazima uwe jizi?
Jikite kwenye hoja ewe mjane
 
Pumbafuuuuuuuuuuuuuuuu, Mwendazake Zurumati ndio Ulimwona Mungu wako. Ikijengwa Hiyo Sanamu Itapigwa Mawe na Viboko Kama Vyote, Hadi Basi.
 
Profesa atulize akili asipaniki, JPM atafanyiwa mengi ya kumkumbuka kama yeye mwenyewe alivyofanya mengi makubwa ya kukumbukwa

Sanamu itajengwa na Taasisi zinakuja na mengine mengi yatafanyika. Tukae kwa utulivu
Kwa hiyo ni bora watu wafe ili sanamu lijengwe kuliko pangejengwa kwanza kituo cha afya chenye jina lake then sanamu likajengwa baadae? Kumjengea jizi sanamu ni sanamu nyingine tena
 
Vyote vifanyike, sanamu lake na shule na hata Zahanati kwa jina lake vijengwe

Kwanza huyo liprofesel lilikuwa jizi tu, lilinyimwa fursa ya upigaji kwenye madini na gas, siliamini, usikute linaongea hayo, kumbe ndani limebeba chuki za kijinga

Mwambieni na yeye ajenge heshima yake tutamuenzi aache upigaji, kwani ukiwa msomi lazima uwe jizi?
Wapumbavu kama wewe mtafutika tu taratiibu
 
Siamini sana Kama ujenzi wa Sanamu ni ishara tosha ya kumkumbuka hayati, Bali ingejengwa shule au taasisi ya kurahisisha Huduma za kijamii ikaitwa jina la anayetaka kukumbukwa na si sanamu “ Professor Sospeter Muhongo.

Chanzo: Tanzania Abroad TV

Kama kuna Profesa ambaye nina uhakika Uprofesa wake ni wa Kustahili kabisa kutokana na Uwezo wake mkubwa wa Akili ( IQ ) hapa Tanzania basi ni 'Poti' wangu wa Kutukuka Sospeter Muhongo.

Profesa kamaliza kila Kitu na GENTAMYCINE siongezi chochote kwani tayari 'Wakosoaji' mbalimbali jana kule Mkoani Morogoro katubatiza Jina na kutuita Watu wa 'Chokochoko' na tusioitakia mema Tanzania yetu huku akisahau kuwa hata Mtangulizi wake nae 'alitudharau' na 'kututisha' hivi hivi ila kaondoka na 'Team Chokochoko' bado tunaendelea Kudunda tu na hata Corona nayo inatuogopa vile vile Kudadadeki.
Genta..hawa watu hurejesha akili zao wakishakosa au kunyimwa madaraka...namkumbuka Muhongo yule waziri alikuwa arrongant na mawazo kama ya Kabudi tu...naona sasa akili zimerudi...ni kama zilivyorudi za jaji Werema!
 
Kwa hiyo ni bora watu wafe ili sanamu lijengwe kuliko pangejengwa kwanza kituo cha afya chenye jina lake then sanamu likajengwa baadae? Kumjengea jizi sanamu ni sanamu nyingine tena
futa O andika zilo 😛
 
Kwa hiyo ni bora watu wafe ili sanamu lijengwe kuliko pangejengwa kwanza kituo cha afya chenye jina lake then sanamu likajengwa baadae? Kumjengea jizi sanamu ni sanamu nyingine tena

MKANDAHARI buana😃😃😃 Kwani umeambiwa hivyo vituo vya afya havijaanza kujengwa?
Vyote vinavyowezekana vitafanya. Vumilia tuu
 
Back
Top Bottom