Kwa ajali za Mv Bukoba, Mv Spice, Mv Skagit; Serikali ya CCM inajali maisha ya watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa ajali za Mv Bukoba, Mv Spice, Mv Skagit; Serikali ya CCM inajali maisha ya watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jiwe Linaloishi, Jul 21, 2012.

 1. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi yanapotokea majanga serikali imekuwa ikiunda tume na kutoa ahadi kibao za kukomesha majanga hayo yanayotafuna maisha ya waTZ kila kukicha, lakini cha kustaajabisha ni kwamba majanga haya yameendelea kujirudia mara kwa mara kama haya ya kuzama kwa meli, milipuko ya mabomu, ajali za Treni na barabarani, Je serikali ya ccm bado wanataka tuendelee kuamini kwamba wanajali maisha ya watanzania?? mbona wao hawatumii hivyo vyombo vya usafiri na kukaa maeneo hayo majanga yanatokea kama kweli wana nia ya kupunguza vifo vya waTZ? Serikali ya ccm kwa miaka 50 iliyokaa madarakani wanajua fika kwamba hatutakiwi kuwa hapa na matatizo haya tunayokumbana nayo leo hii kama si uzembe, unafiki,udhaifu,tamaa na ujinga wa viongozi, wafike mahali wakubali kuwajibika kabla nguvu ya uma haijawalazimisha kwani itakuwa ni aibu kwao.
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  hoja lege lege
   
 3. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sikatai mawazo yako ila kwa wanaojali uhai wa binadamu sidhani kama wanafanya masihara kama serikali dhaifu ya ccm kila siku hadithi wakati watu wanaangamia kwa uzembe.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kuna utafauti MV. BUKOBA ilijengwa MPYA haikuwa VIPORO kama hizo zingine... MV. BUKOBA ni wakati kwa JK. Nyerere

  Alikuwa hanunui VIOZO kwa Wananchi wake; Tatizo lake labda utasema ni Ulafi wa Wafanyakazi sababu ya

  Kutelekezwa na Wizara... MISHAHARA MIDOGO, MALAZI MABOVU, MOTISHA NDOGO... wakawa wanategemea kuwa

  through MV. BUKOBA kujaza watu na mizigo ili wajineemeshe na familia zao

  * KWA MV. SPIES na MV SKAGIT - from binning aim yao ilikuwa ni SUPER PROFIT na SIO KUWAJALI WANANCHI

  WAKANUNUA VIOTA VILIVYOOZA; YAANI HIZO MELI ZILIWEKWA HADI KWENYE E_BAY na hakuna aliyenunua

  Mpaka Msheni ya kulazimisha MV.SKAGIT walizeka mbili kwenye E_BAY kila moja kwa $ 600,000 wakashusha $ 400,000

  lakini hakuna Mnunuzi.

  Mpaka vibepari Uchwara vikajitokeza vikapewa hizo Mbili kwa $ 400,000 -- Na kula watu.

  Lakini waliambia Hali ya Hewa Mbaya Baharini lakini hawakujali, walijali pesa ya siku sio watu

  **** KWAHIYO HIZO AJALI NI TOFAUTI KABISA KIMANTIKI
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Waziri muhusika kadai hawezi kujiuzuru kwakuwa yeye sio Mungu angeweza kuzuia upepo ulioangusha meli...So kadai ni mapenzi ya Mungu!!
   
 6. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mi nailaumu serikali kwasabu ya kutokuchukua hatua kwa wahusika pindi tatizo linapotokea. kama waliambiwa hali ya hewa ni mbaya kwanini mamlaka zinazohusika ziliruhusu meli kuondoka? kuna mamlaka za kufanya ukaguzi wa chombo kabla ya kuondoka je kama hizi meli zilizama sababu kubwa ukiwa ni kuzidisha uzito hao wakaguzi mbona hatujasikia wamechukuliwa hatua? tukiendelea kulindana bila kuwajibishana tutegemee majanga zaidi..
   
Loading...