Kwa aina ya Wachambuzi tulionao tunawahitaji kina Haji Manara wengi

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
4,288
8,281
Naanza kwa kusema 'BIG UP' kwa Manara kwa kueleza waziwazi bila woga kitendo kibaya mno kilichofanywa na Yanga, kukimbia mechi bila kujali umati ule uliojazana pale kwa kivuli cha kanuni.

La pili ambalo nalo linastahili pongezi ni kuonesha uzandiki kwa wanaojiita Wachambuzi...kwa kutetea na kuubeba utopolo uliofanywa na utopolo yenyewe 'Eti wamefanya kitendo cha kishujaa’.

Hawa utopolo hawana pa kuchoropoka mwaka huu, naziona game mbili clear zinakuja, ya FA na hii ya VPL ambayo itapangiwa tarehe nyingine. Lazima vyura wapigwe.

Wachambuzi uchwara wamekuwa wengi mno....! Tatizo la ajira linakuja na matokeo anuai, wengine wanavamia fani.
 
Naanza kwa Kusema 'BIG UP' Kwa Manara.Kwa Kueleza Waziwazi bila Woga Kitendo kibaya Mno Kilichofanywa na Yanga,Kukimbia Mechi Ya Darby bila kujali Umati Ule uliojazana Pale Kwa Kivuli cha Kanuni...
unaandika ki shabiki sana, unaanza na utabiri kuhusu hizo game 2,Yani hueleweki,unabwata hapa lakini wakina kapombe ndio wanao wajua yanga pale kwenye pitch.wewe kata mauno hapa jf
 
Sasa hivi wanazua eti ni kwa vile yanga wana jakamoyo ns TFF! Hivi hawa yanga ni x wa TFF?Mbona visirani si visirani kila siku kama vya uke wenza
Huyu aliyesema hivi ni Waziri? ... Hapa kuna shida. TFF ni mlezi Wa Vilabu Vyote! Ni baba wa Wote...Leo Unamchukua Mtoto mmoja tena Toto lenyewe ni toto Tundu eti unamweka Kikao na Baba ambaye ni Mlezi Wa Wote..

Hapa Mh Samia tunaomba kwa heshima na taadhima embu Tafakari Upya hii teuzi labda kuna sehemu tuliteleza...Hii ni Wizara Nyeti Sana...! Haistahili kukabidhiwa Watu Wa Hovyo hovyo
 
Elimu za hao unaowaita waandishi na WACHAMBUZI ni zero kbsa. Hawajielewi hao. Ukiwafuata wenye akili tutahoji akili zako
Huyo Haji mnayemuabudu ana elimu gani? Ile barua aliyoandika hata mtoto wa chekechea asingeandika vile! Mbona mikia wamepaniki sana?
 
Manara Kajenga Hoja Yenye mashiko Mechi kusogezwa mbele masaa mawili haimaanishi mchezo umehairishwa...Sasa Wachambuzi wanaacha hoja Wanasifia Ushujaa Wa Yanga 'kutimua mbio' .
All in all Ipo haja na Wao kujitathmini wasitumie vyombo vyao Vibsya.
Naunga mkono hoja ya Haji. Huwezi kuacha kucheza mpira baada ya game kusogezwa mbele kwa masaa

Huu si uungwana hata kidogo ambao wametendewa mashabiki na wadau wa soka kwa vile kuna games nyuma zimefanywa hivyo, kanuni ilikuwa wapi? Au kanuni kwa Simba na Yanga tu..!
 
Kwenye matamko ya serikali hayaanzii kwenye kwanini waliahirisha bali way forward kwenye swala la mechi itachezwa lini. Ndio utajua TFF walipewa maagizo.

Yanga wanaivimbia serikali wakihisi wanaivimbia TFF.
 
Nikimsikia mchambuzi mmoja anaitwa dada ni taka taka kabisa.

Anasema Simba imenufaika na corona ndiyo maana imefika hapo ilipo!Ni ajabu sana kwani Simba siyo mara ya kwanza kifika hapo.
Lakini pia wamewahi kufika fainali za CAF.

Kusema wamefaidika na corona ni dharau za wazi kwa uwekezaji uliofanyika,kwa wachezaji wa Simba,na kwamba anawaona si lolote isipokuwa ni corona imewabeba.
Kibaya sana ni pale hajui hata kuwa ligi ya Misri haikusimama na bado tumewafunga Al ahly.
Simba imeshinda mechi za ugenini na si nyumbani tu.

Wanatia kinyaa kwa uchambuzi wao usio fair ila unajali matumbo yao tu,hasa kwa vile wanaambiwa wafikiri nini na anayewalipa
 
Naanza kwa Kusema 'BIG UP' Kwa Manara.Kwa Kueleza Waziwazi bila Woga Kitendo kibaya Mno Kilichofanywa na Yanga,Kukimbia Mechi Ya Darby bila kujali Umati Ule uliojazana Pale Kwa Kivuli cha Kanuni.La Pili ambalo nalo linastahili pongezi ni kuonyesha Uzandiki kwa Wanaojiita wachambuzi...kwa kutetea na kuubeba Utopolo Uliofanywa na Utopolo Yenyewe 'eti wamefanya Kitendo Cha kishujaa.Hawa Utopolo hawana pa Kuchoropoka mwaka huu, Naziona game mbili clear zinakuja, ya FA na Hii ya VPL ambayo itapangiwa tarehe nyingine .Lazima Vyura wapigwe...!
Wachambuzi Uchwara wamekuwa wengi mno....! Tatizo la ajira linakuja na matokea anuai, wengine Wanavamia fani...!
Acha ushabiki mkuu

kwann simba hamjaja kweny mechi saa kumi na moja kma mnajali mashabiki
 
Back
Top Bottom