Kwa Africa kutokuwa na hela ni shida, ila kuwa na hela ni shida zaidi

gwankaja

JF-Expert Member
May 16, 2011
5,658
2,000
Wakuu kwa Afrika ukiwa na kauwezo kidogo basi ni matatizo zaidi, watu wanaona matatizo yote umeshayamaliza na kilichobaki ni kutatua matatizo yao.

Na usipofanya hivyo basi utapigwa vita za kila aina na kuonekana una roho mbaya na mkatili sana. Kibaya ni kwamba wanakuwa hawajui yaliyo nyuma ya pazia..

Kuna muda unaweza pewa majukumu yaliyo nje ya uwezo wako, na kuyakataa waziwazi unashindwa.

Wana JF Wenye pesa, mnakabiliana vipi na hizi changamoto?
 
mbaritsamenya

JF-Expert Member
Apr 28, 2019
339
500
Huwezi kumzuwia binadam kusema ukiwa huna hela utasemwa na ukiwa nazo utasemwapia chamsingi ni kufanya kileambacho wewe una kiamini na moyo wako unakutuma ufanye hivyo maana hatakama utatoa msaada kama moyo wako hautaki kufanya hivyo hilo nalo ni tatizo pia,(KATAA KUWA MNAFIK)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,629
2,000
Wakuu kwa Afrika ukiwa na kauwezo kidogo basi ni matatizo zaidi, watu wanaona matatizo yote umeshayamaliza na kilichobaki ni kutatua matatizo yao.

Na usipofanya hivyo basi utapigwa vita za kila aina na kuonekana una roho mbaya na mkatili sana. Kibaya ni kwamba wanakuwa hawajui yaliyo nyuma ya pazia..

Kuna muda unaweza pewa majukumu yaliyo nje ya uwezo wako, na kuyakataa waziwazi unashindwa.

Wana JF Wenye pesa, mnakabiliana vipi na hizi changamoto?
Hapo unapopewa majukumu yaliyo nje ya uwezo alafu unayakubali ndipo unapokosea, kataa pale pale atakayekulaumu akulaumu tu kuliko kuyabeba alafu mbeleni unashindwa then lawama zinafata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom