Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Mar 3, 2018
75
799
19983DB5-66CB-4C09-A529-CEF6931B1F57.jpeg

FDC568D7-5F23-42B7-A7FC-DB8FF3C781AA.jpeg

AA9B20A7-3D19-4244-9985-57539E610A9A.jpeg


Nimesoma kwa ufasaha Taarifa zilizoandikwa na Mwandishi Tom Wilson kwenye Gazeti la FINANCIAL TIMES akiwa Uingereza kuwa baadhi ya viongozi wa Jamii ya Tanzania wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Ndugu yangu Zitto Kabwe kuiomba Benki Kuu ya Dunia kuahirisha kuipa Tanzania Dollar Milion 500 za mkopo kwa kile kilichoelezwa kuwa kufanya hivyo ni kuwapiga kofi la uso wanawake ambao wamezuiliwa kusoma huku wakiwa na ujauzito kwenye shule za Tanzania.

Kupitia Barua iliyoandikwa na kutumwa kwenda Benki ya Dunia na Zitto Kabwe wiki iliyopita na kupokelewa na Bodi ya Benki hiyo, Zitto ameandika taarifa za uongo kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli imewanyima haki wanafunzi Wajawazito kusoma na badala yake inawahamasisha wanawake kuzaa kwa kadri ya uwezo wao ili kuongeza idadi ya Watu wa Tanzania. Nitanukuu "Excluded pregnant Girls from School and encourage women to free their ovaries to boost the country's population"

Ndugu Zitto Kabwe na washirika wake wanaamua kupotosha Hotuba za Rais kwenye maeneo tofauti tofauti kwa makusudi ili kukidhi matarajio yao.

Kuunganisha Hotuba za Mh. Rais za maeneo tofauti tofauti ili kuleta maana isiyo sahihi ili kukidhi matarajio yako ni makosa lakini pia ni dhambi.

Kupitia Barua yake Zitto Kabwe ya kushinikiza Tanzania kunyimwa fedha na Benki ya Dunia ameandika pia kuhusu fedha za kupunguza umasikini dola Milioni 450 ambazo ziliidhinishwa mwezi Septemba na benki hiyo kwa kujiridhisha kuwa Tanzania inafuata matakwa ya masharti ya fedha hizo, Zitto ameenda mbali zaidi na kuandika kuwa hakuna kilichobadilika!

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa ambayo Mwanafunzi wa Kike anakabiliwa na Changamoto Mbalimbali katika Masomo yake na Kwa kutambua hilo Serikali ya Tanzania kupitia mpango wa Elimu Bila malipo haukumtenga mwanafunzi wa Kike.

1. Mpango wa Elimu Bila malipo hauna Ubaguzi

Fedha za Ruzuku ya Elimu bila malipo Chini ya mwongozo uliotolewa Tar 28 Decemba 2015 umeelekeza fedha za Ruzuku kwa kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kuwa ni Tsh 6,000 na Sekondari Tsh 25,000 kwa kila Mwanafunzi kwa mwaka bila kujali kuwa ni wa Kiume ama wa Kike na fedha hizo zinatumwa Shuleni Moja kwa moja na kufanya kwa mwaka Serikali kutumia Tsh 12,329,791,183 kwa mwaka. Je, wasichana wetu wamenyimwa haki ya Kusoma?

2. Serikali imekuwa ikifuatilia kesi zinazohusiana na Wanafunzi wanaobebeshwa mimba na Wahusika wamekuwa wakiwajibishwa kwa Mjibu wa Sheria

Kwetu sisi ambao tumekuwa viongozi wa wananchi na kushughulika na matatizo ya wananchi wetu moja kwa moja tumekuwa tukikimbizana na watu wanaowapa mimba wanafunzi wetu na watu wanaokutwa na hatia hiyo wamekuwa wakiwajibishwa.

Kwahiyo maneno ya Zitto kuwa wasichana wenye mimba wamekuwa hawaruhusiwi kusoma na badala yake wanahamasishwa kuongeza jitihada katika kuongeza idadi ya watu Tanzania si za kweli kwani nchi inayowahamasisha wasichana kubeba mimba haiwezi kuweka sheria Kali za kuwaadhibu wanaowabebesha mimba wanafunzi wakati lengo ni kuongeza watu wa Tanzania.

3. Mfumo wa Elimu Nchini umewezeshwa kuwasaidia watu walioacha masomo kwa sababu mbalimbali ili kutimiza ndoto zao

Vituo mbalimbali vya Mitihani na Program za muda mfupi (miaka 2) inatambuliwa na Serikali ya Tanzania kwa miaka kadhaa sasa ili kuendeleza dhana ya Elimu kutokuwa na mwisho.

Ni dhahiri kwamba kama Tanzania ingekuwa inapinga mwanafunzi aliyebeba mimba kukosa haki ya kujielimisha isingetambua mifumo hii inayowarudisha watu hawa kupata haki hii ya Elimu na bado matokeo ya Mitihani yao inawawezesha kujiunga na Elimu ya Juu. Kwa hiyo si kweli kwamba wananyimwa haki ya Elimu.

4. Waziri wa Elimu ni Mwanamke.

Hili nalo pia linaweza kuwa chachu ya kuonyesha ni jinsi gani Serikali ya awamu ya 5 inadhamini mtoto wa kike kwenda shule. Mimi nimeona hivyo sijui nyie mnaonaje. Siamini kama Prof Ndalichako, mama huyu wa Kigoma anaweza kusimamia Wizara ambayo inachimbia handaki jinsia yake. Siamini pia kama Rais Magufuli anaweza kumteua mwanamke kwa lengo la kuzika matumaini ya wanawake kupata Elimu. Inahitaji kuwa na akili ya kichaa kuelewa lengo la Zitto katika kuamusha hisia za jinsia fulani kutengwa kielimu.

Mikopo na misaada inayotulazimisha kuchanganya wajawazito na wasio wajawazito hiyo inatakiwa kuangaliwa kwa macho na akili.

Mkuu wa nchi kukemea tabia za kubebesha na kubebeshwa mimba wanafunzi hapo anakuwa anatimiza wajibu wake. Tafsiri ya maneno ya Rais inayobebwa na mtu kupeleka sehemu fulani kwa lengo la kupotosha huko ni kukosa uzalendo.

Kuandika barua kwa siri kwenda kwenye taasisi ya fedha duniani kwa lengo la kudhuru nchi yako huku ukijua hauna nchi nyingine ya ahadi pia ni kiwango cha juu cha usaliti wa Utanzania wako. Ishitaki Serikali ya Tanzania kwa Watanzania wenzako na siyo kwa Mabeberu pamoja na mawakala wa Ukoloni mamboleo ambao hata hivyo uhusiano wetu na wao unatakiwa uwe wa kutumia akili sana.

Hata hivyo nimeona mrejesho wa Msemaji wa Benki ya Dunia akisema kuwa "Kutakuwa ni kutokomaa ikitokea yeye akazungumza chochote wakati Bodi ya Benki kuu ikiwa haijalitathmini jambo hilo "

Natambua matamanio ya mwanasiasa yoyote kama Zitto ni kuona Kunatokea Agenda yoyote inayoweza kusaidia Chama chake kukua na kutimiza malengo lakini napenda nimueleze kuwa Urais hautafutwi hivyo.

Siku ukiona unasaidiwa na Mataifa ya Nje kutawala Nchi ambayo mwanzoni mlipambana kwa hali zote muachwe ili muwe huru ujue ndio utakuwa mwanzo wa kuwakaribisha Wakoloni tena.

Upinzani wenye nia njema na Tanzania unajishughulisha na Watanzania wenyewe kwenye nchi yao, nenda Kusini, kasikazini Magharibi na Mashariki na kila kona zote za Tanzania, wakikuelewa watakupa Nchi. Urais wa Tanzania haupo mkononi mwa Benki kuu ya Dunia wala Ulaya.

Umewaacha Watanzania kwenye ardhi yao wakiwa wanafaidi mema ya Magufuli itakuwa ni ngumu kwao kukuelewa.

Mwambieni Zitto Serikali ya Magufuli anayoitumu vitu vingi vibaya inaendelea kumlipa Mshahara wake wa Mwezi na hajawahi kukataa hata siku moja Mshahara huo.

Najua atasema ni haki yake kulipwa lakini pia akumbuke kuwa haki hiyo inakumbukwa na Serikali ile ile anayoituhumu kwamba inavunja haki za Binadamu.

Ninasikitika sana kwamba Serikali ya awamu ya nne ilikuwa na mfumo wa kufanya kazi na Zitto lakini hii ya awamu 5 kidogo imejitenga nae kwa kiasi fulani na hivi ndivyo ameamua kuishi na Serikali hii.

Ni matumaini yangu kuwa sasa umefungua ukurasa rasmi wa kuachana na wewe kwenye vyombo vya uwakilishi.

Nchi haitafutwi hivyo.

#KigomaVoteWisely2020 #ourleaderisourproblem

Elia Fredrick Michael
Buyungu, Kakonko Kigoma
 
Kama uliyoandika humu ni kweli nalaumu mfumo mzima wa usalama wa nchi.

Hongera uliyendika, acha chuki za kisiasa zitutafuna iko shida sana kwa black skinned race. Wazungu wajinga tu sijawahi kuwaamini wala kuwapenda nacheka nao meno tu ila moyoni siko nao hawajawahi kumpenda Mwafrika na sitajikomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa mawazo yako ni yako hialuna chama hapa! Nenda kwenye mijadala ya Zitto na kajibu kule. Kajibu hoja ndiyo utaratibu wetu hakuna mambo ya vikundi hapa ni mawazo yako.
 
Back
Top Bottom