Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Ndugu Watanzania,
Dalili zilizowahi kuonekana huko Rwanda kabla ya Mauaji ya Halaiki, Somalia kabla ya Kuvunjika kwa Dola na Sudan katika kipindi hiki cha Kugawanyika kwa Taifa zinajitokeza katika maeneo kadhaa hapa nchini. Watafiti wa masuala ya migogoro, kama Profesa Mahmood Mamdani, wanasisitiza kuwa ni muhimu sana kuelewa nini kinaendelea kabla ya kuzuia tatizo. Hivyo ni vyema watafiti wetu mkafanya hivyo kabla nchi haijasambaratika. Kwa wale ambao mmeshaanza kutafiti migogoro ya Tarime, Hanang, Pemba na sehemu zingine tafadhali naomba muweke wazi matokeo ya tafiti zenu ili tujua ni nini hasa kinaendelea na kufukuta.
Kinga ni bora kuliko Tiba!
Alamsiki,
Kamaradi Kompanero