Kuzuia ya Somalia, Rwanda na Sudan Yasitokee Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuzuia ya Somalia, Rwanda na Sudan Yasitokee Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Feb 12, 2010.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,490
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Ndugu Watanzania,

  Dalili zilizowahi kuonekana huko Rwanda kabla ya Mauaji ya Halaiki, Somalia kabla ya Kuvunjika kwa Dola na Sudan katika kipindi hiki cha Kugawanyika kwa Taifa zinajitokeza katika maeneo kadhaa hapa nchini. Watafiti wa masuala ya migogoro, kama Profesa Mahmood Mamdani, wanasisitiza kuwa ni muhimu sana kuelewa nini kinaendelea kabla ya kuzuia tatizo. Hivyo ni vyema watafiti wetu mkafanya hivyo kabla nchi haijasambaratika. Kwa wale ambao mmeshaanza kutafiti migogoro ya Tarime, Hanang, Pemba na sehemu zingine tafadhali naomba muweke wazi matokeo ya tafiti zenu ili tujua ni nini hasa kinaendelea na kufukuta.

  Kinga ni bora kuliko Tiba!

  Alamsiki,

  Kamaradi Kompanero
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  matatizo yaliyoikumba Rwanda, / Somalia huwezi ukalinganisha na matatizo yanayokumba baadhi ya jamii zetu umenda mbali saana.
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,490
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Ndugu nina nukuu mbalimbali za zamani zinazoonesha kuwa na wao walikuwa wakidai hivyohivyo, kuwa watu wameenda mbali sana. Walionywa sana kuhusu dalili ambazo zilianza kujitokeza toka zamani ila wakazifumbia macho. Ni hatari.
   
 4. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  sio kwamba tafiti hazifanyinki umeenda mbali saana, mfano Mgogoro uliopo tarime huwezi ulinganisha na mgogoro uliopo hanang hata kidogo, njia za kusuluhisha zitakazo tumika tarime ni tofauti kabisa na utakazo zitumia Pemba, kuna report moja tunakaribia kukamilisha naamini ukisoma ukaelewa utajua namaanisha nini,

  Umeenda mbali saana, matatizo ya Sudan na Rwanda ni tofauti saana na matatizo yanayokumba baadhi ya jamii zetu.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,490
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  "The Rwanda genocide unfolded at the same time as the elections marking the transition to postapartheid South Africa - during the first half of 1994. At a meeting of African intellectuals called in Arusha later that year to reflect on lessons of Rwanda, I pointed out that if we had been told a decade earlier that there would be reconciliation in one country and genocide in another, none of us could have been expected to identify the locations correctly - for the simple reason that 1984 was the year of reconciliation in Rwanda and repression in the townships of South Africa. Indeed, as subsequent events showed, there was nothing inevitable about either genocide in Rwanda or reconciliation in South Africa" - Mahmood Mamdani on Saviours and Survivors: Darfur, Politics and The War on Terror
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,490
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Sijasema Tanzania = Rwanda = Sudan = Somalia. Nimesema baadhi ya viashiria vya matatizo yaliyotokea huko na hapa vipo. Hivyo tunapaswa kuvitafiti ili kubaini vyanzo vyake na jinsi ambavyo tunaweza kuvizuia visije vikaleta matatizo makubwa zaidi hapo mbeleni. Kwa taarifa yako jana watu wamepigana huko Hanang. Nasikia wengine wameleta tafrani Segera. Yaani hivi vimlipuko vidodo vikiachiwa vitaungana na kuwa mlipuko mkubwa. Tuelewe matatizo yetu, tujifunze kutoka kwa wenzetu waliolea matatizo yao, kisha tuchukue hatua haraka!
   
 7. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  "haki huinua taifa, bali dhambi i aibu ya watu wote"

  ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake akajitahidi kutenda haki na kusaidia wengine kutend yaliyo ya haki...................
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna tofauti kati yetu sisi na nchi zilizotajwa, tatizo la nchi hizi ni uongozi uliosahau wajibu wa kutoa haki kwa wananchi wake je sisi (TZ) viongozi wetu wanaheshimu wananchi na haki zao? (public opinion ni malalamishi kila kona) dalili namba moja ya kwamba hali haiko salama

  Pili Ugawanaji wa resource unalalamikiwa ndio kuna watu wengi wanaamini wengine (wachache) wanakomba sana mali ya taifa kwakuwa ni kina ndullu, wanasiasa wakati manesi wakilia kila siku..dalili namba mbili (ikaja pasuka huwezi jua hasira ilianzia wapi???

  Tatu Viongozi wanatimiza ahadi zao walizoahadi NO kuanzia mahakama ya kadhi, muungano, uchaguzi wa serikali za mitaaa, uonevu kwa raia (wamachinga vs askari wa jiji) ikaja kulipuka huwezi kujua hasira zote zilianzia wapi...

  Yes tuepuke kuwa buruza wananchi kwenye mambo ya msingi kama haki, usawa wa fursa, na kutimiza ahadi za uchaguzi hivi ni viashiria vya haraka kuleta vurugu popote...
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 0
  Hapa mi sijaona dalili yoyote mbaya. Dalili mbaya kabisa ambayo pindi ikitokea ni lazima tushituke ni wananchi kukata tamaa ya maisha, kuona kuwa kifo na kuishi vyote vina nafasi sawa. Sasa sisi Tanzania kwa sasa wengi tunapenda kuishi ndiyo maana hata kudai haki zetu kwa maandamano tunaogopa mabomu, virungu na risasi za FFU. Kama dalili hii ingekuwepo kwa jinsi bunge lilivyo "flip the bird" on Tanzanians kuhusu Richmond et al basi tungeshapinga.

  Kwa ujumla Tanzania ni nchi ya amani na itaendelea kuwa hivyo mpaka hapo tutakapokata tamaa ya kuishi kutokana na maisha kutokuwa na thamani kwetu kwa umasikini na dhuluma zitakapokuwa zimezidi. Kwa sasa hivi nchi ni shwari kabisa na October tutapiga kura kuchagua tunaowataka watuongoze lakini hatutapata fursa ya kuwapata hao tunaowataka watuongoze kwani timu imeshapangwa na watakaotangazwa washindi hata kama hatukuwapa kura tutakubaliana nao tu kwani ndiyo jadi na utamaduni wetu watanzania kuogopa KUFA kwa risasi na virungu huku umasikini na ufisadi ukituua kwa mamlioni kwa kukosa huduma bora za afya, lishe bora n.k

  IDUMU AMANI YETU TANZANIA MILELE NA WOTE WANAOTUOMBEA MABAYA WASHINDWE
   
 10. Companero

  Companero Platinum Member

  #10
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,490
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Kimya kina mshindo mkuu, ndivyo wambavyo wavyele,
  Kimya chataka kumbuu, viunoni mtatile:
  Kimya msikidharau, nami sikidharawile;
  Kimya kina mambo mbele; tahadharini na kimya.

  Kimya ni kinga kizushi, kuzukia wale wale;
  Kimya kitazua moshi, mato msiyafumbule:
  Kimya kina mshawishi, kwa daima na milele;
  Kimya kina mambo mbele, tahadharini na kimya.

  Kimya vuani maozi, vuani mato muole;
  Kimya kitangusha mwanzi, mwendako msijikule;
  Kimya chatunda pumzi kiumbizi kiumbile!
  Kimya kina mambo mbele, tahadharini na kimya.

  Bwana Muyaka bin Haji

  Kimya kimya msidhani
  Ni ishara ya amani

  - Julius K. Nyerere, Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania
   
 11. b

  bigilankana Senior Member

  #11
  Feb 12, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kesi ya Rwanda, Somalia nk hailingani na Tanzania Kompanero! Ukilinganisha Ivory Coast na Tanzania nitakukubalia. Huko ndiko tunakoelekea kama hatutokuwa makini.
  We are more disunited than ever before. We are more suspicious than ever before. Cracks are widening and we tend not to know. That the country is slowly falling apart is no longer an Unknown UnKnown, but an Unknown Known. By the time it is a Known Known there will be no Tanzania.
  This Nation if founded on what grounds? If i may ask
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,400
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Me nakwambia kwa ufisadi huu lazima badae masikini wawachinje mafisadi!
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Waswahili wana msemo kuwa MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA.
  Matatizo yaliyowapata wenzetu yanaweza kutokea hapa kwetu kwasababu chama tawala kinafumbia macho uovu ambao unazidisha pengo la mgawanyo wa rasilimali za Taifa kati ya walionacho na wasionacho. Wananchi wengi wanapata mlo mmoja kwa siku na wengine wanalala na njaa wakati majirani zao matajiri Masaki wanakula na kusaza; wabunge wanajilimbikizia mishahara minono na marupurupu mengi wakati walimu na wafanyakazi wengine wakiomba kima cha chini cha mshahara kiongezwe serikali inasema haina fedha!! Mambo kama haya ndio yanasababisha machafuko katika nchi.
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Feb 18, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,490
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Unaona sasa yametokea Tarime!
   
 15. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #15
  Feb 18, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  "Hakuna watu waliozaliwa wameshika bunduki wanapigana" -- L. Mrema.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...