Ninajiuliza suala la kupinga huu wimbo wa chura ni kuzuia uhuru wa wananchi kufanya wanachotaka au ni kuvuka mipaka ya uhuru uliopo kikatiba. Tukiwaacha hawa na wafanyao, tutaathirika vipi? Hiyo ndio kazi ya rasilimali chache tulizonazo? Kwa msio ufaham wimbo huo fikeni YouTube unaitwa chura. Nchi hii wananchi wake wanapenda sifa
Nilikua nairudia hii video ya Marehem Chura wa Snura niangalie Hicho kinachoitwa utovu wa nidham na Uvunjifu wa Maadili!!Mbona kuna video za hivi nyingi Sugua gaga,diamond Ule wa mahadhi ya taarab!!na nyingine nyingi ! Sijakiona cha ajab kwenye Chura au kilichozidi zaidi ukilinganisha na...
1.Video nyingine za bongo ambazo wamekua wanakata mauno hasa za miondoko ya hivo
2.video za nyimbo za nje kama Marekani ambazo zinapgwa kwenye runinga zetu
3.Post za Picha za uchi na video za wa bongo wanazo advertise Instagram,Facebook au Whatsapp
Unafungiaje wimbo kama huu ambao n afadhali wakati kuna access ya porngraph internet 24hrs,kuna baikoko live,kanga moja live na YouTube tena ni Bongo!! Hivyo vyote bado vipo na vinatazamwa deilee na ndivo vinaharibu jamii??
Mawazo yangu tu!!
Labda wengine mniambie
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ni si kongwe kama ilivyo BASATA, lakini pamoja na kuongozwa na wasomi na watu wenye uzoefu mkubwa lakini matokeo ya utendaji wao aidha umekuwa butu wa makengeza au usiokidhi viwango vya kile kilichotegemewa kutoka kwao.
Tasnia ya sanaa Tanzania inakua kwa kasi, sasa ni ajira rasmi inayotegemewa na wengi...! Kazi ya kutengeneza mziki mmoja au filamu hujumisha utaalam tofauti ambako kote huko watu hupata kula yao.
Kumekuwa tabia ya mlipuko wa kufungia kazi za wasanii kutoa adhabu baada ya hapo kimya.
Lakini hawa wana jukumu kubwa sana la kusimamia hii tasnia muhimu
Waunde sasa chombo cha kuratibu kazi zote za sanaa kabla ya kurushwa hewani, hiki chombo ndio kitakuwa na jukumu la kuangalia mapungufu ya kazi yenyewe na kuona kama inafaa kuwapelekea walaji kulingana na mila tamaduni na desturi zetu.
Wasanii wengi ni vijana chini ya miaka 30 wanaohitaji miongozo ya kila aina, wana vipaji lakini wanakosa uzoefu na hata hekima kwenye mengi...pesa zao wanapata kwa shida Sana hivyo ni vema wakapata chombo cha kupitia kazi zao kabla hawajazitoa ili kuepuka hasara kama hizo za kufungiwa.
Kutegemea wasimamizi binafsi na waongozaji haisaidii kwakuwa tumeona mara nyingi makosa yakijirudia.
Isaidieni Tanzania wasaidieni vijana wetu waweze kusimama tokeni ofisini undeni chombo cha kuratibu kazi zao kabla hazijatoka hili ni jukumu lenu nyie