Kuzuia ujenzi wa kituo cha mafuta Lake Oil Mwanza ni hujuma?

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,142
15,130
Wanabodi taarifa ya habari itv imeonesha maafisa wa NEMC Mwanza wakizuia ujenzi uliokamilika wa kituo cha mafuta lake oil kisa ni hatari kwa mazingira. Binafsi nakifaham kituo hicho na nimekiona tangu wanaanza kuchimba na kukata mwamba ajabu siku zote hizo NEMC hawakuona hadi watu mamemaliza wako hatua za mwisho eti ndio wanatutangazia kuzuia sabab ya hatari za kimazingira.

Binafsi nimewadharau sana NEMC kwa hili kwa sabab wanaonekana kufanya kazi kisiasa kwani kituo hicho hakijaota kama uyoga na ardhi hawajaokota tu kuanza ujenzi huo. Huku ni kurudishana nyuma kama nchi na namna hii hatuwezi kufika kwani kituo barabarani kabisa na wamekiona tangu jamaa wanakata mwamba
 
Hata wenye kujenga kituo hicho walitakiwa kulijua hilo kama kosa limegundulika unataka liachwe liendelee?
 
Wanabodi taarifa ya habari itv imeonesha maafisa wa NEMC Mwanza wakizuia ujenzi uliokamilika wa kituo cha mafuta lake oil kisa ni hatari kwa mazingira. Binafsi nakifaham kituo hicho na nimekiona tangu wanaanza kuchimba na kukata mwamba ajabu siku zote hizo NEMC hawakuona hadi watu mamemaliza wako hatua za mwisho eti ndio wanatutangazia kuzuia sabab ya hatari za kimazingira. Binafsi nimewadharau sana NEMC kwa hili kwa sabab wanaonekana kufanya kazi kisiasa kwani kituo hicho halijaota kama uyoga na ardhi hawajaokota tu kuanza ujenzi huo
Ha ha ha baba umeuaaa... "WAMEZUIA UJENZI WA KITUO CHA MAFUTA AMBAO UMEKAMILIKA." c ndo wanatafuta kick... Wapuuz sana hawa jamaa walikua wapi mpaka ujenzi umefika mbali kiasi kile..
 
Kwani mmiliki wa Lake Oil ni nani?

Labda tuanzie hapo ndo tujue kama ni sababu za kisiasa ama la?
 
Ha ha ha baba umeuaaa... "WAMEZUIA UJENZI WA KITUO CHA MAFUTA AMBAO UMEKAMILIKA." c ndo wanatafuta kick... Wapuuz sana hawa jamaa walikua wapi mpaka ujenzi umefika mbali kiasi kile..
Yaani hizi siasa sasa zinatupeleka kubaya mkuu...haiingii akilini kabisa...kituo hicho kimejengwa mchana kweupe kabisa mi napendaga kukaa pale Hotel Tillapia kupata drink na unaona kila kitu kinavyojengwa pale kituoni halafu wao wanadanganya umma kinajengwa usiku. Wawajibishwe kwa uzembe hawa jamaa wa NEMC
 
Hata wenye kujenga kituo hicho walitakiwa kulijua hilo kama kosa limegundulika unataka liachwe liendelee?

Inaelekea NEMC walitengeneza mazingira ya rushwa kwa sasa wanaona wajikakamue kwani itakula kwao, NEMC watumbuliwe pia kwa kufumbia macho makosa hadi muwekezaji akamaliza ujenzi! Kuna harufu ya mulungula hapo, watumbuliwe bila ganzi! Uzembe kama huo ndio unamfanya JPM kuagiza wataalamu wa IT kutoka Rwanda sisi tunabaki tunalalama tu!
 
Kwani mmiliki wa Lake Oil ni nani?

Labda tuanzie hapo ndo tujue kama ni sababu za kisiasa ama la?
Regardless mkuu... Haiingii akilini maana kile kitendo cha kupasua mwamba na kusawazisha kimechukua mda mrefu tu na wao kama kweli wanafanya kazi wangehoji..si hapo kilipofikia inaonekana imebaki kufunga pump tu ndio wanaibuka. Mi kama msaka pesa wa kawaida inaniuma sana...huko ni kutafutana ubaya na watu
 
Ndio mjue serikali hailali ila watumishi ndio hulaza kazi za serikali.

Unaweza kutoa rushwa kulinda maslai yako kwa muda mfupi, lakini huwezi kutoa rushwa ili kubadili sheria za nchi zikulinde wewe.!
 
Yaani hizi siasa sasa zinatupeleka kubaya mkuu...haiingii akilini kabisa...kituo hicho kimejengwa mchana kweupe kabisa mi napendaga kukaa pale Hotel Tillapia kupata drink na unaona kila kitu kinavyojengwa pale kituoni halafu wao wanadanganya umma kinajengwa usiku. Wawajibishwe kwa uzembe hawa jamaa wa NEMC
Ndo nchi ya mwendokasi hii baba... Haya nyie wa mwanza c wa dar tunasubir utekelezaj wa kupaka rangi zetu nyumba, tunakaz ya kukagua akaunt zetu za mitandao kama tumewah kufollow mashoga ... #nchiyamwendokasi
 
Regardless mkuu... Haiingii akilini maana kile kitendo cha kupasua mwamba na kusawazisha kimechukua mda mrefu tu na wao kama kweli wanafanya kazi wangehoji..si hapo kilipofikia inaonekana imebaki kufunga pump tu ndio wanaibuka. Mi kama msaka pesa wa kawaida inaniuma sana...huko ni kutafutana ubaya na watu
For sure mkuu, kuna maelekezo mahala fulani, maana nimemsikia mwanasheria mkuu wa NEMC akisema kwamba wanachosubiri sasa hivi ni saini ya waziri wa mamlaka husika....

Inatia shaka sana.!
 
Ndo nchi ya mwendokasi hii baba... Haya nyie wa mwanza c wa dar tunasubir utekelezaj wa kupaka rangi zetu nyumba, tunakaz ya kukagua akaunt zetu za mitandao kama tumewah kufollow mashoga ... #nchiyamwendokasi
Mkuu mi si wa Mwanza kule naenda mara nyingi sana kikazi.. Ndio maana nimeshangaa maana kila nikienda nikirudi nakuta ujenzi unaendelea mchana kweupe kabisa
 
Ndio mjue serikali hailali ila watumishi ndio hulaza kazi za serikali.

Unaweza kutoa rushwa kulinda maslai yako kwa muda mfupi, lakini huwezi kutoa rushwa ili kubadili sheria za nchi zikulinde wewe.!
Yatawafika tu....wanakurupuka sana
 
Back
Top Bottom