Kuzuia mikutano kwa miaka 5 kumeleta CCM kuwa butu kwenye Siasa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Mimi kama Mtanzania nashangazwa na viongozi wa CCM wa kisasa kuwa butu kiasi hiki.

Wakati wa Kinana walikuwa wazuri kujibu hoja, kuongea na wananchi na kupiga kampeni. Ukiangalia vizuri viongozi wa CCM ni kama wamezubaa ukilinganisha na Lissu, Membe, Zitto au Lipumba. Hii ni kwa sababu kwa miaka mitano kulikuwa hakuna mikutano.

Kwa miaka mitano walikuwa wanaongea na makada tu ambao wanapiga makofi. Hawa viongozi wa sasa hawajawahi kuzomewa, kukutana wa wananchi wa vyama vingine na kujibu hoja. Kibaya zaidi hata vyombo vya habari vinaogopa kuuliza maswali ya muhimu.

Kwasababu ya kuwa butu wameishia kutishia zaidi kuanzia waandishi wa habari mpaka wasanii. Mimi nashauri waanze kutoka na kujibu hoja hasa katibu mkuu. Huwezi kujaza watu kwenye gari moshi kwenda Arusha kwa masaa mengi zaidi ya kwenda Dodoma kutokea Kilimanjaro ukafikiri watu watapiga kura kwasababu ya viti kama hivi.

Vilevile huwezi kutegemea kuiba pekee kwasasa mbinu zote wamezijua kwasababu ukiwa butu hata ubunifu unapungua
 
Back
Top Bottom