Kuzuia mchakato wa Katiba Mpya ni kuwadharau watanzania

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,131
2,000
Ndugu wanaoweza kutafakari vizuri na kuweza kuangalia mambo kwa upana na umuhimu wake mtakubaliana na mimi kuwa mchakato wa katiba uliungwa mkono na Watanzania takribani wote. Katiba mpya siyo uhitaji wa chama fulani au utashi wa mtu fulani, ni hitaji kubwa la nchi yetu kuwa na katiba ambayo tumeitunga wenyewe kwani tuliyonayo siyo maoni ya watanzania kama ilivyo hii rasimu ya mzee Warioba.

Rais JK pamoja na serikali aliyokuwa anaiongoza aliona ni vema kukubaliana na matakwa na wananchi ya kuwa na katiba mpya kama wanavyotaka. Hivyo mchakato wa katiba mpya ulianza na wananchi wote walifurahia sana.

Kitendo cha mtu kusitisha mchakato huo na kujinadi kuwa haikuwa agenda yake wakati wa kampeni ni kuwadharau wananchi waliamua kuwa na katiba mpya kwa maslahi mapana ya taifa lao. Katiba siyo mali ya Rais wala chama chochote cha siasa bali ni makubaliano ya wananchi ya jinsi gani ya kuendesha nchi.

Hivi kwa hali ya kawaida, kuna mtu mwenye hekima na akili nyingi kuliko Watanzania wote kiasi cha kuona yeye ndiye mwenye haki ya kuzuia kile wananchi wanachokitaka? Kuzuia mchakato wa katiba ni kuwadharau Watanzania.
 

Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,943
2,000
Ni kwali kabisa. Hili sio la kulidharau kwani katiba ni muhimu kuliko huduma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom