Kuzuia kwa kurusha maudhui ya nje ya nchi katika vyombo vya habari, tutegemee nini?

Spectator

JF-Expert Member
Aug 26, 2017
225
509
Habari za usiku jamvini,

Kuzuia kwa kurusha maudhui ya nje ya nchi katika vyombo vya habari, tutegemee nini?. Kwenye international trade kuna kitu kijaitwa “retaliation” au majibizo ya kisasi.

Mfano; Nchi zingine zikizuia pia kuonyesha maudhui ya Tanzania itakuaje?

1. Matangazo ya vivutio vya kitalii Tanzania ykifungiwa, inamaana ndio kifo cha utaliu Tanzania?

2. Wasanii, yaani muziki na filamu kazi zao zikizuiwa nchi za nje, inamaa hata fedha za kigeni zitapungua. Diamond, Alikiba na wengine wakienda matamasha huwa wanalipwa hivyo tunapata fedha za kigeni. Hivyo tunaua soko?

3. Matangazo ya biashara na taarifa kwa wawekezaji wageni zikisitishwa itakuaje? Je tunaua soko letu na mvuto wa kibiashara nje ya nchi?

Nakaribisha maoni.
 
Lissu aliposema tumerudi nyuma miaka 50 iliyopita watu hawakumuelewa kabisa!!!!!
 
Mfano; Nchi zingine zikizuia pia kuonyesha maudhui ya Tanzania itakuaje?

hivi ni nani huko nje anyehitaji maudhui ya Tanzania? Kama yapi?

Soma hii thread:

Tanzania haijulikani Duniani kiivyooo kama magazeti yetu yanavyoripoti eti Dunia nzima ni Tundu Lissu tu!

Naona waandishi wetu wamekazana kweli kutafuta taarifa za Tundu Lissu zilivyoripotiwa nje ya nchi.

Maajabu hata mtu mmoja kutoka nchi fulani aki tweet tu basi inachukiliwa eti huo ni mtandao nao ulioripoti habari ya Tundu Lissu.

Lengo la wana habari ni kuifanya taarifa ya Tundu Lissu kuwa Dunia nzima imekuwa inaripoti kwahiyo ni taarifa kubwa sana.

Hata CNN hawajaripoti tu halafu tumetoka mishipa ya shingo eti Dunia nzima ni Lissu tu.

Watanzania tuna shida sana Mimi sijui lengo la waandishi hawa ni nini sijui?
 
Back
Top Bottom