Kuzuia kuhoji matokeo ya uraisi mahakamani ni udikteta...............

Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
Ukitaka kujua sifa za nchi ambazo haziendeshwi kidemokrasia kama hii ya kwetu utaona viongozi waliko madarakani hawapo tayari kuhojiwa na mahakama au chombo cho chote kile pale wanapofanya maamuzi................wao hujiona ni Miungu watu kwenye maamuzi yao na wako juu ya sheria kwa kutoweza kuwajibishwa na chombo chochote kile................

Kwa kuelewa vile, ndiyo maana NEC imetumia mabavu kumtangaza JK ambaye hata hakufikisha kura milioni tatu kuwa Raisi wetu huku wakimwibia Dr. Slaa kura zaidi ya milioni nne kwa mahesabu yangu ya kujumlisha matokeo ya kila kituo hapa nchini..

Dhuluma hii ni balaa na kama Baba wa taifa Mwalimu J.K Nyerere alivyotutahadharisha siku za nyuma ya kuwa aliyezoea kula nyama ya mtu ataendelea hivyo hivyo kubeba laana hiyo ya kula nyama ya watu.............Na CCM ambao wameingia madarakani kwa misingi ya dhuluma usiwategemee kamwe kuwa wataijenga nchi hii kwa misingi ya utu hata kidogo................watendeleza dhuluma iliyowaingiza madarakani tu.............Huu ni wakati wa kuendelea kulilia kufa kwa demokrasia hapa nchini...........
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Ukitaka kujua sifa za nchi ambazo haziendeshwi kidemokrasia kama hii ya kwetu utaona viongozi waliko madarakani hawapo tayari kuhojiwa na mahakama au chombo cho chote kile pale wanapofanya maamuzi................wao hujiona ni Miungu watu kwenye maamuzi yao na wako juu ya sheria kwa kutoweza kuwajibishwa na chombo chochote kile................

Kwa kuelewa vile, ndiyo maana NEC imetumia mabavu kumtangaza JK ambaye hata hakufikisha kura milioni tatu kuwa Raisi wetu huku wakimwibia Dr. Slaa kura zaidi ya milioni nne kwa mahesabu yangu ya kujumlisha matokeo ya kila kituo hapa nchini..

Dhuluma hii ni balaa na kama Baba wa taifa Mwalimu J.K Nyerere alivyotutahadharisha siku za nyuma ya kuwa aliyezoea kula nyama ya mtu ataendelea hivyo hivyo kubeba laana hiyo ya kula nyama ya watu.............Na CCM ambao wameingia madarakani kwa misingi ya dhuluma usiwategemee kamwe kuwa wataijenga nchi hii kwa misingi ya utu hata kidogo................watendeleza dhuluma iliyowaingiza madarakani tu.............Huu ni wakati wa kuendelea kulilia kufa kwa demokrasia hapa nchini...........
Tuandamane au vp?
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
Tuandamane au vp?
Hakuna uhaja kutokana na mazingira ya uchaguzi huu kwani Chadema haki ya kimsingi wanayo ya kuhoji NEC kutofuata taratibu za kisheria kama zilivyoainisha na Ibara 41(5) kwa sababu zifuatazo:-

Ibara Na 41(5) ya Katiba ambayo yasema NEC ni lazima iheshimu taratibu za kisheria za sheria ya uchaguzi zilizowekwa katika kumpata Raisi..........................na baada ya hapo rudia kusoma Ibara Na. 41(7) ambayo imeweka bayana kuwa matokeo ya Uraisi hayatahojiwa na chombo cho chote kama yalipatikana kulingana na maelekezo ya Ibara hii ya 41......................

Swali ambalo unapaswa kujiuliza hivi NEC walizingatia Ibara 41(5) ya katiba katika kumtangaza JK kuwa ni Raisi? Jibu ni hapana.........sasa kama ni hapana maangalizo yaliyotolewa na katiba ya aina gani ya matokeo ya Uraisi ambayo mahakama haiwezi kuyahoji imetimizwa? Jibu ni hapana............sasa hoja ya kuwa Ibara 41(7) imekataza mahakama kuingilia NEC linatoka wapi?

Labda kwa manufaa ya ambao hawajui Ibara hii ya 41(5) ninainakili hapa:-

"All the other matters concerning to the procedures for the election of the President, shall be as provided for in law enacted by Parliament in that behalf,..............................

Sasa Ibara ya 41(7) ambayo wengi humu wanaikimbilia kutetea ututusa uliomo ndani ya Chadema ni hii hapa:-

"When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate."

Maeneo niliyoyawekea alama nyekundu ndiyo ambayo mahakama itabidi iyachunguze ya kuwa je NEC iliheshimu Ibara ndogo 41(5) kabla ya kumtangaza JK kuwa Raisi wetu na hivyo kuinyima mahakama uhuru wa kuchunguza matokeo hayo? Na matokeo ambayo mahakama haiwezi kuyachunguza ni yale tu ambayo mahakama itajithibitishia ya kuwa hayakukiuka Ibara yote ya 41 kama angalizo hili lisemavyo kwenye Ibara tajwa:-..................................to have been duly elected in accordance with this Article.....................
Kwa hiyo Chadema hawapaswi kuandamana kwa sababu wao wanadai kura za Uraisi zilizotangazwa vituoni au na wasimamizi wa chaguzi majimboni NEC hawakuzitumia katika kumtangaza JK kuwa ni Raisi wetu hivyo masharti ya Ibara Na. 41(7) iliyoweka mazingira ya kuzuia mahakama kuhoji matokeo haijazingatiwa na hivyo mahakama inao uhuru wa kuyahoji matokeo hayo...................

Kwa sababu hizi, hatuna msingi wa kuandamana hata chembe.......ila Chadema watimize jukumu lao la kikatiba la kwenda kudai haki yao ya kimsingi Mahakamani iliyobainishwa na Ibara Na.
41(5) ambayo ndiyo kama imefuatwa yawa ni msingi mkuu wa kuzuia mahakama zisihoji uhalali wa kura ya Uraisi chini ya Ibara Na.41(7).........
 
Forum statistics

Threads 1,236,923
Members 475,327
Posts 29,272,800