Kuzuia baadhi ya mavazi CBE ni kinyume na haki za binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuzuia baadhi ya mavazi CBE ni kinyume na haki za binadamu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Tuko, Apr 6, 2012.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nimekerwa sana na kitendo cha naibu mkuu wa chuo cha CBE, Bw Othman Hemed na timu take kukataza wanafunzi kuvaa mitindo mbalimbali ya nguo na kuamuru wavae mitindo anayopenda yeye kwa kisingizio cha MAADILI YA KITANZANIA.

  Kwanza nina uhakika (kama yupo anayebisha na aje), kuwa hakuna mwongozo wowote ni yapi MAADILI YA MTANZANIA. Kwa maana hiyo hayo maadili ya mtanzania ni kitu cha kufikirika tu, hakipo.

  Watanzania tunaongozwa na katiba, na mwananchi yeyote ana haki ya kufanya lolote ili mradi asivunje sheria. Bw Othman aulizwe sheria gani anayokuwa amevunja mwanachuo akivaa jeans iwe ya kubana au kuachia? Bw Othman atuonyeshe katika sheria za nchi au za chuo ni wapi pameanishwa urefu wa sketi ili isiwe kimini, mitindo ya nywele au upana wa suruali. Tunafahamu sheria inakataza mtu mzima na mwenye akili timamu kuwa uchi hadharani, na imedefine uchi kuwa ni hali ya mtu kutokuvaa nguo zinazositiri uke/uume. Kuna nchi nyingine hairuhusiwi hata kuonyesha matiti nje, lakini kwa Tanzania haikatazwi, na ndio maana sio kitu cha ajabu kuwaona kina mama wakiwa vifua wazi.

  Tunafahamu kuwa zipo tamaduni za makabila tofauti ya kitanzania, na kati ya hizo zipo za uvaaji zinazoruhusu sehemu kubwa ya mwili kuachwa wazi.

  Kwa mantiki hiyo, kitendo cha uongozi wa CBE kuwazuia kusoma wanafunzi wanaovaa baadhi ya mitindo ya nguo na nywele, ambayo kwa uhakika wangu ni kuwa haivunji sheria za nchi, na wanaovaa ni watu wenye akili timamu na wanajua wanachokifanya, ni kitendo cha kizandiki, na kinafiki, na cha kipumbavu.
   
 2. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Vaeni Magagulo hayo acheni kulia lia.
   
 3. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,805
  Likes Received: 20,766
  Trophy Points: 280
  mimi nafikiri huyu mkuu wa chuo CBE ana chanamoto nyingi sana na hicho chuo kuliko mavazi,nilibahatika kuona darasa la cbe kwa kweli linasikitisha!lkn leo hii mkuu wa chuo badala ya kuhangaika kuimprove quality ya education chuoni anahangaika na mavazi,kama tumefikia kumfundisha mwanachuo hata nguo gani avae basi tuna kazi kubwa.....
   
 4. c

  cilla JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  mambo ya haki haki utafungishwa ndoa ya ushoga. kwani nguo sizakujisitiri iweje uonyeshe viungo. vyako nje. hayo ni mavazi ya kikahaba. unahaki ya kufanya lolote lakini sio sahihi kufanya lolote.mimi nampongeza. munataka kujifanya wazungu wakati waafrika unatofauti gani na anayejikoboa ngozi.
   
 5. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Big up mkuu wa chuo cha CBE,viungo vya mwili (haswa wa mwanamke) vinavutia sana wanaume! Sasa wewe unafkiria nini kitatokea mwanamke akivaa nguo zinazoonyesha sehemu za mwili wake (kama vile mapaja,matiti,mgongo,kifua,kiuno,tumbo nk)?? Haya ndo mambo yanayoendekeza umalaya na gonjwa la ukimwi kuendelea kusambaa. Wewe unazungumzia haki za binadamu,wewe unazijua haki za binadamu? Kwa hali hii hata USHOGA utasema haki ya binadamu.Fikiri kabla ya kuzungumza wewe!
   
 6. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha fikra finyu,haki za binadamu zinatetea mtu kukaa matiti wazi?
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  fafanua vema haki zipi za binadamu kakiuka na zimeanishwa ktk katiba ipi?
  katiba haiheshimu tamaduni na haiba ya Mtanzania?
  vaeni mavazi yanayostahili na msome acheni kuonyesha maungo nddio maana elimu ya sasa imeshuka sana
   
 8. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  umekurupuka hujui usemalo na lilolosemwa. .
   
 9. s

  silent lion JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Hawa ndo kina Cameroon. Siku amkute mtoto wake anashikishwa ukuta ndo atajua haki za binaadamu
   
 10. m

  mgadafi Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkaeta mada anaect uzungu kumbe mbwibi la hatari
   
 11. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Uhuru bila mipaka ni uendawazimu, unaishi kwa kuangalia maandiko waliyoandika binadamu wenzio ambao nao pia ni dhaifu kama wewe, maadili zaid hupatikana ktk utashi wa binadamu na ndipo busara ilipo,
  haki,haki, haki? Haya anza na familia yenu hadi wanao wavae hayo mavazi yaliyopigwa marufuku,
  unaelekea kwenye ushoga!!
   
 12. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mpeleke mahakamani akakuonyeshe ametumia vifungu gani vya katiba. Labda umesoma ukurasa mmoja umeacha ule wenyewe unaokataza kwa sababu hutaki kuona yaliyoandikwa hapo. Uchi kwa kweli watoto wa kike na midume fulani ilikuwa inavaa, hata kama haisemwi popote, nina hakika inasemwa kwenye dhamira zako. Kama wewe unapenda basi shinikiza chuo cha watu wanaovaa hivyo kifunguliwe kisiwani ambako watu hawana hisia za kujamiiana zinazoweza kuamka haraka kwa uchokozi wa dada zetu ambao wamekubuhu utadhani ukiwaambia una njaa watakupa hapohapo, kumbe wanachombeza maksi za walimu wasiovumilia.
   
 13. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  wale waliozoea kula kwa macho halafu wanahifadhi taswira kwenye bongo zao kisha wanaenda kupigia nyeto kunako faragha kwisha habari yao! wanaume wamechoka kutembea mitaani huku mikono mfukoni siku nzima ili kumficha "mzee mabruk" asionekane kapanda jazba!
   
 14. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  huu ndio uendawazimu mbaya kuliko, sasa wewe unawezaje kupaka rangi nyumba ilikongoroka kwa nyufa,
  kumbuka maadili/uadilifu ni msingi mkubwa wa maarifa,
   
 15. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  Mimi naona hatua aliyochukua sawa kabisa, maana hasa madada wanavaa ovyo mpaka wa lecturer wanapata wakati mgumu darasani kisa maungo nje nje.
  Haya masuala ya haki za binadamu ndio yametufikisha hapa tulipo na ukameruni, watoto wasipigwe hata wakikosa kisa haki za binadamu.
  Bora vyuo vyote waseme watu wavae mavazi ya kujisitiri makata k, na vimini vipungue maana khaaaa......
   
 16. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  Hahaha uzungu umezidi mimi ningekuwa na madaraka nchi hii na wale watoto wakiume kama wa clouds tv amabao wamejitoboa toboa wakaweka mahereni, ngepiga marufuku.
  Uzungu na umarekani umezidi ulimbukeni tu mmeambiwa mvae vizuri manaanza kulalamika hahaha
   
 17. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,485
  Likes Received: 5,961
  Trophy Points: 280
  mbona makazini kuna sheria za uvaaji, nao wanavunja haki za binadamu? acha ugebwe.
   
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kuna watu huwa wanaropoka tu kwa sababu hatuwaoni. Hivi waliliona tangazo lililowekwa na michoro ya mavazi yaliyokatazwa? Watu wanakuja na visketi vinavyoonesha chup.i hadharani na we unatetea? Watu wanatembe matiti nje na we unataka haki za binadamu wakusaidie? Hizi haki za binadamu zinatufanya tuwe na mawazo mgando na kufikiria kufanya mambo ya kipumbavu badala ya kufikiria kutumia elimu yetu itukomboe na umaskini.
   
 19. mamLook

  mamLook Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Dah yani umemjibu kiungwana sana
  -hopeful atasoma na kulaumu nafsi kwann ameandika hii post
   
 20. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Sahihi kabisa kuna haki na wajibu. Ni haki yako kukaa bila nguo yo yote mwilini lakini ni wajibu wako kuvaa nguo za heshima kwenye jamii.
   
Loading...