Kuzuia akina 'Zitto na Nassari' zaidi, CHADEMA inahitaji kuwa na mafunzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuzuia akina 'Zitto na Nassari' zaidi, CHADEMA inahitaji kuwa na mafunzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bams, Jul 27, 2012.

 1. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,612
  Likes Received: 2,993
  Trophy Points: 280
  Taasisi yeyote ile ili iweze kutenda kazi kwa uadilifu, ufasaha na kwa tija ni lazima ifanye kazi kama team, na ukitaka kuwa na team ni lazima uwe na mafunzo, program za mafunzo na mfumo wa kupima ufanisi.

  CHADEMA imekusanya watu wengi kwa muda mfupi; viongozi, wanachama na wapenzi na hawa watu wameunganishwa na tamaa kubwa ya kutaka mabadiliko. Kila mmoja ametoka kwake akitaka mabadiliko japo ni dhahiri kuwa si mabadiliko yote yanayotakwa na kundi fulani ndiyo yanayotakiwa na makundi mengine yote. Kuna vijana wengi ndani ya CHADEMA, wenye akili, ujasiri na mbinu mbalimbali lakini hakuna mwonekano wa wazi wa hao wote kuwa na akili za kufanya kazi pamoja kwaajili ya kutenda mambo kwa umoja kwa lengo moja. Wapo vijana wenye ujasiri, lakini ni ujasiri wa kufanya nini? Kuna wenye uwezo wa kupanga mbinu mbalimbali, lakini ni mbinu za kufanya mambo gani?

  Natoa mifano michache kwa wale ninaowafahamu japo inawezekana wapo wengine ambao hatuwafahamu.

  Nawatumia Zitto, Mnyika na Nasari kuelezea hoja hii. Zitto ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja, kuiwasilisha na kuitetea kiasi cha hata kuifanya hoja isiyo sahihi ikaonekana kuwa ni sahihi. Zitto ana uwezo mkubwa wa mbinu za chini chini, nzuri na chafu katika kuyafikia malengo anayoyataka. Matatizo ya wazi ya Zitto ni ubinfsi, uking'ang'anizi na kutokusiliza watu wengine. Anapenda sana kusikilizwa kuliko kusikiliza wakati ni ukweli kuwa kiongozi mzuri ni yule anayependa zaidi kusikiliza kuliko kusikilizwa,ni yule anayependa zaidi kutenda kuliko kuongea.

  Nasari ni kijana mpya sana katika siasa. Ana uwezo mkubwa wa kuongea na kuvuta watu lakini mlipukaji, na wala hana umakini katika kuongea. Kupita kwake katika kinyang'anyiro cha ubunge kulichangiwa zaidi na watu kuichukia CCM, nguvu za watanzania wengi nje ya jimbo lake na vyombo vya habari vingi kutaka mabadiliko na siyo imani juu ya uwezo wake wa kuongoza.

  Mnyika, ni kijana mwenye utulivu mkubwa wa akili, anaonekana anapenda sana kusoma na kufuatilia vitu hata vile vilivyo vidogo sana. Ni mtu anayependa sana uongozi wa kitimu na ni mwenye uvumilivu wa hali ya juu na subira kubwa. Huyu ni kijana ambaye, tofauti na wenzie kama akina Zitto, Mdee na Nasari, ameitumikia CHADEMA kwa muda mrefu bila kuwa na nafasi za kumletea malipo binafsi/mshahara lakini hakuonekana kukata tamaa. Inaonekana anakipenda sana chama chake na ndiyo maana haijaweka kutokea hata mara moja akaonekana kutenda kinyume cha matakwa ya chama chake.

  Sifa hizi nilizozitaja kwa pamoja kwa hawa wachache ni muhimu katika uongozi wowote ule kama zikiwekwa pamoja, zikafanya kazi pamoja, huku kila mmoja kufuatana na sifa zake, akatumika mahali ambapo ana nguvu (strengths) na akazuiwa kufanya mahali ambapo ana mapungufu makubwa (weaknesses). Na hilo litawezekana endapo tu CHADEMA itakuwa na mafunzo yake ya ndani kwa viongozi wake, watendaji wake na makada wake. CHADEMA inahitaji kuwa na intelijensia yake ya ndani ambayo kazi mmojawapo iwe ni kuwasoma viongozi, makada na watendaji wake ili kujua uwezo na mapungufu yao kwa lengo la kuimarisha na kujenga vipaji na uwezo wao na kuondoa mapungufu yao.

  Kwa mfano, kwa kujua mapungufu ya Nasari na kutambua uwezo wake wa kuongea, anatakiwa ashauriwe kutokuhutubia au kufanya press conference bila ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi wenzake. Kwa kufahamu kasoro kubwa ya Zitto ya ubinafsi, ashirikishwe zake kwenye mijadala ya maumuzi lakini asiwe msemaje wa maamuzi, na aongozwe mpaka afikie mahali ambapo katika lolote analolifanya ni lazima awashirikishe na kuwahusisha viongozi wengine. Kwa kutambua uwezo mkubwa wa Mnyika wa umakini wake, uvumilivu na tabia ya kupenda sana kusoma na kuchungua, anastahili kutumika kama mhimili mkuu wa chama, huyu ni kiongozi ambaye hakuna mwanachama ambaye ana mashaka naye juu ya 'commitment' yake kwa chama.

  CHADEMA pia inahitajika kuweka miiko ya viongozi wa chama. Kwa mfano wewe ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyeketi, Katibu Mkuu au Naibu Katibu mkuu ambaye una majukumu ya kuhakikisha chama chako kinapata wagombea wazuri, halafu unabaki unazunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi na wanachama kuwa mimi nitagombea Urais, haileti mantiki. Ukifanya hivyo wewe kiongozi wa chama unawanyima fursa na kuwavunja nguvu wanachama wenzako wenye nia hiyo hiyo ambapo katika hatua fulani ni lazima wafikishe maombi yao kwenye meza yako wewe kiongozi wao. Kwa uzoefu wetu, viongozi wa juu wa chama kama kila mmoja akataka na hata kutangaza nia ya kugombea Urais, basi ni lazima mshikamano wa uongozi wa juu wa chama utapotea kwa vile kila mmoja wao ataanza kuunda timu yake ya kampeni. Wanachama wa kawaida wakitangaza nia zao hakuna madhara makubwa kwa chama, ndiyo maana kila kiongozi wa juu anayetangaza nia ya kugombea Urais anadhoofisha nguvu na umoja wa uongozi na wanachama. Ni vizuri ukawekwa mwongozo unaozuia viongozi wakuu wa vyama kutangaza nia zao mapema. Wale wanaotaka kufanya hivyo wasizuiwe bali wanatakiwa kuachia nafasi zao za uongozi wa chama.
   
 2. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  "Mwenye masikio na asikie neno Bams awaambia CHADEMA" Well said Mzalendo wa kweli.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Umesomeka Mkuu..
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Bams umejipanga vizuri, umenena vizuri....Well done kamanda.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  tatizo ni kwamba chadema kama walivyo sasa...sidhani kama wanaweza kuunda baraza la mawaziri that's their handicap... kuna kama five ppo chadema ambao wanaweza kua viongozi imara na bora sasa baraza la mawaziri ni zaidi ya watu watano...hapo bado hujachagua manaibu waziri...
   
Loading...